Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


MAWENZI YAVUNJA REKODI: MITUNGI 3,313 YA OKSIJENI YAZALISHWA KWA MIEZI 6, ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 126 ZAOKOLEWA!

alternative

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mawenzi imeendelea kuonyesha matokeo makubwa ya uwekezaji wa Serikali ya Awamu ya Sita baada ya kuzalisha mitungi 3,313 ya oksijeni ndani ya miezi sita pekee tangu kuanza kwa mradi wa kisasa wa hewa tiba. Mradi huo wenye thamani ya Shilingi Bilioni 1.94 umeondoa changamoto ya upatikanaji wa oksijeni, kuimarisha huduma kwa wagonjwa mahututi na kuokoa zaidi ya Shilingi Milioni 126 zilizokuwa zikitumika kununua na kusafirisha oksijeni kutoka nje ya mkoa. Akikagua mradi huo, Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM Taifa, Kenani Kihongosi amesema mafanikio hayo ni matokeo ya dhamira thabiti ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuboresha sekta ya afya na kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora kwa wakati. #KaziIendelee #CCMImara #MamaYukoKazini #TanzaniaYaSamia

alternative alternative alternative alternative alternative alternative alternative alternative alternative
Habari Nyingine