MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR MHE HEMED SULEIMAN ABDULLA AMESEMA SERIKALI YA ZANZIBAR INAENDELEA KUWEKA MAZINGIRA BORA ILI KUEPUKANA NA MAGONJWA YA MIRIPUKO NA KUCHUKUA HATUA ZA MATIBABU PINDI MAGONJWA HAYO YATAKAPOJITOKEZA.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Hemed Suleiman Abdulla amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaendelea kuweka mazingira bora ya kuweza kuepukana na magonjwa mbali mbali ya miripuko sambamba na kuchukua hatua za matibabu pindi magonjwa hayo yatakapojitokeza.
Ameyasema hayo katika Uzinduzi wa Kituo cha Mawasiliano ya Magonjwa ya Miripuko (Zanzibar Afya Call Center) katika Viwanja vya Magomeni - Sogea Zanzibar.
Mhe. Hemed amesema Sekta ya Afya Zanzibar imekuwa ikichukua hatua mbali mbali katika kuboresha upatikanaji na utowaji wa huduma bora pamoja na kudhibiti magonjwa ya miripuko ambayo yalikuwa na changamoto kubwa kutokana na kutokuwa na njia bora za mawasiliano kutoka kwa mwananchi kwenda katika Mifumo ya Afya ili kuweza kupatiwa suluhisho la chanamoto hio.
Amefahamisha kuwa Zanzibar ni miongoni mwa nchi zilizokumbwa na Janga la COVID 19 ambalo lilipoteza maisha ya watu wengi na kuathiri mifumo ya uchumi kutokana na ugumu uliokuwepo wa kusambaza taarifa kutoka kwa wananchi kwenda Serikalini juu ya ugonjwa huo.
Amesema kuwa uzinduzi wa kituo hicho cha mawasiliano kitakuwa ni muarubaini utakaorahisisha upatikanaji wa mawasiliano baina ya wananchi na watoa huduma za Afya pindi magonjwa ya miripuko na dharura yatakapojitokeza sambamba na kuwataka wananchi kukitumia kituo hicho kama kilivyokusudiwa ili kurahisisha upatikanaji wa huduma bora na kwa wakati husika.
Aidha Mhe Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema kuwepo kwa kituo hicho kitatoa faida nyingi kwa wananchi ikiwa ni pamoja na mgonjwa kuelekezwa sehemu sahihi ya kupata matibabu kulingana na ugonjwa wake kwa kufuata utaratibu uliowekwa na Wizara ya Afya .
Sambamba na hayo amesema Kituo cha mawasiliano ya magonjwa ya miripuko kitawasaidia wananchi kufahamu juu ya Mfuko wa wa Huduma za Bima ya Afya Zanzibar ikiwemo namna ya kujiunga, masharti, faida na wanufaika wa amfuko huo pamoja na kuwaunganisha watalii na wageni mbali mbali ambao watapatiwa taarifa za huduma za Afya zinazopatikana hapa Zanzibar .
Mheshimiwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ametoa wito kwa Uongozi wa Wizara ya Afya kuendelea kukitunza kituo hicho kwa kuhakikisha mambo ya msingi yanayohitajika katika kuleta ufanisi wa utowaji wa huduma bora yanapatikana, kuwepo kwa mafundi watakaotoa msaada wa marekebisho pindi watakapohitajika na kuwa na ulinzi wa uhakika kwa masaa ishirini na nne (24) ili kufikia malengo yaliyowekwa na serikali.
Nae Waziri wa Afya Mhe. Nassor Ahmed Mazrui amesema uendeshaji wa kituo hicho unahitaji fedha na nyenzo za kutosha ili kiweze kufanya kazi kwa ufanisi na uweledi wa kuweza kuwahudumia Wazanzibari na wageni wanaoingia nchini kwa wakati.
Mhe. Mazrui amewataka wahudumu wa kituo hicho kufanya kazi kwa uaminifu na uadilifu mkubwa, Ari na kasi zaidi ili kuendana na kasi ya serikali ya awamu ya nane (8) inayoongozwa na Dkt. Hussein Ali Mwinyi ya kuwatumikia wazanzibar na kutoa huduma bora za afya kwa wote.
