Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


𝐑𝐀𝐈𝐒 𝐒𝐀𝐌𝐈𝐀 𝐑𝐀𝐒𝐌𝐈 𝐔𝐑𝐔𝐒𝐈, 𝐀𝐊𝐔𝐓𝐀𝐍𝐀 𝐍𝐀 𝐏𝐔𝐓𝐈𝐍

alternative

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, amepokelewa na kuakaribishwa rasmi na Rais wa Shirikisho la Urusi, Vladimir Putin, katika mazungumzo ya ngazi ya juu yaliyofanyika jijini Moscow, Urusi. Katika mazungumzo hayo, viongozi hao wamepongeza ukuaji wa mahusiano ya kibiashara kati ya Tanzania na Urusi uliofikia takribani asilimia 72 katika kipindi cha mwaka 2020 hadi 2025. Aidha, wamekubaliana kuendelea kuimarisha ushirikiano wa muda mrefu uliopo kati ya mataifa hayo kwa kuongeza fursa za biashara na uwekezaji, hatua inayolenga kuleta manufaa zaidi ya kiuchumi na ustawi wa wananchi wa pande zote mbili. Vilevile, viongozi hao wamejadili namna ya kuimarisha ushirikiano katika sekta mbalimbali za kimkakati zikiwemo sayansi na teknolojia, elimu, nishati, madini, kilimo, miundombinu na utalii. Tembelea: www.ccm.or.tz _______ #KazinaUtuTunasongaMbele #CCMIpoKazini #SamiaSuluhuHassan #Putin

alternative alternative alternative alternative alternative alternative alternative alternative alternative alternative
Habari Nyingine