CHAMA Chama Cha Mapinduzi(CCM)Zanzibar kimesema kinahitaji viongozi wachapakazi,wazalendo na waadilifu katika kuwatumikia Wananchi ambao ndio wenye nguvu ya mamlaka ya kukiweka madarakani kupitia michakato ya Uchaguzi wa kidemokrasia
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt.Mohamed Said Dimwa wakati akikabidhi nyumba iliyojengwa na Mbunge wa Jimbo la Magomeni Mhe.Mwanakhamis Kassim Said kwa Mwananchi wa shehia ya Nyerere ndugu Mussa Juma Hemed huko Magomeni Zanzibar.
Dkt.Dimwa,alisema viongozi wanaotekekeza kwa vitendo ahadi walizoahidi kupitia Uchaguzi mkuu uliopita wanaenda sambamba na malengo ya Chama Cha Mapinduzi katika kuwatumikia Wananchi na kwamba wanatakiwa kuongeza Kasi ya utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi Ili CCM ishinde kwa ngazi mbali mbali katika Uchaguzi mkuu ujao.
Alieleza kuwa Wananchi wanahitaki kuona maendeleo katika majimbo yao ikiwemo huduma Bora za maji safi na salama,hospitali,skuli,barabara zenye ubora,umeme na makaazi bora ya kuishi.
Katika maelezo yake Dkt.Dimwa,alisema kuwa CCM inaendelea kutathmini na kufuatilia utendaji wa kila kiongozi wakiwemo madiwani,Wabunge na wawakilishi kwa lengo la kujiridhisha kama wanakidhi vigezo vya kuendeleza kuongoza kuwatumikia wananchi.
Kupitia hafla hiyo alimpongeza Mbunge huyo wa Jimbo la Magomeni kwa juhudi zake za kuhakikisha Mwananchi huyo anapata nyumba nzuri ya kuishi na kwamba sio kuwa ametekeleza ilani ya CCM pia ametoa sadaka kubwa itanayoongeza baraka kwa Mwenyezi Mungu.
Alisema kuwa Chama Cha Mapinduzi hakitowavumilia baadhi ya viongozi wasiotekeleza ilani ya Uchaguzi ya CCM badala yake kitatoa nafasi za kuendeleza kuongoza kutokana na uchapakazi wa kiongozi na sio umaarufu wake.
"Tunapowatumikia Wananchi kwa uadilifu kwa kutatua changamoto zao inasadia kutengeneza mazingira bora ya ushindi wa CCM wa ngazi mbali mbali katika Uchaguzi Mkuu ujao.
Nitumie nafasi hii tu kuwaeleza kuwa CCM kwa awamu hii ya Mwenyekiti wetu Rais Dkt.Samia npamoja na Rais Dk.Mwinyi,haitomuonea mtu bali tutaenda na kutoa kipaumbele kwa wale tuliolima nao mazao juani ndio tutakaovuna na kula nao kivulini.",alisisitiza Dkt.Dimwa.
Alisemea tabia za baadhi ya makada na wanachama kupita majimbo kuanza kampeni za kuharibu sifa za viongozi waliopo madarakani kwa sasa na kueleza kuwa viongozi hao waachwe na kupewa nafasi za kuwatumikia Wananchi na kwamba wanaotaka kuwania Uongozi wasubiri muda wa Uchaguzi ufike mwaka 2025.
Naye Mbunge wa Jimbo la Magomeni Zanzibar Mhe.Mwanakhamis Kassim Said, alipongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais wa Zanzibar Dk.Hussein Mwinyi kwa utendaji wao mzuri wa kuwaletea wananchi maendeleo.
Alisema maendeleo yaliyopatikana katika Jimbo Hilo yametokana na ushirikiano mzuri ulipo baina ya wanachama,viongozi wa ngazi za mashina hadi Mkoa ikiwemo Kamati ya Jimbo na Wananchi wote kwa ujumla.
Akizungumzia ujenzi wa nyumba ya Mwananchi huyo ndugu Mussa Juma,alisema imegharimu kiasi cha shilingi milioni 17,357,000.