Kwa upande wake Mwakilishi kutoka UNICEF Bibi. AWETY ATIE amesema Shirika la UNICEF limekuwa likishirikiana kwa karibu ba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kutekeleza miradi mbali mbali ya Maendeleo ikiwemo kukikarabati kituo cha Mawasiliano ya Magonjwa ya Mripuko ili kuweza kufanya kazi kwa ufanisi na kupambana na magonjwa ya mripoko yanatotokea nchini.
Amesema UNICEF itaendelea kutoa misaada na mashirikiano kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kukiendesha kituo hicho kwa muda wa miaka mitano (5) ambacho kitafanya kazi kwa Mfumo wa kidijitali pamoja na kutoa na kupokea taarifa mbali mbali zinazohusiana na masuala ya Afya.
Aidha Bibi. ATIE amewataka wananchi wa Zanziabar kukitumia kituo hicho pale wanapopatwa na dharura ama kutaka kupatiwa ufafanuzi na ufumbuzi juu ya masuala ya Afya kwa kupiga simu bure kwa namba 190 ama kutuma ujumbe mfupi wa maandishi kupitia namba 30 ili kuweza kupatiwa ufumbuzi juu ya tatizo linalowakabili kwa wakati husika.
𝐒𝐀𝐒𝐀 𝐍𝐈 𝐙𝐀𝐌𝐔 𝐘𝐀 𝐏𝐖𝐀𝐍𝐈; 𝐀𝐑𝐃𝐇𝐈 𝐘𝐀 𝐇𝐈𝐒𝐓𝐎𝐑𝐈𝐀, 𝐌𝐖𝐄𝐍𝐄𝐙𝐈 𝐀𝐍𝐀𝐊𝐔𝐉𝐀!!!!!
25-06-2026
𝐈𝐑𝐈𝐍𝐆𝐀 𝐌𝐉𝐈𝐍𝐈 𝐘𝐀𝐌𝐏𝐀 𝐊𝐄𝐍𝐀𝐍𝐈 𝐌𝐀𝐏𝐎𝐊𝐄𝐙𝐈 𝐘𝐀 𝐊𝐈𝐇𝐈𝐒𝐓𝐎𝐑𝐈𝐀
25-06-2026
𝐌𝐖𝐄𝐍𝐄𝐙𝐈 𝐊𝐄𝐍𝐀𝐍𝐈 𝐀𝐙𝐈𝐍𝐃𝐔𝐀 𝐒𝐇𝐈𝐍𝐀 𝐋𝐀 𝐖𝐀𝐊𝐄𝐑𝐄𝐊𝐄𝐓𝐖𝐀 𝐌𝐋𝐀𝐍𝐃𝐄𝐆𝐄, 𝐊𝐈𝐋𝐎𝐒𝐀-𝐈𝐑𝐈𝐍𝐆𝐀
25-06-2026
𝐌𝐖𝐄𝐍𝐄𝐙𝐈 𝐊𝐄𝐍𝐀𝐍𝐈 𝐀𝐓𝐄𝐌𝐁𝐄𝐋𝐄𝐀 𝐒𝐇𝐈𝐍𝐀 𝐍𝐀. 𝟏𝟎 𝐌𝐀𝐅𝐈𝐅𝐈, 𝐀𝐒𝐈𝐒𝐈𝐓𝐈𝐙𝐀 𝐀𝐌𝐀𝐍𝐈, 𝐔𝐌𝐎𝐉𝐀 𝐍𝐀 𝐌𝐒𝐇𝐈𝐊𝐀𝐌𝐀𝐍𝐎
25-06-2026
𝐌𝐑𝐀𝐃𝐈 𝐖𝐀 𝐌𝐀𝐅𝐔𝐍𝐙𝐎 𝐘𝐀 𝐔𝐅𝐔𝐍𝐃𝐈 𝐊𝐈𝐋𝐎𝐋𝐎 𝐊𝐔𝐅𝐔𝐍𝐆𝐔𝐀 𝐅𝐔𝐑𝐒𝐀 𝐙𝐀 𝐀𝐉𝐈𝐑𝐀 𝐊𝐖𝐀 𝐕𝐈𝐉𝐀𝐍𝐀
25-06-2026
𝐊𝐈𝐋𝐎𝐋𝐎, 𝐙𝐀𝐌𝐔 𝐘𝐄𝐍𝐔 𝐍𝐈 𝐋𝐄𝐎!
