Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo amekutana na Balozi wa Denmark nchini Tanzania Mhe. Mette Nørgaard Dissing-Spandet jijini Dodoma.
Katika mazungumzo hayo, Mhe. Dkt. Jafo amesema Tanzania inathamini ushirikiano uliopo baina ya nchi hizo mbili na inatarajia kuendelea kushirikiana zaidi katika hifadhi ya mazingira.
Amesema kuwa Tanzania inashirikiana na Denmark katika kusukuma mbele ajenda ya matumizi ya nishati safi ya kupikia ambayo itasaidia katika kupunguza kasi ya ukataji wa miti kwa ajili ya kuni na mkaa.
Kupitia ajenda hiyo amemtaja Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa ameonesha dhamira ya dhati ya kuhakikisha asilimia kubwa ya wanawake wa Tanzania na Afrika kwa ujumla wanatumia nishati safi ya kupikia.
Dkt. Jafo amesema kuwa katika Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tanianchi (COP28) uliofanyika Dubai, Falme za Kiarabu, Rais Dkt. Samia alizindua Mradi wa Nishati Safi ya kupikia itakayowasaidia wanawake barani Afrika.
Kutokana na umuhimu wa matumizi ya nishati safi ya kupikia, Waziri Dkt. Jafo amesisitiza ni wakati sasa Tanzania inahitaji kuwabadilisha wananchi kuachana na matumizi ya kuni na mkaa na kuanza kutumia nishati safi ya kupikia.
Ameongeza kwa kuwashukuru wawekezaji wa nishati safi ya kupikia hususan gesi kwa kuunga mkono Serikali kwa kutoa mitungi ya gesi kwa taasisi mbalimbali zinazolisha watu zaidi ya mia moja.
Halikadhalika, Dkt. Jafo amesema Tanzania inatekeleza mikakati mbalimbali ya kukabiliana na athari za uharibifu wa mazingira ambapo ilizindua Sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021, Mpango Kabambe wa Taifa wa Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (2022-2032).
Kwa upande wake Mhe. Balozi Dissing-Spandet amemuhakikishia Waziri Jafo kuwa nchi yake itaendeleza ushirikiano wake kwa Tanzania katika sekta mbalimbali ikiwemo ya mazingira.
DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AONGOZA KIKAO MAALUMU CHA KAMATI KUU YA CCM
09-12-2025
RAIS SAMIA AKIWAAPISHA MAWAZIRI NA MANAIBU WAZIRI WATEULE- IKULU CHAMWINO DODOMA
09-12-2025
WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU NCHEMBA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA DODOMA (GENERAL)
09-12-2025
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ..
09-12-2025
RAIS SAMIA AKIHUTUBIA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
09-12-2025
DKT SAMIA:TUNAFANYA UCHAGUZI KWA FEDHA ZETU WENYEWE
09-12-2025
MGOMBEA URAIS KUPITIA CCM DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA MANYARA
09-12-2025
π¨ππππ£πππππ πͺπ πππ§. π¦ππ ππ π¨π ππππ§π ππ ππ‘π ππͺπ πͺππ£ππ‘πππ‘π, πͺππππ¨ππππ πππ
πππ©πππͺ ππ πͺπͺ πΏπ π©. πππππ§π€ ππ¬ππ₯π€π ππ πππ€π£ππ€π―π π¬π πΎππΌπΏπππΌ π£π πΌπΎπ
09-12-2025
πππ§. π¦ππ ππ ππ§π¨π π‘πππ‘π π¬π ππ₯πππ π¬π ππππ’π π
09-12-2025
KATIBU MKUU WA CCM, BALOZI DKT. ASHA-ROSE MIGIRO AKUTANA NA RAIS MWINYI – ZANZIBAR
09-12-2025
ILANI YA UCHAGUZI YA CCM 2025-2030
09-12-2025
WASIRA:CCM HATUKATI MGOMBEA ILA TUNATEUA WACHACHE KATI YA WENGI
09-12-2025
WANACHAMA 280 WA CHADEMA WATIMKIA CCM
09-12-2025
BALOZI NCHIMBI: MAONI YOYOTE KUHUSU AMANI YA TANZANIA HAYATAPUUZWA
09-12-2025
π¦ππ₯πππππ π¬π π₯πππ¦ πππ§. π¦ππ ππ ππ ππͺπππ ππππ π π¬π π πππ‘πππππ’ ππππ π¦ππππ π¨ - ππ£π. ππ π’π¦ π ππππππ
09-12-2025
MAKALLA: BARABARA YA MPWAPWA NJIAPANDA KONGWA KUJENGWA LAMI
09-12-2025
BALOZI NCHIMBI AWASILI ARUSHA
09-12-2025
TAARIFA KWA UMMA
09-12-2025
UCHAGUZI MKUU SIO AJALI-WASIRA
09-12-2025
πͺπππ¨π ππ π π¦ππππππ¨π π©ππ’π‘ππ’ππ ππππππππ ππͺππ‘π¬π ππ¨π₯π ππ π ππ’π‘π - (π ππ) πππ©π¨
09-12-2025