Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


ZIARA YA RAIS WA MISRI-TANZANIA

alternative

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, Mhe. Abdel Fattah El-Sisi, wameshuhudia utiaji saini wa mikataba na hati za makubaliano ya kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Misri katika sekta za umeme, nishati jadidifu pamoja na masuala ya uchukuzi. Hatua hii inaakisi utekelezaji wa sera na maono ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) chini ya uongozi wa Rais na ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kuimarisha diplomasia ya uchumi, kuvutia uwekezaji na kuendelea kusukuma mbele ajenda ya maendeleo yenye manufaa kwa Watanzania. Hafla hiyo imefanyika Ikulu, Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 18 Julai, 2026. Tembelea: www.ccm.or.tz _______ #KaziNaUtuTunasongaMbele #DiplomasiaYaUchumi #CcmIpoKazini

alternative alternative alternative alternative alternative
Habari Nyingine