WASIRA ATOA RAI KWA VIJANA WENYE SIFA KUJITOKEZA KUGOMBEA UBUNGE,UDIWANI
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Stephen Wasira ametoa rai kwa vijana wenye sifa kujitokeza kugombea udiwani na ubunge katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba mwaka huu.
Wasira ametoa rai hiyo leo Machi 16,2025 a alipokuwa akizungumza na Wana CCM Wilaya ya Ileje mkoani Songwe.
Amesema kwa vijana ambao wanajiona wana uwezo na sifa za kugombea udiwani au ubunge wajipange katika uchaguzi Mkuu ujao kwani hakuna mwenye haki miliki ya kushikilia nafasi hizo kwa miaka mitano, isipokuwa leseni zinapatikana kupitia kinyang'anyiro cha kushawishi wananchi na mwenye nguvu ya kushawishi wanapata ridhaa.
Makamu Mwenyekiti Wasira alitoa rai alipokuwa akiunga hoja iliyotolewa na Mwenyekiti wa Chama hicho mkoa wa Songwe Radiweli Mwapashi akiyetaka kuona vijana wanapewa nafasi kugombea uongozi katika uchaguzi huo.
Wasira amesema ili kada apate nafasi ndani ya chama hicho lazima apambane na kukubalika kwa wananchi na kuongeza hata wabunge na madiwani waliopo hawakugombea peke yao.
Amesema katika uchaguzi Mkuu mwaka huu hakuna mtu kupita bila kupingwa kwahiyo hata watakao gombea lazima walijue hilo maana wamekubaliana kijana kama anataka kugombea muda ukifika ajitokeze na kama anataka kuwa msindikizaji shauri yake.
Wasira amesema katika kuelekea uchaguzi huo kwa nafasi ya udiwani na ubunge vitakuwa wazi isipokuwa nafasi ya urais pekee ambayo tayari Mkutano Mkuu Maalum uliofanyika Dodoma umeshapitisha jina la Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea urais.
Amesisitiza mkutano mkuu maalum ulikubali nafasi ya urais kugombewa na Rais Samia Suluhu Hassan kutokana na kazi nzuri aliyofanya ndani ya kipindi chake cha miaka minne ya uongozi wake.
“Tanzania inavijana wengi na kazi ya CCM ni kujenga viongozi bora kazi waliyoifanya tangu kupata uhuru hivyo wajitokeze wakanolewe ili wawe tayari kuwatumikia wananchi.”
Awali Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Songwe Radiweli Mwapashi amesema vijana wengi hasa katika mkoa huo wanaingiwa na uoga kukabiliana na madiwani na wabunge watakaotetea nafasi hizo katika uchaguzi ujao.
Hata hivyo amesema kuhamasisha vijana wachukue fomu isitafsiriwe kuwa anawabagua au kuwatenga waliopo madarakani, bali anatamani kuona wanatengeneza viongozi vijana ili Chama hicho kiendelee kupika viongozi kizazi hadi kizazi.
CCM YAIPA POLE MSUMBIJI KWA KUKUMBWA NA MAFURIKO
03-02-2026
INJINI YA CHAMA CHA MAPINDUZI IPO MASHINANI; DKT.MIGIRO
03-02-2026
DK.MIGIRO:CCM INAJENGWA KUANZIA NGAZI YA MASHINA SIO MAJUKWAANI.
03-02-2026
πππ¦πππ‘ππ’ πππ πππ§. π ππππ₯π’ ππππ£π’πππππͺπ ππͺπ π¦πππ‘ππͺπ πππ₯ ππ¦ π¦πππππ
03-02-2026
NAIBU KATIBU MKUU WA CCM BARA AMWAKILISHA KATIBU MKUU WA CCM KWENYE MSIBA WA MBUNGE WA JIMBO LA PERAMIHO
03-02-2026
π©ππππ‘π π§π¨ππππ‘ππ ππ ππ‘π π¬π π‘πππ π¬ππ§π¨ - π πͺππ‘πππ πππ‘ππ‘π
03-02-2026
DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AONGOZA KIKAO MAALUMU CHA KAMATI KUU YA CCM
03-02-2026
RAIS SAMIA AKIWAAPISHA MAWAZIRI NA MANAIBU WAZIRI WATEULE- IKULU CHAMWINO DODOMA
03-02-2026
WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU NCHEMBA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA DODOMA (GENERAL)
03-02-2026
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ..
03-02-2026
RAIS SAMIA AKIHUTUBIA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
03-02-2026
DKT SAMIA:TUNAFANYA UCHAGUZI KWA FEDHA ZETU WENYEWE
03-02-2026
MGOMBEA URAIS KUPITIA CCM DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA MANYARA
03-02-2026
π¨ππππ£πππππ πͺπ πππ§. π¦ππ ππ π¨π ππππ§π ππ ππ‘π ππͺπ πͺππ£ππ‘πππ‘π, πͺππππ¨ππππ πππ
πππ©πππͺ ππ πͺπͺ πΏπ π©. πππππ§π€ ππ¬ππ₯π€π ππ πππ€π£ππ€π―π π¬π πΎππΌπΏπππΌ π£π πΌπΎπ
03-02-2026
πππ§. π¦ππ ππ ππ§π¨π π‘πππ‘π π¬π ππ₯πππ π¬π ππππ’π π
03-02-2026
KATIBU MKUU WA CCM, BALOZI DKT. ASHA-ROSE MIGIRO AKUTANA NA RAIS MWINYI – ZANZIBAR
03-02-2026
ILANI YA UCHAGUZI YA CCM 2025-2030
03-02-2026
WASIRA:CCM HATUKATI MGOMBEA ILA TUNATEUA WACHACHE KATI YA WENGI
03-02-2026
WANACHAMA 280 WA CHADEMA WATIMKIA CCM
03-02-2026
BALOZI NCHIMBI: MAONI YOYOTE KUHUSU AMANI YA TANZANIA HAYATAPUUZWA
03-02-2026