Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


𝐑𝐀𝐁𝐈𝐀: 𝐂𝐂𝐌 𝐈𝐍𝐀𝐓𝐇𝐀𝐌𝐈𝐍𝐈 𝐉𝐀𝐒𝐇𝐎 𝐋𝐀 𝐊𝐈𝐋𝐀 𝐌𝐓𝐀𝐍𝐙𝐀𝐍𝐈𝐀

alternative

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Idara ya Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Ndugu Rabia Abdalla Hamid, amesema CCM inathamini mchango na jasho la kila Mtanzania katika kujiletea maendeleo kupitia shughuli mbalimbali za kiuchumi. Akizungumza na makundi mbalimbali ya kijamii mkoani Lindi, Ndugu Rabia amesema Serikali ya CCM itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wakulima, wavuvi, wafugaji, wafanyabiashara na wajasiriamali ili waweze kunufaika zaidi na shughuli zao. Amesema dhamira ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ni kuhakikisha maendeleo yanawagusa Watanzania wote na kwamba fursa za kiuchumi zinaendelea kuimarishwa kwa manufaa ya wananchi. Tembelea: www.ccm.or.tz ____________ #KaziNaUtuTunasongaMbele #CCMKimbilioLaWananchi #TabasamuKwaKilaMtanzania #RabiaAbdallaHamid

alternative alternative alternative alternative alternative alternative alternative alternative
Habari Nyingine