RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI, AL HAJJ DK. HUSSEIN ALI MWINYI, AMEENDELEA KUIHIMIZA JAMII JUU YA UMUHIMU WA KUDUMISHA AMANI
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Al hajj Dk. Hussein Ali Mwinyi, ameendelea kuihimiza jamii juu ya umuhimu wa kudumisha amani na kubeba imani ya dhati ndani ya mioyo yao kwa mustakbali wa taifa na ustawi wa jamii bora kwa maendeleo ya uchumi endelevu nchini.
Al hajj Dk. Mwinyi, alitoa nasaha hizo kwenye Msikiti Mabuluu Mfereji wa Wima, Mkoa wa Mjini Magharibi, alikojumuika pamoja na waumini wa dini ya Kiislamu kwenye ibada ya sala ya Ijumaa.
Rais, Al hajj Mwinyi, aliieleza Imani na amani ni vitu viwili vinavyokwenda sambamba na kutegemeana wakati wote, hivyo aliisihi jamii kadri wanapokusanyika pamoja kwenye maisha yao ya kila siku, wasichoke kuamini na kuendelea kuhimiza amani ya nchi na kuidumisha muda wote katika kuyaendea mazuri yote kwa ustawi wa jamii njema na taifa kwa ujumla.
“Imani na amani vinakwenda sambamba, amani ndio dini yetu, Uislamu unatutaka tueneze amani wakati wote, amani ikikosekana mambo mengine yote hayawezekani na hili tunalijua kutokana na wenzetu wanayoyapitia huko kwenye mataifa ya wenzetu, tunaona sehemu zenye vita hata ibada hazifanyiki, ili ipatikane amani lazima tuwe na Imani ndani ya nyoyo zetu” alisisitiza Al hajj Mwinyi.
Al hajj Dk Mwinyi alieleza, kila mmoja anawajibu wa kuitunza na kueneza amani kwa mustakbali wa taifa na ustawi wa jamii iliyobora.
Pia, aliwahimiza waumini hao kuendelea kuliombea taifa na viongozi kwa ujumla ili kuendelea kuwaongoza vyema na kuyatekeleza yote waliyowaahidi wananchi.
Rais Al Hajj Mwinyi alieleza, viongozi wanamajukumu makubwa na kubeba dhima kubwa hivyo, aliwasihi wanaumini hao na jamii kwa ujumla wasichoke kuwaombea mazuri na kuzidi kuwaombea kheir kwa Mwenyezi Mungu (S. W).
Akitoa nasaha za Ijumaa, Katibu Mtendaji kutoka Ofisi ya Mufti Zanzibar, Sheikh Khalid Ali Mfaume, alisifu juhudi za Rais Al Hajj Dk. Mwinyi kwa Imani aliyoijenga kwa waumini wa dini ya kiislamu na taifa kwa ujumla ikiwemo kujumuika nao pamoja kwenye ibada katika misikiti mbalimbali nchini sambamba na kuwaboresha ustawi wa maendeleo na uchumi wananchi wote.
Alisema juhudi zote hizo ni Imani yake kwa Wazanzibari na taifa lote, hasa jitihada za kuendelea kuimarisha huduma za jamii, uchumi na maendeleo ikiwemo ujenzi wa miundombinu imara na kuboresha mawasiliano.
Naye, Khatibu wa sala ya Ijumaa msikitini hapo, Sheikh Abdul Karim Said Abdulla aliihusia jamii kuendelea kupendana na kutendeana mema kwa kujizuia kuudhiana na kutendea mabaya.
Aliwashajihisha waumini hao kuendeleza mshikamo kwa kudumisha amani, umoja na upendo baina yao kwa ustawi wa jamii iliyo njema.
