Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


𝐑𝐀𝐁𝐈𝐀 𝐀𝐏𝐎𝐊𝐄𝐋𝐄𝐖𝐀 𝐍𝐉𝐎𝐌𝐁𝐄, 𝐀𝐇𝐈𝐌𝐈𝐙𝐀 𝐕𝐈𝐎𝐍𝐆𝐎𝐙𝐈 𝐖𝐀 𝐂𝐂𝐌 𝐊𝐔𝐈𝐒𝐇𝐈 𝐃𝐇𝐀𝐍𝐀 𝐘𝐀 𝐊𝐀𝐙𝐈 𝐍𝐀 𝐔𝐓𝐔 𝐊𝐖𝐀 𝐕𝐈𝐓𝐄𝐍𝐃𝐎

alternative

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Idara ya Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Ndugu Rabia Abdalla Hamid, amepokelewa rasmi katika Ofisi za CCM Mkoa wa Njombe kuanza ziara yake ya kusikiliza na kuzungumza na makundi mbalimbali ya kijamii. Katika ziara hiyo, Ndugu Rabia amewahimiza viongozi wa CCM ngazi zote kuendelea kutekeleza kwa vitendo falsafa ya Kazi na Utu kwa kuwa karibu na wananchi na kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii. Amesema viongozi wanapaswa kugusa maisha ya wananchi kwa kushiriki shughuli za maendeleo, kutembelea na kuwahudumia wenye mahitaji maalum, wazee, pamoja na kushiriki katika shughuli za usafi wa mazingira, masoko, hospitali na maeneo mengine ya kijamii. Aidha, amesisitiza kuwa uimara wa CCM unatokana na viongozi wake kuwa sehemu ya jamii na kushiriki kikamilifu katika kutatua changamoto zinazowagusa wananchi. Tembelea: www.ccm.or.tz ______ #KaziNaUtuTunasongaMbele #TabasamuKwaKilaMtanzania #CCMIpokazini

alternative alternative alternative alternative alternative alternative alternative alternative alternative alternative
Habari Nyingine