Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amesema Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar , imeridhishwa na hatua nzuri ya ujenzi wa skuli za Sekondari za ghorofa ( G+3 ) zinazojengwa na Kampuni ya Simba Developers Ltd katika kijiji cha Bumbwini Makoba na Bumbwini Misufini Wilaya ya Kaskazini “ B” Unguja
Akikagua maendeleo ya ujenzi wa skuli hizo pamoja na kumbi za Mitihani zinazojengwa katika skuli hizo, Mhe.Hemed amesema wakadarasi kutoka kampuni ya Simba Developers wanaendelea kuipatia heshima kampuni yao sambamba na kuendana na kasi ya serikali ya awamu ya nane ya kuwaletea maendeleo wananchi wake.
Amesema kuwa Serikali imekusudia kuondoa changamoto zote zinazowakabili wananchi wa mijini na vijijini ikiwemo chanagamoto ya msongamano wa wanfunzi madarasani na kuingia kwa mikondo miwili ya masomo hivyo ameitaka kampuni ya Simba Developers inayojenga Skuli hizo kuongeza kasi zaidi ili kuweze kumalizika kwa wakati ujenzi huo,
Aidha Mhe. Hemed ameitaka Wizara ya Elimu kukaa pamoja na viongozi wa Jimbo la Bumbwini kuangalia namna watakavyoifanyia ukarabati skuli ya Msingi ya Bumbwini Makoba na kuliangalia kwa umakini suala zima la ajira hasa katika kuajiri walimu wazawa ambao watasaidia kuondosha changamoto ya walimu kuchelewa kufika maskulini na kuzorotesha maendeleo katika Sekta ya Elimu.
Sambamba na hayo Makamu wa Pili wa Rais amesema Serikalini ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuzisimamia changamoto zote na kuzitafuta ufumbuzi na kuwaahidi wananchi wa Bumbwini waliotoa maeneo yao kupisha ujenzi wa miradi mbali mbali ya maendeleo kuwa Serikali itahakikisha inawapatia stahiki zao kwa mujibu wa taratibu na sheria.
Aidha Mhe. Hemed amewataka Wananchi wa Bubwini na wazanzibari kwa ujumla kuendelea kumuunga mkono Rais Dkt Hussen Mwinyi pamoja na Serikali zote mbili katika jitihada wanazozifanya za kuwaletea maendeleo na kuwataka kukipa mashirikiano chama cha Mapinduzi ili kiendele kushikilia dola katika uchaguzi Mkuu ujao wa mwaka 2020-2025, Sambamba na kuwasisitiza kuendelea kuitunza na kuidumisha amani iliyopo nchini kwani hakuna Taifa lolote litakalopiga hatua za kimaendeleo bila ya kuwa na Amani, Umoja na mshikamano.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Ali Abdulghulam Hussein amesema Mipango ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar ni kuhakikisha ifikapo Januari 2025 wanafunzi wote wa Zanzibar wawe wanaingia skuli kwa mkondo mmoja wa asubuhi pamoja na kuondoa changamoto ya msongamano wa wanafunzi madarasani.
Aidha Mhe. Ghulam amesisitiza kuwa vifaa vyote kwa ajili ya skuli mpya zinazojengwa na zinazofanyiwa ukarabati vipo tayari na hakuna skuli itakayokosa vifaa vya kufundishia na kusomea kwa wanafunzi wote wa Zanzibar.
Mhe. Ghulam amesema Serikali imeongeza Bajeti ya Wizara ya Elimu na kufikia zaidi ya Bilioni 800 kwa mwaka wa fedha 2024-2025 fedha ambazo zitatumika kwa ajili ya kujengea skuli za ghorofa za kisasa, kuzifanyia ukarabati skuli ambazo ni chakavu na kujenga madarasa mapya kwa lengo la kupunguza msongamano wa wanafunzi madarasani.
Kwa upande wake mkandarasi anaenjenga skuli hizo pamoja na kumbi za Mitihani Simba Developers Ltd amesema wapo katika hatua za mwisho za ujenzi na kuahidi kuwa mwishoni mwa mwezi wa saba wanatarajia kuzikabidhi skuli hizo Serikalini ili wanafunzi waweze kuendeleo na masomo yao katika skuli hizo.
