Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


𝐊𝐈𝐇𝐎𝐍𝐆𝐎𝐒𝐈 𝐀𝐀𝐍𝐙𝐀 𝐙𝐈𝐀𝐑𝐀 𝐀𝐑𝐔𝐌𝐄𝐑𝐔 𝐊𝐖𝐀 𝐊𝐔𝐊𝐀𝐆𝐔𝐀 𝐔𝐇𝐀𝐈 𝐖𝐀 𝐂𝐇𝐀𝐌𝐀

alternative

Ziara ya Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Ndugu Kenani Laban Kihongosi, imeanza rasmi Wilaya ya Arumeru kwa kutembelea Shina Na. 8 eneo la Waya na kujionea uhai wa Chama ngazi ya shina. Akizungumza na wanachama na wananchi, Ndugu Kihongosi ameeleza kufurahishwa na uimara wa Chama baada ya kupokea taarifa kuwa uhai wa CCM katika shina hilo umefikia asilimia 100. Aidha, ametoa maelekezo kwa viongozi wa Serikali kuendelea kushughulikia changamoto za wananchi kwa wakati na kwa ufanisi ili kuendelea kuimarisha imani ya wananchi kwa Chama na Serikali yake. Kwa upande wao, wanachama na wananchi wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kutekeleza Ilani ya CCM kupitia miradi mbalimbali ya maendeleo inayogusa maisha ya wananchi. Tembelea: www.ccm.or.tz _____________ #KazinaUtuTunasongaMbele #CCMIpoKazini #KaziInaendelea #Arusha

alternative alternative alternative alternative alternative alternative alternative alternative
Habari Nyingine