Mhe.Mwanakhamis,amesema lengo la kujenga nyumba hiyo ni kuhakikisha Mwananchi huyo anaishi katika maakazi Bora kama ilivyo kwa Wananchi wengine wa Jimbo hilo.
MAFURIKO YA WANANCHI WA SIHA KWENYE MKUTANO MKUBWA WA HADHARA
29-05-2026
MAPOKEZI YA KATIBU MWENEZI WA CCM NDUGU KENANI L KIHONGOSI MKOANI KILIMANJARO
29-05-2026
🔰 𝐊𝐈𝐇𝐎𝐍𝐆𝐎𝐒𝐈 𝐀𝐖𝐀𝐒𝐈𝐋𝐈 𝐊𝐖𝐀 𝐊𝐈𝐒𝐇𝐈𝐍𝐃𝐎 𝐊𝐈𝐋𝐈𝐌𝐀𝐍𝐉𝐀𝐑𝐎
29-05-2026
CCM INAWATAKIA HERI YA SIKUKUU YA EID AL ADHA
29-05-2026
🔰VYAMA VYA UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA VYAIMARISHA MSHIKAMANO, DKT. DIMWA AHITIMISHA MAFUNZO MAALUM
29-05-2026
KATIBU WA NEC, ITIKADI, UENEZI NA MAFUNZO CCM TAIFA NDUGU KENANI KIHONGOSI AMNADI MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA ISIMANI EMMANUELA KAGANDA MTATIFIKOLO
29-05-2026
MUENDELEZO WA MAFUNZO YA VIONGOZI KATIKA SHULE YA UONGOZI YA MWALIMU JULIUS NYERERE – KIBAHA
29-05-2026
SIKU YA KWANZA YA MAFUNZO KATIKA SHULE YA UONGOZI YA MWALIMU JULIUS NYERERE LEADERSHIP SCHOOL.
29-05-2026
UFUNGUZI WA MAFUNZO YA VYAMA SITA RAFIKI VYA UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA
29-05-2026
MHE. DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA MJUMBE WA KAMATI KUU YA CPC, KOMREDI LIU HAIXING IKULU DAR ES SALAAM
29-05-2026
KIKAO CHA KAMATI KUU YA HALMASHAURI KUU YA CCM
29-05-2026
CCM NA FRELIMO KUIMARISHA USHIRIKIANO WA KIUCHUMI
29-05-2026
UZINDUZI WA JENGO LA MAKAO MAKUU YA ULINZI WA TAIFA
29-05-2026
CCM YAIPA POLE MSUMBIJI KWA KUKUMBWA NA MAFURIKO
29-05-2026
INJINI YA CHAMA CHA MAPINDUZI IPO MASHINANI; DKT.MIGIRO
29-05-2026
DK.MIGIRO:CCM INAJENGWA KUANZIA NGAZI YA MASHINA SIO MAJUKWAANI.
29-05-2026
𝗞𝗜𝗦𝗛𝗜𝗡𝗗𝗢 𝗖𝗛𝗔 𝗗𝗞𝗧. 𝗠𝗜𝗚𝗜𝗥𝗢 𝗖𝗛𝗔𝗣𝗢𝗞𝗘𝗟𝗘𝗪𝗔 𝗞𝗪𝗔 𝗦𝗛𝗔𝗡𝗚𝗪𝗘 𝗗𝗔𝗥 𝗘𝗦 𝗦𝗔𝗟𝗔𝗔𝗠
29-05-2026
NAIBU KATIBU MKUU WA CCM BARA AMWAKILISHA KATIBU MKUU WA CCM KWENYE MSIBA WA MBUNGE WA JIMBO LA PERAMIHO
29-05-2026
𝗩𝗜𝗝𝗔𝗡𝗔 𝗧𝗨𝗜𝗟𝗜𝗡𝗗𝗘 𝗔𝗠𝗔𝗡𝗜 𝗬𝗔 𝗡𝗖𝗛𝗜 𝗬𝗘𝗧𝗨 - 𝗠𝗪𝗘𝗡𝗘𝗭𝗜 𝗞𝗘𝗡𝗔𝗡𝗜
29-05-2026
DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AONGOZA KIKAO MAALUMU CHA KAMATI KUU YA CCM
29-05-2026