Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


𝐌𝐖𝐄𝐍𝐄𝐙𝐈 𝐊𝐄𝐍𝐀𝐍𝐈 𝐀𝐒𝐈𝐌𝐀𝐌𝐈𝐒𝐇𝐀 𝐌𝐒𝐀𝐅𝐀𝐑𝐀 𝐊𝐔𝐒𝐀𝐋𝐈𝐌𝐈𝐀 𝐖𝐀𝐍𝐀𝐍𝐂𝐇𝐈 𝐍𝐀 𝐊𝐈𝐉𝐈𝐖𝐄 𝐂𝐇𝐀 𝐂𝐇𝐀𝐃𝐄𝐌𝐀 𝐀𝐑𝐔𝐒𝐇𝐀 𝐌𝐉𝐈𝐍𝐈

alternative

Katika kuonesha mfano wa siasa za ustaarabu, umoja na mshikamano wa kitaifa, Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Ndugu Kenani Laban Kihongosi, alisimamisha msafara wake na kusalimiana na wananchi pamoja na vijana waliokuwa katika kijiwe cha CHADEMA jijini Arusha tarehe 06 Juni, 2026. Hatua hiyo imeendelea kuakisi falsafa ya CCM ya kuimarisha amani, kuheshimu tofauti za kiitikadi na kuendeleza mshikamano miongoni mwa Watanzania. Ujumbe mkubwa ukiwa ni kwamba tofauti za kisiasa hazipaswi kuwa sababu ya kugawanyika, bali ziwe chachu ya kujenga hoja na kushindana kwa sera kwa ajili ya maendeleo ya Taifa. Tanzania yetu imejengwa juu ya misingi ya umoja, upendo na amani. Hivyo, jukumu la kila kiongozi na mwananchi ni kuilinda hazina hiyo kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho. “Umoja Wetu ndiyo Nguvu Yetu. Amani Yetu ndiyo Mtaji Wetu.” MTUMISHI WA WOTE Tembelea: www.ccm.or.tz _____________ #KaziNaUtuTunasongaMbele #CCMIpoKazini #MtumishiWaWote #SiasaZaUstaarabu #UmojaNiNguvu

alternative alternative alternative alternative alternative alternative alternative
Habari Nyingine