Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kutoa mashirikiano kwa Mashirika na Taasisi za kifedha zilizopo nchini ikiwemo Bank ya NMB ili kuimarisha uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla
Hayo yamesemwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla katika FTARI iliyoandaliwa na Bank ya NMB hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Hotel ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege jijini Zanzibar.
Amesema kuwa Mashirika ya kifedha yamekuwa na mchango mkubwa kwa Serikali zote mbili katika kukuza uchumi wa Taifa kwa kutoa misaada mbali mbali kwa Serikali na wananchi kulingana na mahitaji yao.
Mhe. Hemed amesema kuwa Bank ya NMB imekuwa mstari wa mbele katika kuyaunganisha Mashirika mbali mbali hivyo ameutaka uongozi kuendelea kutanua wigo kwa kuongeza matawai mijini na vijijini ili kuwarahisishia wananchi kupata huduma zilizo bora na kwa wakati.
Aidha Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar amesema Serikali na wananchi wameridhishwa na utendaji kazi wa Benk ya NMB kwa kuendana na kasi ya dunia katika kutoa huduma masaa 24 kwa wananchi sambamba na kutoa gawiwo kwa seriali kuu kwa kila mwaka.
Sambamba na hayo Makamu wa pili wa Rais ameutaka uongozi wa NMB Benk kuwa karibu na wananchi na wateja wake katika kutoa huduma zilizo bora ili kuongeza wateja na kukuza biashara nchini.
Hata hivyo Mhe. Hemed ameupongeza uongozi wa Bank ya NMB kwa kuendeleza utamaduni wa kuwafutarisha wateje wao pamoja na watoto mayatima huku wakitaraji kupata fadhila kutoka kwa Mwenyezi Mungu hasa kwa kipindi hichi cha mwezi mtukufu wa Ramadhan.
Nae Mtendaji mkuu wa Bank ya NMB Tanzania Bi. RUTH ZAIKUNA amesema Bank ya NMB imekuwa nautamaduni wa kuungana na wateja wake na wananchi kwa ujumla katika mambo mbali mbali ya kijamii ikiwemo Kuwafutarisha kila ifikapo mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Bi Ruth amesema kuwa lengo la Ftari hio ni kukaa na wateja wao karibu katika kudumisha umoja, mshikamano na upendo baina ya Uongozi, wafanya kazi wa wateja wao ili kukuza biashara na kupiga hatua kimaendeleo.
Amesema kuwa kwa mwaka huu Bank ya NMB imeamua kuwaalika watoto yatima kwenye ftari hio kwa lengo la kuwafanya watoto hao kujiona na wao ni sawa na watoti wengine na Taifa halijawatenga kwa kuondokewa na wazazi wao
MAFURIKO YA WANANCHI WA SIHA KWENYE MKUTANO MKUBWA WA HADHARA
30-05-2026
MAPOKEZI YA KATIBU MWENEZI WA CCM NDUGU KENANI L KIHONGOSI MKOANI KILIMANJARO
30-05-2026
🔰 𝐊𝐈𝐇𝐎𝐍𝐆𝐎𝐒𝐈 𝐀𝐖𝐀𝐒𝐈𝐋𝐈 𝐊𝐖𝐀 𝐊𝐈𝐒𝐇𝐈𝐍𝐃𝐎 𝐊𝐈𝐋𝐈𝐌𝐀𝐍𝐉𝐀𝐑𝐎
30-05-2026
CCM INAWATAKIA HERI YA SIKUKUU YA EID AL ADHA
30-05-2026
🔰VYAMA VYA UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA VYAIMARISHA MSHIKAMANO, DKT. DIMWA AHITIMISHA MAFUNZO MAALUM
30-05-2026
KATIBU WA NEC, ITIKADI, UENEZI NA MAFUNZO CCM TAIFA NDUGU KENANI KIHONGOSI AMNADI MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA ISIMANI EMMANUELA KAGANDA MTATIFIKOLO
30-05-2026
MUENDELEZO WA MAFUNZO YA VIONGOZI KATIKA SHULE YA UONGOZI YA MWALIMU JULIUS NYERERE – KIBAHA
30-05-2026
SIKU YA KWANZA YA MAFUNZO KATIKA SHULE YA UONGOZI YA MWALIMU JULIUS NYERERE LEADERSHIP SCHOOL.
30-05-2026
UFUNGUZI WA MAFUNZO YA VYAMA SITA RAFIKI VYA UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA
30-05-2026
MHE. DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA MJUMBE WA KAMATI KUU YA CPC, KOMREDI LIU HAIXING IKULU DAR ES SALAAM
30-05-2026
KIKAO CHA KAMATI KUU YA HALMASHAURI KUU YA CCM
30-05-2026
CCM NA FRELIMO KUIMARISHA USHIRIKIANO WA KIUCHUMI
30-05-2026
UZINDUZI WA JENGO LA MAKAO MAKUU YA ULINZI WA TAIFA
30-05-2026
CCM YAIPA POLE MSUMBIJI KWA KUKUMBWA NA MAFURIKO
30-05-2026
INJINI YA CHAMA CHA MAPINDUZI IPO MASHINANI; DKT.MIGIRO
30-05-2026
DK.MIGIRO:CCM INAJENGWA KUANZIA NGAZI YA MASHINA SIO MAJUKWAANI.
30-05-2026
𝗞𝗜𝗦𝗛𝗜𝗡𝗗𝗢 𝗖𝗛𝗔 𝗗𝗞𝗧. 𝗠𝗜𝗚𝗜𝗥𝗢 𝗖𝗛𝗔𝗣𝗢𝗞𝗘𝗟𝗘𝗪𝗔 𝗞𝗪𝗔 𝗦𝗛𝗔𝗡𝗚𝗪𝗘 𝗗𝗔𝗥 𝗘𝗦 𝗦𝗔𝗟𝗔𝗔𝗠
30-05-2026
NAIBU KATIBU MKUU WA CCM BARA AMWAKILISHA KATIBU MKUU WA CCM KWENYE MSIBA WA MBUNGE WA JIMBO LA PERAMIHO
30-05-2026
𝗩𝗜𝗝𝗔𝗡𝗔 𝗧𝗨𝗜𝗟𝗜𝗡𝗗𝗘 𝗔𝗠𝗔𝗡𝗜 𝗬𝗔 𝗡𝗖𝗛𝗜 𝗬𝗘𝗧𝗨 - 𝗠𝗪𝗘𝗡𝗘𝗭𝗜 𝗞𝗘𝗡𝗔𝗡𝗜
30-05-2026
DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AONGOZA KIKAO MAALUMU CHA KAMATI KUU YA CCM
30-05-2026