MJUMBE WA KAMATI KUU YA HALMASHAURI KUU YA CCM TAIFA NDUGU HEMED SULEIMAN ABDULLA AMESEMA CHAMA CHA MAPINDUZI KIMEJIPANGA KUHAKIKISHA MAJIMBO YOTE YANABAKI KUWA CHINI YA CCM IFIKIA UCHAGUZI WA DOLA WA MWAKA 2025.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Ndugu Hemed Suleiman Abdulla amesema Chama Cha Mapinduzi kimejipanga kuhakikisha Majimbo yote yanabaki kuwa chini ya CCM ifikia Uchaguzi wa Dola wa mwaka 2025. Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ameyasema hayo wakati akizungumza na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi Jimbo la Chumbuni na Jimbo la Mpendae katika muendelezo wa ziara yake ya kuimarisha Chama.
Amesema CCM inaendelea na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2020-2025 ambapo tayari miradi mbali mbali imeshakamilika na mengine inaendelea kujengwa ambacho ni kielelezo kikubwa cha wananchi kukikubali Chama hicho hivyo, ni vyema kuendelea kuchukua jitihada ili kukiimarisha na kiweze kuendelea kushika Dola. Mhe. Hemed ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inayoongozwa ja Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi inaendelea kutekeleza Ilani ya CCM kwa kujenga miradi mbali mbali ambayo kukamilika kwake itazalisha ajira ambazo vijana watanufaika kwa ajili ya kujipatia kipato na kupunguza ukali wa maisha.
Aidha ameeleza kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi pamoja na wasaidizi wake wote wamekuwa mstari wa mbele kuhakikisha wanawatumika vyema wananchi wa Zanzibar kuhakikisha wanawasogezea huduma muhimu wananchi hao waliowachagua na kukikiweka madarakani Chama Cha Mapinduzi.
Pamoja na hayo Mhe. Hemed ameupongeza uongozi wa Jimbo la Chumbuni kwa kuendelea kuhakikisha wanaongeza Idadi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi hatua ambayo inaonesha wazi uwajibikaji wa Viongozi wa Jimbo hilo katika kuwatumikia wananchi wao. Amewakumbusha Viongozi wa Jimbo la Chumbuni na Jimbo la Mpendae Wilaya ya Amani kichama kuhakikisha kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2025 ahadi zote walizoziahidi kwa wananchi wamezitekeleza ili kuwazidishia imani wana CCM na wananchi kwa ujumla.
Kwa upande wake Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Ndugu Sufiani Khamis Ramadhan amemshukuru Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Ndugu. Hemed Suleiman Abdulla kwa kuamua kufanya ziara ya kuimarisha Chama kwa Majimbo yote ya Zanzibar hatua ambayo inazidisha ari na hamasa kwa wanachama wa CCM juu ya uimara wa Chama hicho. Ameeleza kuwa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar kinaridhishwa na kasi ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025 chini ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi kasi ambayo inadhihirisha nia thabiti na dhamira ya Dkt. Mwinyi kuwatumikia wazanzibari.
Nae Mjumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Mjini Ndg. Idriss Kitwana Mustafa ambae pia ni Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi amemuahidi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kuwa Serikali ya Mkoa wa Mjini Magharibi itaendelea kusimamia Amani na Utulivu uliopo ili Serikali iweze kutekeleza vyema majukumu yake ya kusimamia Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2020-2025. Aidha amewasisitiza wanachama wa Chama Cha Mapinduzi kuhubiri Amani na utulivu uliopo na kuepuka makundi yanayokigawa Chama.
Nao wanachama na wananchi wa majimbo hayo wamesema utekelezaji wa ahadikwa chama cha mapinduzi umepitiliza Zaidi ya makadirio hivyo, ahadi yao kwa CCM ni kuhakikisha ifikapo Uchaguzi wa 2023 kuendelea kukiweka tena madarakani Chama Cha Mapinduzi.
DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AONGOZA KIKAO MAALUMU CHA KAMATI KUU YA CCM
09-12-2025
RAIS SAMIA AKIWAAPISHA MAWAZIRI NA MANAIBU WAZIRI WATEULE- IKULU CHAMWINO DODOMA
09-12-2025
WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU NCHEMBA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA DODOMA (GENERAL)
09-12-2025
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ..
09-12-2025
RAIS SAMIA AKIHUTUBIA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
09-12-2025
DKT SAMIA:TUNAFANYA UCHAGUZI KWA FEDHA ZETU WENYEWE
09-12-2025
MGOMBEA URAIS KUPITIA CCM DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA MANYARA
09-12-2025
π¨ππππ£πππππ πͺπ πππ§. π¦ππ ππ π¨π ππππ§π ππ ππ‘π ππͺπ πͺππ£ππ‘πππ‘π, πͺππππ¨ππππ πππ
πππ©πππͺ ππ πͺπͺ πΏπ π©. πππππ§π€ ππ¬ππ₯π€π ππ πππ€π£ππ€π―π π¬π πΎππΌπΏπππΌ π£π πΌπΎπ
09-12-2025
πππ§. π¦ππ ππ ππ§π¨π π‘πππ‘π π¬π ππ₯πππ π¬π ππππ’π π
09-12-2025
KATIBU MKUU WA CCM, BALOZI DKT. ASHA-ROSE MIGIRO AKUTANA NA RAIS MWINYI – ZANZIBAR
09-12-2025
ILANI YA UCHAGUZI YA CCM 2025-2030
09-12-2025
WASIRA:CCM HATUKATI MGOMBEA ILA TUNATEUA WACHACHE KATI YA WENGI
09-12-2025
WANACHAMA 280 WA CHADEMA WATIMKIA CCM
09-12-2025
BALOZI NCHIMBI: MAONI YOYOTE KUHUSU AMANI YA TANZANIA HAYATAPUUZWA
09-12-2025
π¦ππ₯πππππ π¬π π₯πππ¦ πππ§. π¦ππ ππ ππ ππͺπππ ππππ π π¬π π πππ‘πππππ’ ππππ π¦ππππ π¨ - ππ£π. ππ π’π¦ π ππππππ
09-12-2025
MAKALLA: BARABARA YA MPWAPWA NJIAPANDA KONGWA KUJENGWA LAMI
09-12-2025
BALOZI NCHIMBI AWASILI ARUSHA
09-12-2025
TAARIFA KWA UMMA
09-12-2025
UCHAGUZI MKUU SIO AJALI-WASIRA
09-12-2025
πͺπππ¨π ππ π π¦ππππππ¨π π©ππ’π‘ππ’ππ ππππππππ ππͺππ‘π¬π ππ¨π₯π ππ π ππ’π‘π - (π ππ) πππ©π¨
09-12-2025