𝐙𝐈𝐀𝐑𝐀 𝐘𝐀 𝐊𝐀𝐓𝐈𝐁𝐔 𝐖𝐀 𝐍𝐄𝐂, 𝐈𝐓𝐈𝐊𝐀𝐃𝐈, 𝐔𝐄𝐍𝐄𝐙𝐈 𝐍𝐀 𝐌𝐀𝐅𝐔𝐍𝐙𝐎 𝐖𝐀 𝐂𝐂𝐌 𝐓𝐀𝐈𝐅𝐀
16-06-2026
𝐂𝐂𝐌 𝐘𝐀𝐇𝐈𝐌𝐈𝐙𝐀 𝐒𝐈𝐀𝐒𝐀 𝐙𝐀 𝐊𝐈𝐒𝐓𝐀𝐀𝐑𝐀𝐁𝐔 𝐊𝐔𝐋𝐈𝐍𝐃𝐀 𝐀𝐌𝐀𝐍𝐈 𝐍𝐀 𝐔𝐓𝐔𝐋𝐈𝐕𝐔 𝐖𝐀 𝐍𝐂𝐇𝐈
16-06-2026
𝐕𝐈𝐊𝐔𝐍𝐃𝐈 𝐕𝐘𝐀 𝐊𝐈𝐉𝐀𝐌𝐈𝐈 𝐋𝐈𝐍𝐃𝐈 𝐕Y𝐀𝐌𝐒𝐇𝐔𝐊𝐔𝐑𝐔 𝐑𝐀𝐈𝐒 𝐒𝐀𝐌𝐈𝐀 𝐊𝐖𝐀 𝐌𝐈𝐊𝐎𝐏𝐎 𝐈𝐒𝐈𝐘𝐎 𝐍𝐀 𝐑𝐈𝐁𝐀
16-06-2026
𝐑𝐀𝐁𝐈𝐀: 𝐂𝐂𝐌 𝐈𝐍𝐀𝐓𝐇𝐀𝐌𝐈𝐍𝐈 𝐉𝐀𝐒𝐇𝐎 𝐋𝐀 𝐊𝐈𝐋𝐀 𝐌𝐓𝐀𝐍𝐙𝐀𝐍𝐈𝐀
16-06-2026
𝐁𝐀𝐀𝐃𝐇𝐈 𝐘𝐀 𝐍𝐔𝐊𝐔𝐔 𝐊𝐔𝐓𝐎𝐊𝐀 𝐌𝐊𝐔𝐓𝐀𝐍𝐎 𝐍𝐀 𝐖𝐀𝐀𝐍𝐃𝐈𝐒𝐇𝐈 𝐖𝐀 𝐇𝐀𝐁𝐀𝐑𝐈
16-06-2026
𝐌𝐊𝐔𝐓𝐀𝐍𝐎 𝐍𝐀 𝐖𝐀𝐀𝐍𝐃𝐈𝐒𝐇𝐈 𝐖𝐀 𝐇𝐀𝐁𝐀𝐑𝐈
16-06-2026
𝐍𝐔𝐊𝐔𝐔 𝐌𝐁𝐀𝐋𝐈𝐌𝐁𝐀𝐋𝐈 𝐙𝐀 𝐌𝐊𝐔𝐓𝐀𝐍𝐎
16-06-2026
𝐍𝐃𝐆. 𝐑𝐀𝐁𝐈𝐀 𝐀𝐏𝐎𝐊𝐄𝐋𝐄𝐖𝐀 𝐌𝐊𝐎𝐀 𝐖𝐀 𝐋𝐈𝐍𝐃𝐈 𝐊𝐔𝐀𝐍𝐙𝐀 𝐙𝐈𝐀𝐑𝐀 𝐘𝐀 𝐊𝐔𝐙𝐔𝐍𝐆𝐔𝐌𝐙𝐀 𝐍𝐀 𝐌𝐀𝐊𝐔𝐍𝐃𝐈 𝐌𝐁𝐀𝐋𝐈𝐌𝐁𝐀𝐋𝐈 𝐘𝐀 𝐊𝐈𝐉𝐀𝐌𝐈𝐈
16-06-2026
𝐂𝐂𝐌 𝐘𝐀𝐒𝐈𝐅𝐈𝐀 𝐌𝐀𝐄𝐍𝐃𝐄𝐋𝐄𝐎, 𝐘𝐀𝐎𝐍𝐘𝐀 𝐖𝐀𝐍𝐀𝐎𝐇𝐀𝐌𝐀𝐒𝐈𝐒𝐇𝐀 𝐔𝐕𝐔𝐍𝐉𝐈𝐅𝐔 𝐖𝐀 𝐀𝐌𝐀𝐍𝐈
16-06-2026
🔰𝐍𝐃𝐆. 𝐑𝐀𝐁𝐈𝐀 𝐊𝐔𝐙𝐔𝐍𝐆𝐔𝐌𝐙𝐀 𝐍𝐀 𝐌𝐀𝐊𝐔𝐍𝐃𝐈 𝐌𝐁𝐀𝐋𝐈𝐌𝐁𝐀𝐋𝐈 𝐘𝐀 𝐊𝐈𝐉𝐀𝐌𝐈𝐈, 𝐓𝐀𝐀𝐒𝐈𝐒𝐈, 𝐍𝐆𝐎'𝐒 𝐍𝐀 𝐕𝐘𝐀𝐌𝐀 𝐌𝐁𝐀𝐋𝐈𝐌𝐁𝐀𝐋𝐈 𝐕𝐘𝐀 𝐊𝐈𝐉𝐀𝐌𝐈𝐈
