Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


𝐀𝐑𝐔𝐌𝐄𝐑𝐔 𝐘𝐀𝐒𝐈𝐊𝐈𝐀 𝐖𝐈𝐓𝐎 𝐖𝐀 𝐊𝐔𝐋𝐈𝐍𝐃𝐀 𝐌𝐀𝐀𝐃𝐈𝐋𝐈 𝐍𝐀 𝐇𝐀𝐊𝐈 𝐙𝐀 𝐖𝐀𝐓𝐎𝐓𝐎

alternative

Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Ndugu Kenani Laban Kihongosi, amesisitiza umuhimu wa jamii kushikamana katika kupambana na vitendo vya ubakaji, ulawiti na mmomonyoko wa maadili vinavyoathiri ustawi wa watoto na maendeleo ya Taifa. Akizungumza na wananchi wa Shina Na. 7, Tawi la Moivo wilayani Arumeru, Ndugu Kihongosi amesema hakuna jamii inayoweza kufikia maendeleo ya kweli ikiwa itashindwa kulinda usalama, utu na haki za watoto. Ameeleza kuwa malezi bora, uwajibikaji wa wazazi na ushirikiano wa jamii ni nguzo muhimu katika kujenga kizazi chenye maadili, nidhamu na uzalendo. Aidha, amevitaka vyombo husika, viongozi wa dini, walimu na wananchi kwa ujumla kuendelea kutoa elimu, kufichua vitendo vya ukatili na kuchukua hatua stahiki dhidi ya wahalifu ili kulinda mustakabali wa watoto wa Tanzania. MTUMISHI WA WOTE Tembelea: www.ccm.or.tz ________ #KaziNaUtuTunasongaMbele #CCMIpoKazini #MtumishiWaWote #LindaWatoto

alternative alternative alternative alternative
Habari Nyingine