Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Ndugu.Dkt Hussein Ali Mwinyi amesema Chama cha Mapinduzi kinatambua na kuthamini mchango mkubwa unaotolewa na Jumuiya ya wazazi Tanzania katika kuhakikisha CCM inaendelea kushikilia dola awamu kwa awamu
Ameyasema hayo katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Ndugu Hemed Suleiman Abdulla katika uzinduzi wa sherehe za Wiki ya wazazi Kitaifa zinazofanyika Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi.
Dkt Mwinyi amesema Jumuiya ya wazazi imekuwa ikifanya kazi nzuri katika kusimamia elimu, maadili na malezi bora kwa watoto yenye kufuata utamaduni wa Kitanzania jambo ambalo linaendelea kuiletea heshima kubwa Tanzania.
Amesema kuwa jumuiya ya wazazi imekuwa mstari wa mbele katika kupiga vita vitendo vya ukatili, unyanyasaji na udhalishaji wa kijinsia jambo ambalo linazorotesha nguvu kazi na maendeleo ya Taifa hivyo ni wajibu wa kila mwanajumuiya kuhakikisha anasimama imara katika kupinga vitendo hivi.
Rais Dkt. Mwinyi amesema mtaji wa chama chochote cha siasa ni wanachama hai hivyo ameitaka Jumuiya ya Wazazi kuendelea kuhamasisha wananchi kujiunga na CCM, kuwapa elimu ya kupiga kura pamoja na kuwajenga kuwa na utayari wa kukipigia kura kwa wingi chama cha Mapinduzi katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa na uchaguzi mkuu wa mwaka 2020-2025.
Aidha Makamu Mwenyekiti Mwinyi amewasisitiza viongozi kushuka chini kwa wanachama na kufanya ziara ya kuzitembelea jumuia mbali mbali pamoja na kushika kwa wananchi kusikiliza changamoto zinazowakabili na kuziwasilisha Serikali kupatiwa ufumbuzi kwa maslahi ya chama na serikali.
Rais Dkt Mwinyi amesasisistiza kuwataka Watanzania kuwa Umoja na Mshikamano kwa kuweka mbele maslahi ya CCM hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa na uchaguzi mkuu ujao ili CCM iendelee kushinda kwa kishindo na kudhikilia madaraka.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa anaefanyia kazi zake Zanzibar Ndugu DOGO IDDI MABROUK amesema Jumiiya ya Wazazi itaendelea kutoa elimu na kuhamasisha juu ya malezi bora ya watoto kwa kutambua tamaduni zao ambazo zinaonekana kutoweka na kusababisha mmong'onyoko wa maadili jambo linalopelekea kuongezeka kwa vitendo vya udhalilishaji na ukatili wa kijinsia hasa kwa wanawake na watoto.
Ndugu DOGO amesema kupitia Jumuiya ya wazazi itahakikisha sera tano muhimu za jumuiya hio zinatiliwa mkazo katika utekelezaji wake ikiwa ni pamoja na elimu, malezi, utamaduni, mazingira na afya ili kuhakikisha CCM inakuwa na wanachama wenye uweledi na wenye kufuata maadili kama sera na miongozi ya chama inavyoongoza.
Akiwasalimia wananchi wa Mkoa wa Katavi Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Ndugu Mizengo Kayanza Pinda amesisitiza umoja na mshikamano kwa Watanzania wote ambao hujenga upendo miongoni mwao na kupelekea amani na utulivu ambao ndio ngao na muhimili mkubwa wa maendeleo ya Taifa.
Mhe. Pinda amewataka wanakatavi na watanzani wote kuendelea kujiandikisha katika daftari la kupigia kura ili kuweza kupata nafasi ya kukipigia kura kwa wingi chama cha Mapinduzi na kuendelea kukiweka madarakani.
Pinda amesema uhifadhi wa mazingira ni jambo la lazima kwa kila Mtanzania na kuwaomba kuacha tabia ya kukata miti na kuchoma moto kiholela misitu ya hifadhi na badala yake wajenge tabia ya kupanda miti kwa kuhifadhi mazingira.
