Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


𝐊𝐄𝐍𝐀𝐍𝐈 𝐀𝐒𝐀𝐌𝐁𝐀𝐙𝐀 𝐔𝐏𝐄𝐍𝐃𝐎 𝐖𝐀 𝐀𝐆𝐀𝐏𝐄 𝐊𝐖𝐄𝐍𝐘𝐄 𝐊𝐈𝐉𝐈𝐖𝐄 𝐂𝐇𝐀 𝐂𝐇𝐀𝐃𝐄𝐌𝐀 𝐀𝐑𝐔𝐌𝐄𝐑𝐔

alternative

Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Ndugu Kenani Laban Kihongosi, ameendelea kuonesha mfano wa siasa za ustaarabu kwa kusalimiana na kufanya mazungumzo na wananchi waliokuwa katika kijiwe cha CHADEMA wilayani Arumeru. Akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Arusha, Ndugu Kihongosi amesisitiza kuwa tofauti za vyama vya siasa hazipaswi kuvuruga umoja wa Watanzania. Ameeleza kuwa maendeleo, amani na ustawi wa Taifa ni agenda ya pamoja inayowahusu Watanzania wote bila kujali itikadi zao za kisiasa. Amehimiza kuendelea kujenga Tanzania yenye mshikamano, kuheshimiana na kushindana kwa hoja, huku maslahi ya wananchi yakiwekwa mbele wakati wote. Kwa mujibu wake, Upendo wa Agape ni upendo unaojenga mshikamano, kuunganisha watu, kuimarisha matumaini na kuhamasisha maendeleo kwa kila Mtanzania. KAZI NA UTU, TUNASONGA MBELE. Tembelea: www.ccm.or.tz ____________ #MtumishiWaWote 🙏 #KazinaUtuTunasongaMbele #CCMIpoKazini #KaziInaendelea

alternative alternative alternative alternative alternative alternative alternative alternative alternative alternative
Habari Nyingine