Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


𝐑𝐀𝐁𝐈𝐀: 𝐂𝐂𝐌 𝐇𝐀𝐈𝐓𝐀𝐕𝐔𝐌𝐈𝐋𝐈𝐀 𝐔𝐙𝐄𝐌𝐁𝐄, 𝐕𝐈𝐎𝐍𝐆𝐎𝐙𝐈 𝐖𝐀𝐖𝐀𝐉𝐈𝐁𝐈𝐊𝐄 𝐊𝐔𝐓𝐀𝐓𝐔𝐀 𝐂𝐇𝐀𝐍𝐆𝐀𝐌𝐎𝐓𝐎 𝐙𝐀 𝐖𝐀𝐍𝐀𝐍𝐂𝐇𝐈

alternative

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Idara ya Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Ndugu Rabia Abdalla Hamid, ameendelea na ziara yake mkoani Ruvuma ya kusikiliza na kutatua changamoto za makundi mbalimbali ya kijamii. Ndugu Rabia amewataka viongozi wa Halmashauri za Wilaya kuhakikisha wanatatua changamoto za wananchi kwa wakati ili kuwaondolea adha ya kusafiri umbali mrefu kwenda katika Ofisi za Wakuu wa Mikoa kufuatilia masuala ambayo yanapaswa kupatiwa ufumbuzi katika ngazi za wilaya. Amesema CCM haitavumilia uzembe wa viongozi wanaoshindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo na kusababisha mrundikano wa changamoto za wananchi. Aidha, amesema CCM chini ya Mwenyekiti wake, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, imedhamiria kuendelea kuwahudumia wananchi kwa vitendo. Ameeleza kuwa ahadi 695 za CCM katika Mkoa wa Ruvuma zitatekelezwa kikamilifu, huku Serikali ikiendelea kutafuta masoko ya uhakika ili kila mwananchi apate kipato bora na cha uhakika. Tembelea: www.ccm.or.tz ________ #KaziNaUtuTunasongaMbele #CCMTabasamuLaKilaMtanzania #CCMKimbilioLaKilaMtanzania #CCMIpokazini.

alternative alternative alternative alternative alternative alternative alternative alternative alternative alternative
Habari Nyingine