25-06-2026
𝐑𝐀𝐁𝐈𝐀: 𝐃𝐊𝐓. 𝐒𝐀𝐌𝐈𝐀 𝐒𝐔𝐋𝐔𝐇𝐔 𝐇𝐀𝐒𝐒𝐀𝐍 𝐍𝐈 𝐌𝐓𝐄𝐊𝐄𝐋𝐄𝐙𝐀𝐉𝐈 𝐌𝐀𝐇𝐈𝐑𝐈 𝐖𝐀 𝐀𝐇𝐀𝐃𝐈 𝐙𝐀 𝐂𝐂𝐌
25-06-2026
𝐒𝐈𝐌𝐔 𝐈𝐌𝐄𝐈𝐓𝐀, 𝐍𝐄𝐄𝐌𝐀 𝐘𝐀 𝐔𝐓𝐀𝐓𝐔𝐙𝐈 𝐊𝐈𝐋𝐎𝐋𝐎!
25-06-2026
𝐑𝐔𝐀𝐇𝐀 𝐌𝐁𝐔𝐘𝐔𝐍𝐈 𝐘𝐀𝐅𝐔𝐑𝐈𝐊𝐀; “𝐂𝐇𝐈𝐄𝐅 𝐂𝐇𝐎𝐆𝐀𝐕𝐀𝐓𝐀𝐌𝐁𝐔𝐋𝐄” 𝐀𝐊𝐈𝐓𝐄𝐊𝐀 𝐌𝐊𝐔𝐓𝐀𝐍𝐎 𝐖𝐀 𝐇𝐀𝐃𝐇𝐀𝐑𝐀!
25-06-2026
𝐊𝐈𝐋𝐈𝐌𝐎 𝐂𝐇𝐀 𝐔𝐌𝐖𝐀𝐆𝐈𝐋𝐈𝐀𝐉𝐈 𝐍𝐈 𝐔𝐅𝐔𝐍𝐆𝐔𝐎 𝐖𝐀 𝐌𝐀𝐏𝐈𝐍𝐃𝐔𝐙𝐈 𝐘𝐀 𝐔𝐂𝐇𝐔𝐌𝐈 𝐖𝐀 𝐖𝐀𝐍𝐀𝐍𝐂𝐇𝐈: 𝐊𝐈𝐇𝐎𝐍𝐆𝐎𝐒𝐈
25-06-2026
𝐂𝐂𝐌 𝐘𝐀𝐔𝐍𝐆𝐀 𝐌𝐊𝐎𝐍𝐎 𝐖𝐀𝐍𝐀𝐍𝐂𝐇𝐈 𝐖𝐀 𝐍𝐉𝐎𝐌𝐁𝐄 𝐊𝐖𝐀 𝐊𝐀𝐙𝐈 𝐙𝐀 𝐔𝐙𝐀𝐋𝐈𝐒𝐇𝐀𝐉𝐈 𝐌𝐀𝐋𝐈
25-06-2026
𝐀𝐌𝐀𝐍𝐈 𝐍𝐈 𝐌𝐒𝐈𝐍𝐆𝐈 𝐖𝐀 𝐌𝐀𝐄𝐍𝐃𝐄𝐋𝐄𝐎: 𝐊𝐈𝐇𝐎𝐍𝐆𝐎𝐒𝐈
25-06-2026
𝐊𝐈𝐇𝐎𝐍𝐆𝐎𝐒𝐈 𝐑𝐀𝐒𝐌𝐈 𝐈𝐑𝐈𝐍𝐆𝐀!!
