MABALOZI WA MAREKANI, INDIA, ALGERIA, NA UGANDA WAWAPONGEZA DKT. SAMIA, BALOZI NCHIMBI NA DKT. MWINYI
Jumuiya ya kimataifa, hususan mabalozi wa nchi mbalimbali waliopo Tanzania, ikiwa ni pamoja na Uganda, Algeria, India na Marekani, wamepongeza uteuzi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu.
Mbali na kumpongeza Dkt. Samia, ambaye ni Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mabalozi hao pia wamewapongeza Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi kwa kuteuliwa kuwa mgombea mwenza wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa kuthibitishwa kuwa mgombea wa urais wa Zanzibar.
Mabalozi hao walitoa pongezi hizo wakati wa mazungumzo yao na Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, yaliyofanyika kwa nyakati tofauti leo, tarehe 12 Februari 2025, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, jijini Dar es Salaam.
Katika mazungumzo yake na Katibu Mkuu wa CCM, Balozi wa Algeria nchini Tanzania, Mhe. Ahmed Djellal, aliangazia pia uhusiano wa kihistoria kati ya Tanzania na Algeria, hususan mchango wa Tanzania katika harakati za ukombozi wa Afrika. Aidha, alitoa pongezi kwa Rais Dkt. Samia, Rais Dkt. Mwinyi na Balozi Nchimbi kwa kuaminiwa kupeperusha bendera ya CCM katika Uchaguzi Mkuu ujao.
Balozi Nchimbi na Balozi Djellal pia walijadili umuhimu wa kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi baina ya Tanzania na Algeria kupitia sekta mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kubadilishana uzoefu wa kiuongozi na fursa za masomo.
Katika mazungumzo yake na Katibu Mkuu wa CCM, Balozi wa India nchini Tanzania, Mhe. Bishwadip Dey, alieleza kuwa uhusiano kati ya Tanzania na India umeendelea kuimarika na kunufaisha pande zote mbili, hususan katika sekta za biashara, uwekezaji, teknolojia na afya. Pia, alitoa pongezi kwa CCM kwa kuwaamini Rais Dkt. Samia, Rais Dkt. Mwinyi na Balozi Nchimbi kuwa wagombea wake katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.
Vilevile, katika mazungumzo kati ya Balozi Nchimbi na Naibu Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Mhe. Andrew Lentz, pande zote zilisisitiza umuhimu wa kuendeleza uhusiano wa muda mrefu kati ya Tanzania na Marekani katika nyanja mbalimbali. Mhe. Lentz pia alitoa pongezi zake na kuwatakia kila la heri Rais Dkt. Samia, Rais Dkt. Mwinyi na Balozi Nchimbi kufuatia maamuzi ya Mkutano Mkuu Maalum wa CCM.
Kwa upande wake, Balozi wa Uganda nchini Tanzania, Mhe. Kanali Mstaafu Fred Mwesigye, alifikisha salamu za pongezi kutoka kwa Serikali ya Uganda na chama tawala cha NRM, akieleza kuwa Uganda inatambua na kuheshimu mchango wa Tanzania na CCM katika harakati za ukombozi wa Afrika. Alimhakikishia Balozi Nchimbi kuwa uhusiano wa kidugu kati ya Tanzania na Uganda utaendelea kuimarika kwa manufaa ya wananchi wa pande zote mbili.
Mhe. Balozi Mwesigye alisisitiza kuwa urafiki wa kihistoria kati ya Tanzania na Uganda umejengwa juu ya misingi imara ya mshikamano wa kikanda, ushirikiano wa kisiasa na maendeleo ya kiuchumi, ambao utaendelea kuimarika kwa ustawi wa mataifa hayo mawili.
NAIBU KATIBU MKUU WA CCM BARA AMWAKILISHA KATIBU MKUU WA CCM KWENYE MSIBA WA MBUNGE WA JIMBO LA PERAMIHO
05-01-2026
π©ππππ‘π π§π¨ππππ‘ππ ππ ππ‘π π¬π π‘πππ π¬ππ§π¨ - π πͺππ‘πππ πππ‘ππ‘π
05-01-2026
DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AONGOZA KIKAO MAALUMU CHA KAMATI KUU YA CCM
05-01-2026
RAIS SAMIA AKIWAAPISHA MAWAZIRI NA MANAIBU WAZIRI WATEULE- IKULU CHAMWINO DODOMA
05-01-2026
WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU NCHEMBA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA DODOMA (GENERAL)
05-01-2026
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ..
05-01-2026
RAIS SAMIA AKIHUTUBIA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
05-01-2026
DKT SAMIA:TUNAFANYA UCHAGUZI KWA FEDHA ZETU WENYEWE
05-01-2026
MGOMBEA URAIS KUPITIA CCM DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA MANYARA
05-01-2026
π¨ππππ£πππππ πͺπ πππ§. π¦ππ ππ π¨π ππππ§π ππ ππ‘π ππͺπ πͺππ£ππ‘πππ‘π, πͺππππ¨ππππ πππ
πππ©πππͺ ππ πͺπͺ πΏπ π©. πππππ§π€ ππ¬ππ₯π€π ππ πππ€π£ππ€π―π π¬π πΎππΌπΏπππΌ π£π πΌπΎπ
05-01-2026
πππ§. π¦ππ ππ ππ§π¨π π‘πππ‘π π¬π ππ₯πππ π¬π ππππ’π π
05-01-2026
KATIBU MKUU WA CCM, BALOZI DKT. ASHA-ROSE MIGIRO AKUTANA NA RAIS MWINYI – ZANZIBAR
05-01-2026
ILANI YA UCHAGUZI YA CCM 2025-2030
05-01-2026
WASIRA:CCM HATUKATI MGOMBEA ILA TUNATEUA WACHACHE KATI YA WENGI
05-01-2026
WANACHAMA 280 WA CHADEMA WATIMKIA CCM
05-01-2026
BALOZI NCHIMBI: MAONI YOYOTE KUHUSU AMANI YA TANZANIA HAYATAPUUZWA
05-01-2026
π¦ππ₯πππππ π¬π π₯πππ¦ πππ§. π¦ππ ππ ππ ππͺπππ ππππ π π¬π π πππ‘πππππ’ ππππ π¦ππππ π¨ - ππ£π. ππ π’π¦ π ππππππ
05-01-2026
MAKALLA: BARABARA YA MPWAPWA NJIAPANDA KONGWA KUJENGWA LAMI
05-01-2026
BALOZI NCHIMBI AWASILI ARUSHA
05-01-2026
TAARIFA KWA UMMA
05-01-2026