Kampuni ya Simba Developers wamemshukuru Rais Dkt Mwinyi kwa kuwaamini na kuwapatia nafasi ya kujenga miradi mbali mbali ya amendeleo hapa Zanzibar na kuahidi kuwa watahakikisha wanajenga kwa ubora na kwa viwango vinavyokubalika ili majengo hayo yaweze kudumu na kutumika kwa muda mrefu pasipo na changamoto za aina yoyote za kiufundi.
Katika ziara hio Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar ametembelea ujenzi wa skuli ya Ghorofa ya Bumbwini Makoba, na Bumbwini Misufini na kumbi za Mikubtano . katika skuli hizo
𝐑𝐀𝐈𝐒 𝐒𝐀𝐌𝐈𝐀 𝐑𝐀𝐒𝐌𝐈 𝐔𝐑𝐔𝐒𝐈, 𝐀𝐊𝐔𝐓𝐀𝐍𝐀 𝐍𝐀 𝐏𝐔𝐓𝐈𝐍
04-06-2026
𝐊𝐈𝐋𝐈𝐌𝐀𝐍𝐉𝐀𝐑𝐎, 𝐓𝐔𝐍𝐀𝐊𝐔𝐉𝐀
04-06-2026
𝐑𝐀𝐈𝐒 𝐃𝐊𝐓. 𝐒𝐀𝐌𝐈𝐀 𝐀𝐖𝐀𝐒𝐈𝐋𝐈 𝐌𝐎𝐒𝐂𝐎𝐖, 𝐔𝐑𝐔𝐒𝐈 𝐊𝐖𝐀 𝐙𝐈𝐀𝐑𝐀 𝐘𝐀 𝐊𝐈𝐓𝐀𝐈𝐅𝐀
04-06-2026
𝐌𝐖𝐄𝐍𝐄𝐙𝐈 𝐖𝐀 𝐂𝐂𝐌 𝐓𝐀𝐈𝐅𝐀 𝐀𝐖𝐀𝐒𝐈𝐋𝐈 𝐖𝐈𝐋𝐀𝐘𝐀 𝐘𝐀 𝐒𝐈𝐌𝐀𝐍𝐉𝐈𝐑𝐎 𝐊𝐖𝐀 𝐙𝐈𝐀𝐑𝐀 𝐘𝐀 𝐊𝐈𝐊𝐀𝐙𝐈
04-06-2026
𝐅𝐔𝐍𝐆𝐀 𝐊𝐀𝐙𝐈 𝐌𝐊𝐎𝐀 𝐖𝐀 𝐌𝐀𝐍𝐘𝐀𝐑𝐀 𝐋𝐄𝐎!!!
04-06-2026
𝐊𝐈𝐇𝐎𝐍𝐆𝐎𝐒𝐈 𝐀𝐓𝐄𝐌𝐁𝐄𝐋𝐄𝐀 𝐒𝐇𝐈𝐍𝐀 𝐍𝐀. 𝟐 𝐊𝐀𝐓𝐀 𝐘𝐀 𝐁𝐎𝐍𝐆𝐀
04-06-2026
𝐁𝐀𝐁𝐀𝐓𝐈 𝐌𝐉𝐈𝐍𝐈 𝐋𝐄𝐎 𝐓𝐔𝐍𝐀𝐈𝐅𝐔𝐍𝐈𝐊𝐀!!!
04-06-2026
𝐊𝐈𝐇𝐎𝐍𝐆𝐎𝐒𝐈 𝐀𝐊𝐔𝐓𝐀𝐍𝐀 𝐍𝐀 𝐖𝐀𝐍𝐀𝐍𝐂𝐇𝐈 𝐇𝐀𝐍𝐀𝐍𝐆, 𝐀𝐒𝐈𝐊𝐈𝐋𝐈𝐙𝐀 𝐍𝐀 𝐊𝐔𝐓𝐀𝐓𝐔𝐀 𝐊𝐄𝐑𝐎 𝐙𝐀𝐎
04-06-2026
𝐌𝐖𝐄𝐍𝐄𝐙𝐈 𝐀𝐏𝐎𝐊𝐄𝐋𝐄𝐖𝐀 𝐇𝐀𝐍𝐀𝐍𝐆’-𝐌𝐀𝐍𝐘𝐀𝐑𝐀
04-06-2026
𝐍𝐈 𝐍𝐙𝐀𝐌𝐔 𝐘𝐀 𝐌𝐊𝐎𝐀 𝐖𝐀 𝐌𝐀𝐍𝐘𝐀𝐑𝐀!
