Al HAJI DK. HUSSEIN ALI MWINYI AHIMIZA JAMII KUFANYA UTAFITI KWENYE NYANJA MBALIMBALI KATIKA ELIMU ILI KUTANUA WIGO KUPITIA SEKTA ZA KIMAENDELEO.
Al hajj Dk. Mwinyi alitoa nasaha hizo kwenye Masjid Abuu Ubayda, Fuoni Meli Saba, Mkoa wa Mjini Magharibi, alikojumuila na waumini wa dini ya Kiislamu kwenye ibada ya sala ya Ijumaa. Alisema, mataifa makubwa yaliyoendelea yamewekeza mtaji mkubwa kwenye elimu, ambao hutumia fedha nyingi kushajihisha elimu. Al hajj Mwinyi alieleza kadri ya mataifa hayo yanavyotumia pesa nyingi kwenye elimu, ndivyo wanavyopiga hatua zaidi za maendeleo.
“Ukisikia kuna nchi inafanya maendeleo makubwa basi ujue ndani yake watu wamejikita mno katika masuala mazima ya elimu, suala la Utafiti maana elimu inaletwa na utafiti”. Alisema, elimu ndio inayoleta mabadiliko mamkubwa kwenye jamii maendeleo yote yanatokana na elimu watu kujifunza elimu ya dini na dunia.
Kwaupande mwengine Al hajj Dk. Mwinyi alieleza elimu ya dini huwapandisha darja waumini wake kwa kuendelea kumcha Mwenyezi Mungu kikweli kaatika kutekeleza ibada ya haki kama inavyotakiwa. Pia, Alhaj, Dk. Mwinyi amewasihi wazazi/ walezi kuendelea kuwahimiza watoto wao kusoma elimu zote mbili ya dini na dunia, ili kukuza taifa lenye vijana wenye maadili na busara ya kukimbilia maendeleo kwa ajili ya familia zao na taifa kwa ujumla. Alieleza, miongoni mwa sababu zinazochangia mmong’onyoko wa maadili kwenye jamii ni ukosefu wa elimu zote mbili, hivyo aliiasa jamii kuweka mkazo zaidi kwenye elimu na kulinda maadili ya uislamu.
Hata hivyo, Al hajj Dk. Mwinyi aliitaka jamii kuendelea kutekeleza maarisho ya Mwenyezi Mungu kwa kufuata mafundisho ya Mtume (SAW) kwa kufanya yaliyo mema na kuacha mabaya yanayomchukiza Allah (S.W).
Naye, Katibu Mtendaji kutoka Ofisi ya Mufti Zanzibar, Sheikh Khalid Ali Mfaume, ameisistiza jamii ya waislam kuendelea kukithirisha ibada hasa kwenye mwezi mtukufu wa Muharam. Alisema, Mwezi wa Mfunguo nne (Muharami) ni miongoni mwa miezi mitukufu ya Mwenyezi Mungu baada ya Ramadhan. Pia alisisitiza mwezi 10 Muharam ni sunna kufunga kwa waumini wa dini ya kiislam, funga ya Ashura, aliyoieleza ni funga bora baada ya Ramadhani ambayo Mtume (SAW) aliifunga mara baada ya kuhamia Madina.
Naye, Khatibu wa sala hiyo ya Ijumaa, Sheikh Sultan Nassor, aliwahimiza waislam kuendelea kuwa wachamungu kwa kumcha Allah (S.W) kwa haki ili kujiepusha na yote aliyoyakataza.
Akizungumza kwenye msikiti huo wa Abuu Ubayda, Fuoni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Mahad Istiqama, Sheikh Said Khalfan aliisihi jamiii kuendelea kushirikiana na Ofisi ya Muft katika kutatua changamoto zao.
DKT SAMIA:TUNAFANYA UCHAGUZI KWA FEDHA ZETU WENYEWE
04-11-2025
MGOMBEA URAIS KUPITIA CCM DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA MANYARA
04-11-2025
π¨ππππ£πππππ πͺπ πππ§. π¦ππ ππ π¨π ππππ§π ππ ππ‘π ππͺπ πͺππ£ππ‘πππ‘π, πͺππππ¨ππππ πππ
πππ©πππͺ ππ πͺπͺ πΏπ π©. πππππ§π€ ππ¬ππ₯π€π ππ πππ€π£ππ€π―π π¬π πΎππΌπΏπππΌ π£π πΌπΎπ
04-11-2025
πππ§. π¦ππ ππ ππ§π¨π π‘πππ‘π π¬π ππ₯πππ π¬π ππππ’π π
04-11-2025
KATIBU MKUU WA CCM, BALOZI DKT. ASHA-ROSE MIGIRO AKUTANA NA RAIS MWINYI – ZANZIBAR
04-11-2025
ILANI YA UCHAGUZI YA CCM 2025-2030
04-11-2025
WASIRA:CCM HATUKATI MGOMBEA ILA TUNATEUA WACHACHE KATI YA WENGI
04-11-2025
WANACHAMA 280 WA CHADEMA WATIMKIA CCM
04-11-2025
BALOZI NCHIMBI: MAONI YOYOTE KUHUSU AMANI YA TANZANIA HAYATAPUUZWA
04-11-2025
π¦ππ₯πππππ π¬π π₯πππ¦ πππ§. π¦ππ ππ ππ ππͺπππ ππππ π π¬π π πππ‘πππππ’ ππππ π¦ππππ π¨ - ππ£π. ππ π’π¦ π ππππππ
04-11-2025
MAKALLA: BARABARA YA MPWAPWA NJIAPANDA KONGWA KUJENGWA LAMI
04-11-2025
BALOZI NCHIMBI AWASILI ARUSHA
04-11-2025
TAARIFA KWA UMMA
04-11-2025
UCHAGUZI MKUU SIO AJALI-WASIRA
04-11-2025
πͺπππ¨π ππ π π¦ππππππ¨π π©ππ’π‘ππ’ππ ππππππππ ππͺππ‘π¬π ππ¨π₯π ππ π ππ’π‘π - (π ππ) πππ©π¨
04-11-2025
MONGELLA AONGOZA MAZISHI YA KADA WA CCM JIJINI MWANZA
04-11-2025
ASIYETII SHERIA, KATIBA NA KUWA TAYARI KUUA KWA MASLAHI BINAFSI HUO NI UGAIDI’
04-11-2025
πππ π¬ππ¦ππ¦ππ§πππ πͺπππ’π πππ ππ¨πππππππͺπ ππͺπ ππ¨πππ‘πππ§ππ π¨πͺπππ’, π¨πππππ‘ππ’ π‘π π¨πππππππ¨, π¬ππππ ππ π πππ¨π‘ππ - πππ. πππ©π¨
04-11-2025
KAENI KIMYA KAMA HAMJUI NCHI ILIKOTOKA - WASIRA
04-11-2025
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefungua kiwanda cha kutengeneza mabomba ya maji na uchakataji pamba cha MOLI Oil Mills Co. Ltd kilichopo Bariadi Mkoani Simiyu tarehe 16 Juni, 2025.
04-11-2025