Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


𝐑𝐀𝐈𝐒 𝐒𝐀𝐌𝐈𝐀: 𝐌𝐀𝐑𝐈𝐃𝐇𝐈𝐀𝐍𝐎 𝐍𝐈 𝐌𝐒𝐈𝐍𝐆𝐈 𝐖𝐀 𝐌𝐀𝐁𝐎𝐑𝐄𝐒𝐇𝐎 𝐘𝐀 𝐊𝐀𝐓𝐈𝐁𝐀

alternative

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, jana Julai 30, 2026, alikutana na viongozi wa vyama 18 vya siasa Ikulu, Dar es Salaam, ambapo alisisitiza umuhimu wa kuendeleza maridhiano ya kisiasa kuelekea maboresho ya Katiba kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za nchi. Rais Samia alisema Serikali itaendeleza majadiliano na vyama vya siasa ili kujenga mwafaka kuhusu masuala muhimu ya Taifa, huku akibainisha kuwa hatua zote za mchakato wa Katiba zitazingatia maslahi mapana ya Taifa. Aidha, alisema Serikali itaendelea kukutana na viongozi wa vyama vya siasa angalau mara tatu kwa mwaka ili kuimarisha mazungumzo na uelewano. Pia alieleza kuwa uchumi wa nchi uliendelea kukua kwa asilimia 6 mwaka uliopita, huku ukuaji wa asilimia 6.3 ukitarajiwa mwaka huu. Tembelea: www.ccm.or.tz _______ #KaziNaUtuTunasongaMbele #CCMIpoKazini #TanzaniaKwanza

alternative alternative alternative alternative alternative alternative alternative alternative
Habari Nyingine