Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


FEDHA SH 510 MILIONI ZAPATIKANA UJENZI UZIO SHULE YA SEKONDARI YA WASICHANA RUVU

alternative

•Rais Dr Samia achangia milioni 100

Rais Dk Samia Suluhu Hassan amechangia kiasi cha Sh milioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa uzio wa shule ya Sekondari ya Wasichana ya Ruvu iliyopo Kibaha mkoani Pwani, lengo likiwa ni kuimarisha usalama wa wanafunzi hao wawapo shuleni.

Harambee kwa ajili ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi huo ilifanyike Juni 14,2025 katika Ukumbi wa Mikutano wa hoteli ya Golden Tulip Dar es salaam na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alikuwa muwakilishi wa Rais Samia katika hilo.

Katika harambee hiyo ilifanikiwa kukusanywa kiasi cha Sh milioni 510  kwa ajili kujenga uzio

Wakati akizungumza Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Rais Dkt. Samia anaunga mkono uamuzi huo wenye nia ya kuwafanya wanafunzi wa kike katika shule hiyo kusoma katika mazingira salama.

Sambamba na hilo Mheshimiwa Majaliwa ametoa mwito kwa halmashauri nchini kuendelea kutenga fedha kutoka kwenye mapato ya ndani kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa shule katika maeneo hayo badala ya kusubiri serikali kuu pekee.

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Ujenzi, CPA Amos Makala amesema lengo la kukusanya fedha hizo ni kuhakikisha wanajenga uzio huo ili kuwapa usalama watoto wa kike wanaosoma katika shule hiyo.

alternative alternative alternative alternative
Habari Nyingine