Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


𝐑𝐀𝐈𝐒 𝐒𝐀𝐌𝐈𝐀 𝐀𝐓𝐔𝐍𝐔𝐊𝐈𝐖𝐀 𝐒𝐇𝐀𝐇𝐀𝐃𝐀 𝐘𝐀 𝐇𝐄𝐒𝐇𝐈𝐌𝐀 𝐔𝐑𝐔𝐒𝐈

alternative

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametunukiwa Shahada ya Heshima ya Uzamivu (Honoris Causa) na Chuo Kikuu cha Urafiki wa Watu wa Urusi (RUDN), ikiwa ni kutambua mchango wake katika uongozi, maendeleo ya jamii na kuendeleza sekta ya elimu. Akizungumza baada ya kupokea heshima hiyo, Rais Samia amesema tuzo hiyo si yake binafsi bali ni ya walimu, wanafunzi, wazazi na wote wanaoamini kuwa elimu ni msingi wa maendeleo ya watu na mataifa. Rais Samia amesisitiza umuhimu wa elimu katika kuandaa jamii kukabiliana na mabadiliko ya dunia ya sasa, hususan katika maeneo ya sayansi, teknolojia na ubunifu, akieleza kuwa ushirikiano wa kimataifa ni muhimu ili mataifa yaendelee kunufaika na maendeleo hayo. Hii ni miongoni mwa shahada za heshima ambazo Rais Samia ameendelea kutunukiwa kutoka vyuo vikuu mbalimbali duniani kutokana na mchango wake katika maendeleo, uongozi na ustawi wa jamii. _______________ #KazinaUtuTunasongaMbele #SamiaSuluhuHassan #CCMIpoKazini l #ElimuKwanza

alternative alternative alternative alternative alternative alternative alternative alternative alternative alternative
Habari Nyingine