RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI, MHE. DK. HUSSEIN ALI MWINYI AMEHIMIZA USHIRIKIANO WA KIUTENDAJI BAINA YA TAASISI ZA SERIKALI YA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA (SMT) NA ZA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR (SMZ) ILI KUENDELEZA MAGEUZI YA UCHUMI NA UWEKEZAJI.
Dk. Mwinyi aliyasema hayo Ikulu, Zanzibar alipozungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo na ujumbe wake wa watu 20 waliofika kujitambulisha.
Alisema, SMZ na SMT wana ushirikiano mkubwa kwenye utendaji wa taasisi zao na kueleza, mara kadhaa taasisi ya hazina ya Zanzibar imekua ikipata ushirikiano mzuri na ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania pia Mamlaka ya Uwekezaji Zanzibar, ZIPA na TIC pamoja na taasisi nyengine za pande mbili hizo za Muungano hushirikiana katika kuboresha maendeleo kwa ustawi wa uchumi wa taifa la Tanzania na watu wake.
Rais Dk. Mwinyi pia alitumia fursa hiyo, kuwapongeza na kuushukuru ujumbe huo kwa utayari wao kwa kuendelea kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa mawazo ya mageuzi yanayolenga kujenga uchumi wa wananchi wa pande zote mbili za Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia ushirikiano uliopo baina ya tasisi za serikali mbili hizo, zikiwemo Mamlaka ya Bandari, Ofisi ya Msajili Hazina, Mamlaka za Uwekezaji pamoja na Tume ya Mipango ya Taifa.
“Niwapongeze kwa mawazo haya ya mageuzi, ni vizuri mara zote tuwe kunafikiria kujenga uchumi wetu kupitia taasisi zetu” alipongeza Rais Dk. Mwinyi.
Akiizungumzia bandari Jumuishi ya Mangapwaji Rais Dk. Mwinyi, alimueleza Waziri huyo kwamba SMZ imepania kuleta mageuzi makubwa ya uchumi kupitia bandari hiyo, ambayo kutokana na maumbile ya kisiwa cha Zanzibar kilivyo, inakusudiwa kujumuisha shughuli zote za badari mbali na kupakia na kushushia abiria na mizigo lakini kuruhusu meli mbalimbali za kimataifa zitakazoleta mageuzi makubwa ya biashara, uwekezaji na kuimarisha uchumi wa buluu.
Naye, Waziri Mkumbo alimuahidi Rais Dk. Mwinyi ushirikiano wa hali ya juu katika kuujenga uchumi wa nchi hasa kuelekea maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano wa Tanzania na ya Mapinduzi ya Zanzibar wamejipanga kuleta mabadiliko makubwa ya uchumi.
Alisema, mbali na mambo mengine lakini kupitia mradi wa Bagamoyo, ujio wa Zanzibar umewaletea tija na ufanisi mkubwa kwenye utendaji wao hasa kwa taasisi wanazoshirikiana nazo kiutendaji kwani watajifunza mengi kupitia bandari jumishi ya Mangapwani pamoja na taasisi nyengine wanazoshirikiana nazo kiutendaji.
Ujumbe ulioongozana na Waziri Prof. Kitila umemjumuisha Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Dk. Tausi Kida, Msajili wa Hazina Bara, Nehemia Mchechu, Katibu wa Tume ya Mipango Lawrence Mafuru, Mkurugenzi Mkuu EPZA Charles Itembe, Mkurugenzi Mkuu TIC Gilead Teri na Mkurugenzi wa Miundombinu TPA Dk. Hussein Lufunyo.
DKT SAMIA:TUNAFANYA UCHAGUZI KWA FEDHA ZETU WENYEWE
05-11-2025
MGOMBEA URAIS KUPITIA CCM DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA MANYARA
05-11-2025
π¨ππππ£πππππ πͺπ πππ§. π¦ππ ππ π¨π ππππ§π ππ ππ‘π ππͺπ πͺππ£ππ‘πππ‘π, πͺππππ¨ππππ πππ
πππ©πππͺ ππ πͺπͺ πΏπ π©. πππππ§π€ ππ¬ππ₯π€π ππ πππ€π£ππ€π―π π¬π πΎππΌπΏπππΌ π£π πΌπΎπ
05-11-2025
πππ§. π¦ππ ππ ππ§π¨π π‘πππ‘π π¬π ππ₯πππ π¬π ππππ’π π
05-11-2025
KATIBU MKUU WA CCM, BALOZI DKT. ASHA-ROSE MIGIRO AKUTANA NA RAIS MWINYI – ZANZIBAR
05-11-2025
ILANI YA UCHAGUZI YA CCM 2025-2030
05-11-2025
WASIRA:CCM HATUKATI MGOMBEA ILA TUNATEUA WACHACHE KATI YA WENGI
05-11-2025
WANACHAMA 280 WA CHADEMA WATIMKIA CCM
05-11-2025
BALOZI NCHIMBI: MAONI YOYOTE KUHUSU AMANI YA TANZANIA HAYATAPUUZWA
05-11-2025
π¦ππ₯πππππ π¬π π₯πππ¦ πππ§. π¦ππ ππ ππ ππͺπππ ππππ π π¬π π πππ‘πππππ’ ππππ π¦ππππ π¨ - ππ£π. ππ π’π¦ π ππππππ
05-11-2025
MAKALLA: BARABARA YA MPWAPWA NJIAPANDA KONGWA KUJENGWA LAMI
05-11-2025
BALOZI NCHIMBI AWASILI ARUSHA
05-11-2025
TAARIFA KWA UMMA
05-11-2025
UCHAGUZI MKUU SIO AJALI-WASIRA
05-11-2025
πͺπππ¨π ππ π π¦ππππππ¨π π©ππ’π‘ππ’ππ ππππππππ ππͺππ‘π¬π ππ¨π₯π ππ π ππ’π‘π - (π ππ) πππ©π¨
05-11-2025
MONGELLA AONGOZA MAZISHI YA KADA WA CCM JIJINI MWANZA
05-11-2025
ASIYETII SHERIA, KATIBA NA KUWA TAYARI KUUA KWA MASLAHI BINAFSI HUO NI UGAIDI’
05-11-2025
πππ π¬ππ¦ππ¦ππ§πππ πͺπππ’π πππ ππ¨πππππππͺπ ππͺπ ππ¨πππ‘πππ§ππ π¨πͺπππ’, π¨πππππ‘ππ’ π‘π π¨πππππππ¨, π¬ππππ ππ π πππ¨π‘ππ - πππ. πππ©π¨
05-11-2025
KAENI KIMYA KAMA HAMJUI NCHI ILIKOTOKA - WASIRA
05-11-2025
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefungua kiwanda cha kutengeneza mabomba ya maji na uchakataji pamba cha MOLI Oil Mills Co. Ltd kilichopo Bariadi Mkoani Simiyu tarehe 16 Juni, 2025.
05-11-2025