Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


𝐍𝐃𝐆 𝐑𝐀𝐁𝐈𝐀 𝐀𝐏𝐎𝐊𝐄𝐋𝐄𝐖𝐀 𝐑𝐔𝐕𝐔𝐌𝐀, 𝐀𝐇𝐈𝐌𝐈𝐙𝐀 𝐔𝐌𝐎𝐉𝐀 𝐍𝐀 𝐌𝐒𝐇𝐈𝐊𝐀𝐌𝐀𝐍𝐎 𝐍𝐃𝐈𝐎 𝐍𝐆𝐔𝐕𝐔 𝐘𝐀 𝐂𝐂𝐌

alternative

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Idara ya Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Ndugu Rabia Abdalla Hamid, amepokelewa rasmi katika Mkoa wa Ruvuma kuanza ziara yake ya kukutana na kuzungumza na makundi mbalimbali ya kijamii. Akizungumza mara baada ya kuwasili, Ndugu Rabia amesisitiza kuwa umoja na mshikamano ndio msingi wa uimara na mafanikio ya Chama Cha Mapinduzi. Amewahimiza viongozi na wanachama wa CCM kuendelea kudumisha umoja, ushirikiano na mshikamano katika kukijenga na kukitetea Chama. Aidha, amewataka wanachama kuendelea kuwa na fikra chanya na kujitolea katika kusimamia maslahi ya wananchi pamoja na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM. Tembelea: www.ccm.or.tz _____ #KaziNaUtuTunasongaMbele #TabasamuKwaKilaMtanzania #CCMIpoKazini

alternative alternative alternative alternative alternative alternative alternative alternative alternative
Habari Nyingine