Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


πŸ”° πŠπˆπ‡πŽππ†πŽπ’πˆ π€π–π€π’πˆπ‹πˆ πŠπ–π€ πŠπˆπ’π‡πˆππƒπŽ πŠπˆπ‹πˆπŒπ€ππ‰π€π‘πŽ

alternative

SIHA-KILIMANJARO: Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Kenani Kihongosi, leo Mei 29, 2026 amewasili mkoani Kilimanjaro kuanza ziara yake ya kikazi katika mikoa ya Kanda ya Kaskazini. Mkoa wa Kilimanjaro ni mkoa wa 10 kutembelewa na Kihongosi katika ziara zake zinazolenga kukagua uhai wa chama, kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo pamoja na kusikiliza na kutatua kero za wananchi. Mara baada ya kuwasili mkoani humo, Kihongosi alianza rasmi ziara yake katika Wilaya ya Siha ambapo alipokelewa katika Kijiji cha Lawate, Kata ya Kirua. Katika ziara hiyo, anatarajiwa kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo Kilimanjaro Girls Secondary School pamoja na ujenzi wa Hospitali ya Kibong’oto. Aidha, Kihongosi atatembelea Shina namba tisa kwa ajili ya kuangalia uhai wa chama kabla ya kufanya mkutano wa hadhara utakaofanyika katika viwanja vya stendi ya mabasi Sanya Juu. _____________ #KaziNaUtuTunasongaMbele #MaendeleoYaWananchi #KandaYaKaskazini #KaziIendelee.

alternative alternative alternative alternative alternative alternative alternative
Habari Nyingine