Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


𝐌𝐖𝐄𝐍𝐄𝐙𝐈 𝐊𝐄𝐍𝐀𝐍𝐈 𝐀𝐙𝐈𝐍𝐃𝐔𝐀 𝐒𝐇𝐈𝐍𝐀 𝐋𝐀 𝐖𝐀𝐊𝐄𝐑𝐄𝐊𝐄𝐓𝐖𝐀 𝐌𝐋𝐀𝐍𝐃𝐄𝐆𝐄, 𝐊𝐈𝐋𝐎𝐒𝐀-𝐈𝐑𝐈𝐍𝐆𝐀

alternative

Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Ndugu Kenani Laban Kihongosi, ameendelea kuimarisha Chama ngazi ya mashina kwa kuzindua Shina la Wakereketwa la Maafisa wa Usafirishaji wa Abiria na Mizigo Mlandege, Tawi la Kilosa mkoani Iringa. Akizungumza na wanachama wa shina hilo, Ndugu Kihongosi amepongeza hatua ya kuanzishwa kwa shina lenye wanachama zaidi ya 100 wanaoshiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo na ujenzi wa Chama. Amesisitiza kuwa CCM itaendelea kuwa karibu na wananchi kwa kusikiliza changamoto zao na kuzitafutia ufumbuzi kupitia Serikali. Wanachama wa shina hilo wamewasilisha changamoto mbalimbali, ikiwemo miundombinu, maeneo ya mapumziko kwa abiria pamoja na masuala ya usalama. Ndugu Kihongosi ameahidi kuziwasilisha kwa mamlaka husika ili zipatiwe ufumbuzi kwa manufaa ya wananchi na wadau wa sekta ya usafirishaji. "CCM ni daraja la wananchi na Serikali; tunasikiliza, tunawakilisha na tunatatua changamoto za wananchi kwa vitendo," amesema Ndugu Kenani Laban Kihongosi. Tembelea: www.ccm.or.tz _______ #KaziNaUtuTunasongaMbele #CCMIpoKazini #Iringa

alternative alternative alternative alternative alternative
Habari Nyingine