Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


𝐂𝐂𝐌 𝐘𝐀𝐔𝐍𝐆𝐀 𝐌𝐊𝐎𝐍𝐎 𝐖𝐀𝐍𝐀𝐍𝐂𝐇𝐈 𝐖𝐀 𝐍𝐉𝐎𝐌𝐁𝐄 𝐊𝐖𝐀 𝐊𝐀𝐙𝐈 𝐙𝐀 𝐔𝐙𝐀𝐋𝐈𝐒𝐇𝐀𝐉𝐈 𝐌𝐀𝐋𝐈

alternative

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Idara ya Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Ndugu Rabia Abdalla Hamid, ameendelea na ziara yake ya kusikiliza, kuzungumza na kutatua changamoto za makundi mbalimbali ya kijamii mkoani Njombe. Katika ziara hiyo, Ndugu Rabia alitembelea Soko la Wakulima wa Njombe na kuzungumza na wajasiriamali pamoja na wafanyabiashara mbalimbali, ambapo aliwapongeza kwa juhudi zao katika uzalishaji mali na kukuza uchumi wa Mkoa na Taifa. Amesema CCM chini ya Mwenyekiti wake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, itaendelea kuboresha huduma za kijamii, miundombinu na upatikanaji wa masoko ili kuwawezesha wananchi kunufaika zaidi na shughuli zao za kiuchumi. Njombe, Tanzania 18 Juni, 2026 Tembelea: www.ccm.or.tz _______ #KaziNaUtuTunasongaMbele #CCMKimbilioLaWananchi #CCMIpoKazini

alternative alternative alternative alternative alternative alternative alternative alternative alternative alternative
Habari Nyingine