16-06-2026
📊 𝐕𝐈𝐏𝐀𝐔𝐌𝐁𝐄𝐋𝐄 𝐕𝐘𝐀 𝐁𝐀𝐉𝐄𝐓𝐈 𝐊𝐔𝐔 𝐘𝐀 𝐒𝐄𝐑𝐈𝐊𝐀𝐋𝐈 𝟐𝟎𝟐𝟔/𝟐𝟎𝟐𝟕
16-06-2026
📢 𝐌𝐊𝐔𝐓𝐀𝐍𝐎 𝐍𝐀 𝐖𝐀𝐀𝐍𝐃𝐈𝐒𝐇𝐈 𝐖𝐀 𝐇𝐀𝐁𝐀𝐑𝐈
16-06-2026
📢 𝐓𝐀𝐀𝐑𝐈𝐅𝐀 𝐘𝐀 𝐊𝐔𝐒𝐎𝐆𝐄𝐙𝐖𝐀 𝐊𝐖𝐀 𝐌𝐊𝐔𝐓𝐀𝐍𝐎 𝐖𝐀 𝐖𝐀𝐀𝐍𝐃𝐈𝐒𝐇𝐈 𝐖𝐀 𝐇𝐀𝐁𝐀𝐑𝐈
16-06-2026
𝐌𝐊𝐔𝐓𝐀𝐍𝐎 𝐍𝐀 𝐖𝐀𝐀𝐍𝐃𝐈𝐒𝐇𝐈 𝐖𝐀 𝐇𝐀𝐁𝐀𝐑𝐈
16-06-2026
KIPINDI MAALUMU
16-06-2026
𝐌𝐖𝐄𝐍𝐄𝐙𝐈 𝐊𝐄𝐍𝐀𝐍𝐈 𝐀𝐒𝐈𝐌𝐀𝐌𝐈𝐒𝐇𝐀 𝐌𝐒𝐀𝐅𝐀𝐑𝐀 𝐊𝐔𝐒𝐀𝐋𝐈𝐌𝐈𝐀 𝐖𝐀𝐍𝐀𝐍𝐂𝐇𝐈 𝐍𝐀 𝐊𝐈𝐉𝐈𝐖𝐄 𝐂𝐇𝐀 𝐂𝐇𝐀𝐃𝐄𝐌𝐀 𝐀𝐑𝐔𝐒𝐇𝐀 𝐌𝐉𝐈𝐍𝐈
16-06-2026
𝐌𝐖𝐄𝐍𝐄𝐙𝐈 𝐊𝐄𝐍𝐀𝐍𝐈 𝐀𝐓𝐄𝐌𝐁𝐄𝐋𝐄𝐀 𝐊𝐈𝐓𝐔𝐎 𝐂𝐇𝐀 𝐀𝐅𝐘𝐀 𝐊𝐀𝐋𝐎𝐋𝐄𝐍𝐈, 𝐀𝐑𝐔𝐒𝐇𝐀 𝐌𝐉𝐈𝐍𝐈
16-06-2026
𝐀𝐑𝐔𝐒𝐇𝐀 𝐘𝐀𝐀𝐌𝐁𝐈𝐖𝐀 𝐊𝐔𝐂𝐇𝐀𝐆𝐔𝐀 𝐌𝐀𝐄𝐍𝐃𝐄𝐋𝐄𝐎 𝐁𝐀𝐃𝐀𝐋𝐀 𝐘𝐀 𝐌𝐀𝐀𝐍𝐃𝐀𝐌𝐀𝐍𝐎
16-06-2026
𝐌𝐀𝐏𝐎𝐊𝐄𝐙𝐈 𝐘𝐀 𝐊𝐀𝐓𝐈𝐁𝐔 𝐖𝐀 𝐍𝐄𝐂, 𝐈𝐓𝐈𝐊𝐀𝐃𝐈, 𝐔𝐄𝐍𝐄𝐙𝐈 𝐍𝐀 𝐌𝐀𝐅𝐔𝐍𝐙𝐎 𝐂𝐂𝐌, 𝐍𝐃𝐔𝐆𝐔 𝐊𝐄𝐍𝐀𝐍𝐈 𝐋𝐀𝐁𝐀𝐍 𝐊𝐈𝐇𝐎𝐍𝐆𝐎𝐒𝐈, 𝐎𝐅𝐈𝐒𝐈 𝐙𝐀 𝐂𝐂𝐌 𝐖𝐈𝐋𝐀𝐘𝐀 𝐘𝐀 𝐀𝐑𝐔𝐒𝐇𝐀 𝐌𝐉𝐈𝐍𝐈
16-06-2026
𝐒𝐀𝐒𝐀 𝐍𝐈 𝐀𝐑𝐔𝐒𝐇𝐀 𝐌𝐉𝐈𝐍𝐈, 𝐌𝐖𝐄𝐍𝐃𝐎 𝐌𝐃𝐔𝐍𝐃𝐎!
16-06-2026