04-06-2026
🔰𝐀𝐒𝐀𝐍𝐓𝐄𝐍𝐈 𝐒𝐀𝐍𝐀 𝐖𝐀𝐍𝐀𝐍𝐂𝐇𝐈 𝐖𝐀 𝐊𝐈𝐋𝐈𝐌𝐀𝐍𝐉𝐀𝐑𝐎!
04-06-2026
𝐒𝐇𝐔𝐋𝐄 𝐘𝐀 𝐌𝐒𝐈𝐍𝐆𝐈 𝐊𝐖𝐀 𝐒𝐀𝐃𝐀𝐋𝐀 𝐘𝐀𝐎𝐍𝐃𝐎𝐀 𝐊𝐄𝐑𝐎 𝐘𝐀 𝐊𝐔𝐓𝐄𝐌𝐁𝐄𝐀 𝐊𝐈𝐋𝐎𝐌𝐄𝐓𝐀 𝟏𝟐 𝐊𝐖𝐀 𝐖𝐀𝐍𝐀𝐅𝐔𝐍𝐙𝐈
04-06-2026
𝐌𝐖𝐄𝐍𝐄𝐙𝐈 𝐖𝐀 𝐂𝐂𝐌 𝐓𝐀𝐈𝐅𝐀 𝐀𝐀𝐍𝐙𝐀 𝐙𝐈𝐀𝐑𝐀 𝐖𝐈𝐋𝐀𝐘𝐀𝐍𝐈 𝐇𝐀𝐈, 𝐊𝐈𝐋𝐈𝐌𝐀𝐍𝐉𝐀𝐑𝐎
04-06-2026
𝐌𝐖𝐄𝐍𝐄𝐙𝐈 𝐖𝐀 𝐂𝐂𝐌 𝐓𝐀𝐈𝐅𝐀 𝐀𝐀𝐍𝐙𝐀 𝐙𝐈𝐀𝐑𝐀 𝐖𝐈𝐋𝐀𝐘𝐀 𝐘𝐀 𝐇𝐀𝐈 𝐌𝐊𝐎𝐀 𝐖𝐀 𝐊𝐈𝐋𝐈𝐌𝐀𝐍𝐉𝐀𝐑𝐎
04-06-2026
𝐍𝐈 𝐌𝐔𝐃𝐀 𝐖𝐀 𝐖𝐀𝐍𝐀𝐇𝐀𝐈-𝐊𝐈𝐋𝐈𝐌𝐀𝐍𝐉𝐀𝐑𝐎 𝐒𝐀𝐒𝐀
04-06-2026
𝐑𝐀𝐈𝐒 𝐒𝐀𝐌𝐈𝐀 𝐀𝐌𝐏𝐀 𝐁𝐀𝐉𝐀𝐉𝐈 𝐌𝐊𝐀𝐙𝐈 𝐖𝐀 𝐒𝐈𝐇𝐀 𝐌𝐖𝐄𝐍𝐘𝐄 𝐔𝐋𝐄𝐌𝐀𝐕𝐔 𝐖𝐀 𝐌𝐈𝐆𝐔𝐔
04-06-2026
MAWENZI YAVUNJA REKODI: MITUNGI 3,313 YA OKSIJENI YAZALISHWA KWA MIEZI 6, ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 126 ZAOKOLEWA!
04-06-2026
MAFURIKO YA WANANCHI WA SIHA KWENYE MKUTANO MKUBWA WA HADHARA
04-06-2026
MAPOKEZI YA KATIBU MWENEZI WA CCM NDUGU KENANI L KIHONGOSI MKOANI KILIMANJARO
04-06-2026
🔰 𝐊𝐈𝐇𝐎𝐍𝐆𝐎𝐒𝐈 𝐀𝐖𝐀𝐒𝐈𝐋𝐈 𝐊𝐖𝐀 𝐊𝐈𝐒𝐇𝐈𝐍𝐃𝐎 𝐊𝐈𝐋𝐈𝐌𝐀𝐍𝐉𝐀𝐑𝐎
04-06-2026