KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Balozi Dkt.Emmanuel Nchimbi,amesema maendeleo yaliyofikiwa nchini yametokana na juhudi kubwa za kiutendaji zilizoasisiwa na Wazee wa Chama hicho waliohudumu kwa bidii na maarifa katika sekta za umma na binafsi
Kauli hiyo imeitoa katika ziara yake siku moja wakati akizungumza na kujitambulisha kwa Mabaraza ya Wazee wa CCM wa Mikoa ya Kaskazini na Kusini Pemba huko ukumbi wa Makonyo.
Balozi Dkt.Nchimbi,alisema CCM inaendelea kuimarika kisiasa,kijamii na kiuchumi kutokana na misingi mizuri iliyowekwa na Wazee wa Chama hicho enzi za utumishi wao toka walipoviunganisha Vyama vya ASP na TANU na kuzaliwa kwa CCM mwaka 1977.
Alisema wazee hao wamefanya kazi kubwa ya kuasisi Mapinduzi ya Zanzibar na Muungano wa mwaka 1964 kwa dhamira za kuikomboa nchi kutoka katika mikono ya kisultani na kikoloni.
Katika maelezo yake Dkt.Nchimbi,alisema kuwa CCM inatambua mchango mkubwa wa wazee wa Chama hicho kwa juhudi zao kubwa za kuitumikia nchi kwa uadilifu jambo ambalo ndio kielelezo cha kifikia maendeleo endelevu yalipo nchini.
Alisema lengo la ziara hiyo ni kukutana na wazee hao ili kubadilishana nao mawazo pamoja na kusikiliza changamoto,ushauri na mapendekezo yao juu ya kuimarisha masuala mbalimbali ya kisiasa ndani ya Chama Cha Mapinduzi.
“Tunathamini juhudi zenu kwani enzi zenu mlitumikia nchi kwa juhudi kubwa mkaanzisha Chama Cha Mapinduzi na kuweka misingi imara inayotuongoza hadi hivi sasa hivyo nakuombeni muendelee kutushauri na kutuelekeza pale mtakapoona tunaenda kinyume na misingi hiyo”,alisema Dkt.Nchimbi.
Balozi Dkt.Nchimbi,alikemea vitendo vya ubaguzi wa kiitikadi,kidini na kikabila na kwamba vitendo visipokemewa vinaweza kuingiza nchi katika machafuko ya kisiasa.
Katibu Mkuu huyo Dkt.Nchimbi,alipongeza hatua kubwa ya mafanikio iliyofikiwa na Serikali ya awamu na nan echini ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Mwinyi katika nyanja za kisiasa,kiuchumi na kijamii.
Pamoja na hayo aliwasihi Wanachama wa CCM na wananchi kwa ujumla kuendelea kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan ili afikie maono ya kuongoza nchi kwa ufanisi zaidi.
Naye Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt.Mohamed Said Dimwa,amesema kupitia kitabu cha taratibu za sehemu ya wazee wa CCM toleo la 2019 ibara ya 10(2) inafafanua kuwa wazee ni hazina kubwa ya busara,hekima,uzoefu wa kuendesha shughuli za Chama na maendeleo ya nchi.
Dkt.Dimwa,alieleza kuwa CCM Zanzibar ipo imara na itaendelea kutekeleza siasa za kistaarabu zinazozingatia ushindani wa sera kwa vitendo huku ikijipanga kuhakikisha inashinda kwa kishindo katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2025.
Kwa upande wake Katibu wa Wazee wa CCM Mkoa wa Kusini Pemba,Bi.Hanuna Ibrahim Masoud,amesema wamefurahishwa na uteuzi wa Katibu Mkuu huyo wa CCM Dkt.Nchimbi kwani ni kiongozi mchapakazi,mbunifu,mzalendo na anayekijua vizuri Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake.
DKT SAMIA:TUNAFANYA UCHAGUZI KWA FEDHA ZETU WENYEWE
05-11-2025
MGOMBEA URAIS KUPITIA CCM DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA MANYARA
05-11-2025
π¨ππππ£πππππ πͺπ πππ§. π¦ππ ππ π¨π ππππ§π ππ ππ‘π ππͺπ πͺππ£ππ‘πππ‘π, πͺππππ¨ππππ πππ
πππ©πππͺ ππ πͺπͺ πΏπ π©. πππππ§π€ ππ¬ππ₯π€π ππ πππ€π£ππ€π―π π¬π πΎππΌπΏπππΌ π£π πΌπΎπ
05-11-2025
πππ§. π¦ππ ππ ππ§π¨π π‘πππ‘π π¬π ππ₯πππ π¬π ππππ’π π
05-11-2025
KATIBU MKUU WA CCM, BALOZI DKT. ASHA-ROSE MIGIRO AKUTANA NA RAIS MWINYI – ZANZIBAR
05-11-2025
ILANI YA UCHAGUZI YA CCM 2025-2030
05-11-2025
WASIRA:CCM HATUKATI MGOMBEA ILA TUNATEUA WACHACHE KATI YA WENGI
05-11-2025
WANACHAMA 280 WA CHADEMA WATIMKIA CCM
05-11-2025
BALOZI NCHIMBI: MAONI YOYOTE KUHUSU AMANI YA TANZANIA HAYATAPUUZWA
05-11-2025
π¦ππ₯πππππ π¬π π₯πππ¦ πππ§. π¦ππ ππ ππ ππͺπππ ππππ π π¬π π πππ‘πππππ’ ππππ π¦ππππ π¨ - ππ£π. ππ π’π¦ π ππππππ
05-11-2025
MAKALLA: BARABARA YA MPWAPWA NJIAPANDA KONGWA KUJENGWA LAMI
05-11-2025
BALOZI NCHIMBI AWASILI ARUSHA
05-11-2025
TAARIFA KWA UMMA
05-11-2025
UCHAGUZI MKUU SIO AJALI-WASIRA
05-11-2025
πͺπππ¨π ππ π π¦ππππππ¨π π©ππ’π‘ππ’ππ ππππππππ ππͺππ‘π¬π ππ¨π₯π ππ π ππ’π‘π - (π ππ) πππ©π¨
05-11-2025
MONGELLA AONGOZA MAZISHI YA KADA WA CCM JIJINI MWANZA
05-11-2025
ASIYETII SHERIA, KATIBA NA KUWA TAYARI KUUA KWA MASLAHI BINAFSI HUO NI UGAIDI’
05-11-2025
πππ π¬ππ¦ππ¦ππ§πππ πͺπππ’π πππ ππ¨πππππππͺπ ππͺπ ππ¨πππ‘πππ§ππ π¨πͺπππ’, π¨πππππ‘ππ’ π‘π π¨πππππππ¨, π¬ππππ ππ π πππ¨π‘ππ - πππ. πππ©π¨
05-11-2025
KAENI KIMYA KAMA HAMJUI NCHI ILIKOTOKA - WASIRA
05-11-2025
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefungua kiwanda cha kutengeneza mabomba ya maji na uchakataji pamba cha MOLI Oil Mills Co. Ltd kilichopo Bariadi Mkoani Simiyu tarehe 16 Juni, 2025.
05-11-2025