Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


𝐌𝐈𝐊𝐎𝐏𝐎 𝐘𝐀 𝐀𝐒𝐈𝐋𝐈𝐌𝐈𝐀 𝟏𝟎% 𝐘𝐀𝐂𝐇𝐎𝐂𝐇𝐄𝐀 𝐔𝐂𝐇𝐔𝐌𝐈 𝐖𝐀 𝐌𝐀𝐊𝐔𝐍𝐃𝐈 𝐌𝐀𝐀𝐋𝐔𝐌

alternative

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Idara ya Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Ndugu Rabia Abdalla Hamid, ametembelea vikundi vya ufugaji wa kuku pamoja na vikundi vya bodaboda na bajaji vilivyonufaika na mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya Halmashauri mkoani Ruvuma. Katika ziara hiyo, Ndugu Rabia amejionea namna mikopo hiyo ilivyochochea ukuaji wa shughuli za kiuchumi, kuongeza kipato na kuboresha maisha ya wanufaika katika makundi mbalimbali ya kijamii. Aidha, wanufaika wa mikopo hiyo wamempongeza Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kuweka mazingira wezeshi ya kuwawezesha wananchi kiuchumi kupitia mikopo hiyo. Pia wamewataka vijana, wanawake na watu wenye mahitaji maalum kuendelea kuchangamkia fursa zinazotolewa na Serikali sikivu ya CCM ili kujiletea maendeleo, kuongeza kipato na kuimarisha ustawi wa familia na jamii kwa ujumla. Tembelea: www.ccm.or.tz _______ #KaziNaUtuTunasongaMbele #CCMKimbilioLaWananchi #CCMTabasamuLaKilaMtanzania #CCMIpokazini.

alternative alternative alternative alternative alternative alternative alternative alternative alternative
Habari Nyingine