𝐌𝐖𝐄𝐍𝐄𝐙𝐈 𝐊𝐄𝐍𝐀𝐍𝐈 𝐀𝐓𝐄𝐌𝐁𝐄𝐋𝐄𝐀 𝐊𝐈𝐓𝐔𝐎 𝐂𝐇𝐀 𝐀𝐅𝐘𝐀 𝐊𝐀𝐋𝐎𝐋𝐄𝐍𝐈, 𝐀𝐑𝐔𝐒𝐇𝐀 𝐌𝐉𝐈𝐍𝐈
07-06-2026
𝐀𝐑𝐔𝐒𝐇𝐀 𝐘𝐀𝐀𝐌𝐁𝐈𝐖𝐀 𝐊𝐔𝐂𝐇𝐀𝐆𝐔𝐀 𝐌𝐀𝐄𝐍𝐃𝐄𝐋𝐄𝐎 𝐁𝐀𝐃𝐀𝐋𝐀 𝐘𝐀 𝐌𝐀𝐀𝐍𝐃𝐀𝐌𝐀𝐍𝐎
07-06-2026
𝐌𝐀𝐏𝐎𝐊𝐄𝐙𝐈 𝐘𝐀 𝐊𝐀𝐓𝐈𝐁𝐔 𝐖𝐀 𝐍𝐄𝐂, 𝐈𝐓𝐈𝐊𝐀𝐃𝐈, 𝐔𝐄𝐍𝐄𝐙𝐈 𝐍𝐀 𝐌𝐀𝐅𝐔𝐍𝐙𝐎 𝐂𝐂𝐌, 𝐍𝐃𝐔𝐆𝐔 𝐊𝐄𝐍𝐀𝐍𝐈 𝐋𝐀𝐁𝐀𝐍 𝐊𝐈𝐇𝐎𝐍𝐆𝐎𝐒𝐈, 𝐎𝐅𝐈𝐒𝐈 𝐙𝐀 𝐂𝐂𝐌 𝐖𝐈𝐋𝐀𝐘𝐀 𝐘𝐀 𝐀𝐑𝐔𝐒𝐇𝐀 𝐌𝐉𝐈𝐍𝐈
07-06-2026
𝐒𝐀𝐒𝐀 𝐍𝐈 𝐀𝐑𝐔𝐒𝐇𝐀 𝐌𝐉𝐈𝐍𝐈, 𝐌𝐖𝐄𝐍𝐃𝐎 𝐌𝐃𝐔𝐍𝐃𝐎!
07-06-2026
𝐀𝐑𝐔𝐌𝐄𝐑𝐔 𝐘𝐀𝐒𝐈𝐊𝐈𝐀 𝐖𝐈𝐓𝐎 𝐖𝐀 𝐊𝐔𝐋𝐈𝐍𝐃𝐀 𝐌𝐀𝐀𝐃𝐈𝐋𝐈 𝐍𝐀 𝐇𝐀𝐊𝐈 𝐙𝐀 𝐖𝐀𝐓𝐎𝐓𝐎
07-06-2026
𝐊𝐄𝐍𝐀𝐍𝐈 𝐀𝐒𝐀𝐌𝐁𝐀𝐙𝐀 𝐔𝐏𝐄𝐍𝐃𝐎 𝐖𝐀 𝐀𝐆𝐀𝐏𝐄 𝐊𝐖𝐄𝐍𝐘𝐄 𝐊𝐈𝐉𝐈𝐖𝐄 𝐂𝐇𝐀 𝐂𝐇𝐀𝐃𝐄𝐌𝐀 𝐀𝐑𝐔𝐌𝐄𝐑𝐔
07-06-2026
𝐊𝐈𝐇𝐎𝐍𝐆𝐎𝐒𝐈 𝐀𝐀𝐍𝐙𝐀 𝐙𝐈𝐀𝐑𝐀 𝐀𝐑𝐔𝐌𝐄𝐑𝐔 𝐊𝐖𝐀 𝐊𝐔𝐊𝐀𝐆𝐔𝐀 𝐔𝐇𝐀𝐈 𝐖𝐀 𝐂𝐇𝐀𝐌𝐀
07-06-2026
𝐌𝐊𝐔𝐓𝐀𝐍𝐎 𝐖𝐀 𝐇𝐀𝐃𝐇𝐀𝐑𝐀 𝐖𝐀 𝐌𝐖𝐄𝐍𝐄𝐙𝐈 𝐖𝐀 𝐂𝐂𝐌 𝐓𝐀𝐈𝐅𝐀 𝐖𝐈𝐋𝐀𝐘𝐀 𝐘𝐀 𝐊𝐀𝐑𝐀𝐓𝐔 - 𝐌𝐊𝐎𝐀 𝐖𝐀 𝐀𝐑𝐔𝐒𝐇𝐀
07-06-2026
𝐑𝐀𝐈𝐒 𝐒𝐀𝐌𝐈𝐀 𝐀𝐓𝐔𝐍𝐔𝐊𝐈𝐖𝐀 𝐒𝐇𝐀𝐇𝐀𝐃𝐀 𝐘𝐀 𝐇𝐄𝐒𝐇𝐈𝐌𝐀 𝐔𝐑𝐔𝐒𝐈
07-06-2026
𝐀𝐑𝐔𝐌𝐄𝐑𝐔, 𝐌𝐖𝐄𝐍𝐄𝐙𝐈 𝐖𝐀 𝐂𝐂𝐌 𝐀𝐍𝐀𝐊𝐔𝐉𝐀!