25-06-2026
𝐑𝐀𝐁𝐈𝐀 𝐀𝐏𝐎𝐊𝐄𝐋𝐄𝐖𝐀 𝐍𝐉𝐎𝐌𝐁𝐄, 𝐀𝐇𝐈𝐌𝐈𝐙𝐀 𝐕𝐈𝐎𝐍𝐆𝐎𝐙𝐈 𝐖𝐀 𝐂𝐂𝐌 𝐊𝐔𝐈𝐒𝐇𝐈 𝐃𝐇𝐀𝐍𝐀 𝐘𝐀 𝐊𝐀𝐙𝐈 𝐍𝐀 𝐔𝐓𝐔 𝐊𝐖𝐀 𝐕𝐈𝐓𝐄𝐍𝐃𝐎
25-06-2026
𝐑𝐀𝐁𝐈𝐀: 𝐂𝐂𝐌 𝐇𝐀𝐈𝐓𝐀𝐕𝐔𝐌𝐈𝐋𝐈𝐀 𝐔𝐙𝐄𝐌𝐁𝐄, 𝐕𝐈𝐎𝐍𝐆𝐎𝐙𝐈 𝐖𝐀𝐖𝐀𝐉𝐈𝐁𝐈𝐊𝐄 𝐊𝐔𝐓𝐀𝐓𝐔𝐀 𝐂𝐇𝐀𝐍𝐆𝐀𝐌𝐎𝐓𝐎 𝐙𝐀 𝐖𝐀𝐍𝐀𝐍𝐂𝐇𝐈
25-06-2026
𝐈𝐑𝐈𝐍𝐆𝐀 𝐓𝐔𝐍𝐀𝐊𝐔𝐉𝐀𝐀𝐀, 𝐓𝐔𝐍𝐀𝐀𝐍𝐙𝐈𝐀 𝐑𝐔𝐀𝐇𝐀 𝐌𝐁𝐔𝐘𝐔𝐍𝐈!
25-06-2026
𝐌𝐈𝐊𝐎𝐏𝐎 𝐘𝐀 𝐀𝐒𝐈𝐋𝐈𝐌𝐈𝐀 𝟏𝟎% 𝐘𝐀𝐂𝐇𝐎𝐂𝐇𝐄𝐀 𝐔𝐂𝐇𝐔𝐌𝐈 𝐖𝐀 𝐌𝐀𝐊𝐔𝐍𝐃𝐈 𝐌𝐀𝐀𝐋𝐔𝐌
25-06-2026
𝐍𝐃𝐆 𝐑𝐀𝐁𝐈𝐀 𝐀𝐏𝐎𝐊𝐄𝐋𝐄𝐖𝐀 𝐑𝐔𝐕𝐔𝐌𝐀, 𝐀𝐇𝐈𝐌𝐈𝐙𝐀 𝐔𝐌𝐎𝐉𝐀 𝐍𝐀 𝐌𝐒𝐇𝐈𝐊𝐀𝐌𝐀𝐍𝐎 𝐍𝐃𝐈𝐎 𝐍𝐆𝐔𝐕𝐔 𝐘𝐀 𝐂𝐂𝐌
25-06-2026
𝐊𝐇𝐄𝐑𝐈 𝐘𝐀 𝐒𝐈𝐊𝐔 𝐘𝐀 𝐊𝐈𝐌𝐀𝐓𝐀𝐈𝐅𝐀 𝐘𝐀 𝐌𝐓𝐎𝐓𝐎 𝐖𝐀 𝐀𝐅𝐑𝐈𝐊𝐀
25-06-2026
𝐌𝐇𝐄. 𝐑𝐀𝐈𝐒 𝐀𝐍𝐀𝐖𝐀𝐏𝐄𝐍𝐃𝐀 𝐒𝐀𝐍𝐀 𝐖𝐀𝐓𝐀𝐍𝐙𝐀𝐍𝐈𝐀, 𝐖𝐀𝐓𝐔𝐌𝐈𝐒𝐇𝐈 𝐖𝐀 𝐔𝐌𝐌𝐀 𝐓𝐈𝐌𝐈𝐙𝐄𝐍𝐈 𝐖𝐀𝐉𝐈𝐁𝐔 𝐖𝐄𝐍𝐔 𝐊𝐈𝐊𝐀𝐌𝐈𝐋𝐈𝐅𝐔: 𝐑𝐀𝐁𝐈𝐀
25-06-2026