07-06-2026
𝐑𝐀𝐈𝐒 𝐒𝐀𝐌𝐈𝐀 𝐑𝐀𝐒𝐌𝐈 𝐔𝐑𝐔𝐒𝐈, 𝐀𝐊𝐔𝐓𝐀𝐍𝐀 𝐍𝐀 𝐏𝐔𝐓𝐈𝐍
07-06-2026
𝐊𝐈𝐋𝐈𝐌𝐀𝐍𝐉𝐀𝐑𝐎, 𝐓𝐔𝐍𝐀𝐊𝐔𝐉𝐀
07-06-2026
𝐑𝐀𝐈𝐒 𝐃𝐊𝐓. 𝐒𝐀𝐌𝐈𝐀 𝐀𝐖𝐀𝐒𝐈𝐋𝐈 𝐌𝐎𝐒𝐂𝐎𝐖, 𝐔𝐑𝐔𝐒𝐈 𝐊𝐖𝐀 𝐙𝐈𝐀𝐑𝐀 𝐘𝐀 𝐊𝐈𝐓𝐀𝐈𝐅𝐀
07-06-2026
𝐌𝐖𝐄𝐍𝐄𝐙𝐈 𝐖𝐀 𝐂𝐂𝐌 𝐓𝐀𝐈𝐅𝐀 𝐀𝐖𝐀𝐒𝐈𝐋𝐈 𝐖𝐈𝐋𝐀𝐘𝐀 𝐘𝐀 𝐒𝐈𝐌𝐀𝐍𝐉𝐈𝐑𝐎 𝐊𝐖𝐀 𝐙𝐈𝐀𝐑𝐀 𝐘𝐀 𝐊𝐈𝐊𝐀𝐙𝐈
07-06-2026
𝐅𝐔𝐍𝐆𝐀 𝐊𝐀𝐙𝐈 𝐌𝐊𝐎𝐀 𝐖𝐀 𝐌𝐀𝐍𝐘𝐀𝐑𝐀 𝐋𝐄𝐎!!!
07-06-2026
𝐊𝐈𝐇𝐎𝐍𝐆𝐎𝐒𝐈 𝐀𝐓𝐄𝐌𝐁𝐄𝐋𝐄𝐀 𝐒𝐇𝐈𝐍𝐀 𝐍𝐀. 𝟐 𝐊𝐀𝐓𝐀 𝐘𝐀 𝐁𝐎𝐍𝐆𝐀
07-06-2026
𝐁𝐀𝐁𝐀𝐓𝐈 𝐌𝐉𝐈𝐍𝐈 𝐋𝐄𝐎 𝐓𝐔𝐍𝐀𝐈𝐅𝐔𝐍𝐈𝐊𝐀!!!
07-06-2026
𝐊𝐈𝐇𝐎𝐍𝐆𝐎𝐒𝐈 𝐀𝐊𝐔𝐓𝐀𝐍𝐀 𝐍𝐀 𝐖𝐀𝐍𝐀𝐍𝐂𝐇𝐈 𝐇𝐀𝐍𝐀𝐍𝐆, 𝐀𝐒𝐈𝐊𝐈𝐋𝐈𝐙𝐀 𝐍𝐀 𝐊𝐔𝐓𝐀𝐓𝐔𝐀 𝐊𝐄𝐑𝐎 𝐙𝐀𝐎
07-06-2026
𝐌𝐖𝐄𝐍𝐄𝐙𝐈 𝐀𝐏𝐎𝐊𝐄𝐋𝐄𝐖𝐀 𝐇𝐀𝐍𝐀𝐍𝐆’-𝐌𝐀𝐍𝐘𝐀𝐑𝐀
07-06-2026
𝐍𝐈 𝐍𝐙𝐀𝐌𝐔 𝐘𝐀 𝐌𝐊𝐎𝐀 𝐖𝐀 𝐌𝐀𝐍𝐘𝐀𝐑𝐀!
07-06-2026