Dk. Hussein Ali Mwinyi "Sera ya Uchumi wa Buluu ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ina dhamira njema ya kuimarisha uchumi wa nchi kwa haraka na uhakika wa upatikanaji wa maendeleo endelevu ya vyanzo vya nishati ya uhakika".
Rais Dk. Mwinyi ameyasema hayo ukumbi wa hoteli ya Golden Tulip, Uwanja wa ndege Mkoa wa Mjini Magharibi alipozindua Duru ya kwanza ya utoaji wa vitalu kwa kampuni kwenye maeneo ya bahari kwa Zanzibar. Alisema, katika utekelezaji wa dhana ya Uchumi wa Buluu, Serikali inatoa fursa kubwa kwa wawekezaji wa sekta ya Mafuta na Gesi Asilia na kuwahakikishia mazingira rafiki ya utekelezaji wa shughuli hizo.
Rais Dk. Mwinyi alieleza kuwa eneo la Zanzibar limepata sifa ya kutambulika kuwa ni mahali pazuri kwa makampuni kuwekeza kwani ni maeneo salama. Pia, alisema Serikali inaamini fursa zinazotokana na Uchumi wa Buluu zitakuza mipango ya maendeleo ya uchumi yenye lengo la kupunguza umaskini na kutengeneza ajira nyingi nchini.
Vile vile Rais Dk. Mwinyi alieleza dhamira ya Serikali kuzindua duru ya kwanza ya utoaji wa Vitalu, awali ilifanya mapitio ya mifumo ya sheria na mikataba ya Mafuta na Gesi Asilia ili kuvutia uwekezaji, iliolenga kuimarisha masharti ya fedha sambamba na
kuimarisha mazingira rafiki ya uwekezaji kwenye sekta ya mafuta na gesi Asilia Zanzibar.
Dk. Mwinyi pia alieleza matarajio yake mara baada ya uzinduzi huo, kwamba utasaidia kufungua na kuharakisha shughuli za utafutaji wa mafuta na gesi asilia kwenye vitalu hivyo vipya vya baharini na hatimae kuitangaza Zanzibar kuwa sehemu ya uwekezaji
wa mafuta na gesi asilia. Hata hivyo, Rais Dk. Mwinyi aliwahakikishia wawekezaji wote wa sekta ya mafuta na gesi pamoja na sekta nyengine za uchumi kwamba, Serikali iko tayari kuwawekea mazingira mazuri ya uwekezaji kwa taifa kwa ujumla.
Naye, Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi, Shaaban Ali Othman alisema Sekta ya Uchumi wa Buluu kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ni miongoni mwa maeneo makuu ya vipaumbele vyake. Shughuli za utafutaji wa Mafuta na Gesi Asilia Zanzibar, zilianza tangu miaka ya 1950 kwa kampuni ya mafuta ya British Petroleum (BP) kushirikiana na Kampuni ya Shell zilipofanya uchunguzi wa kina na kuchimba visima viwili kwa visiwa vya Zanzibar vilivyokamilika baadae mwaka 1963 na kutoa msingi mzuri wa kuendeleza shughuli za Mafuta na Gesi Asilia Zanzibar.
Mwaka 1964, baada ya Mapinduzi ya Zanzibar na Muungano wa Tanzania, shughuli za utafutaji wa mafuta na gesi zilikua chini ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Shirika la Maendeleo la Petroli Tanzania (TPDC) na kufanikiwa
kufanya tafiti mbalimbali. Aidha, hatua mpya ya maendeleo ya sekta ya mafuta na gesi Zanzibar ilianzishwa mwaka 2015 kufuatia kupitishwa kwa Sheria ya Petroli Na 21 ya mwaka 2015 ya Tanzania iliyoiruhusu kila upande wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kusimamia shughuli za Mafuta na Gesi Asilia wenyewe.
🔰𝐀𝐒𝐀𝐍𝐓𝐄𝐍𝐈 𝐒𝐀𝐍𝐀 𝐖𝐀𝐍𝐀𝐍𝐂𝐇𝐈 𝐖𝐀 𝐊𝐈𝐋𝐈𝐌𝐀𝐍𝐉𝐀𝐑𝐎!
31-05-2026
𝐒𝐇𝐔𝐋𝐄 𝐘𝐀 𝐌𝐒𝐈𝐍𝐆𝐈 𝐊𝐖𝐀 𝐒𝐀𝐃𝐀𝐋𝐀 𝐘𝐀𝐎𝐍𝐃𝐎𝐀 𝐊𝐄𝐑𝐎 𝐘𝐀 𝐊𝐔𝐓𝐄𝐌𝐁𝐄𝐀 𝐊𝐈𝐋𝐎𝐌𝐄𝐓𝐀 𝟏𝟐 𝐊𝐖𝐀 𝐖𝐀𝐍𝐀𝐅𝐔𝐍𝐙𝐈
31-05-2026
𝐌𝐖𝐄𝐍𝐄𝐙𝐈 𝐖𝐀 𝐂𝐂𝐌 𝐓𝐀𝐈𝐅𝐀 𝐀𝐀𝐍𝐙𝐀 𝐙𝐈𝐀𝐑𝐀 𝐖𝐈𝐋𝐀𝐘𝐀𝐍𝐈 𝐇𝐀𝐈, 𝐊𝐈𝐋𝐈𝐌𝐀𝐍𝐉𝐀𝐑𝐎
31-05-2026
𝐌𝐖𝐄𝐍𝐄𝐙𝐈 𝐖𝐀 𝐂𝐂𝐌 𝐓𝐀𝐈𝐅𝐀 𝐀𝐀𝐍𝐙𝐀 𝐙𝐈𝐀𝐑𝐀 𝐖𝐈𝐋𝐀𝐘𝐀 𝐘𝐀 𝐇𝐀𝐈 𝐌𝐊𝐎𝐀 𝐖𝐀 𝐊𝐈𝐋𝐈𝐌𝐀𝐍𝐉𝐀𝐑𝐎
31-05-2026
𝐍𝐈 𝐌𝐔𝐃𝐀 𝐖𝐀 𝐖𝐀𝐍𝐀𝐇𝐀𝐈-𝐊𝐈𝐋𝐈𝐌𝐀𝐍𝐉𝐀𝐑𝐎 𝐒𝐀𝐒𝐀
31-05-2026
𝐑𝐀𝐈𝐒 𝐒𝐀𝐌𝐈𝐀 𝐀𝐌𝐏𝐀 𝐁𝐀𝐉𝐀𝐉𝐈 𝐌𝐊𝐀𝐙𝐈 𝐖𝐀 𝐒𝐈𝐇𝐀 𝐌𝐖𝐄𝐍𝐘𝐄 𝐔𝐋𝐄𝐌𝐀𝐕𝐔 𝐖𝐀 𝐌𝐈𝐆𝐔𝐔
31-05-2026
MAWENZI YAVUNJA REKODI: MITUNGI 3,313 YA OKSIJENI YAZALISHWA KWA MIEZI 6, ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 126 ZAOKOLEWA!
31-05-2026
MAFURIKO YA WANANCHI WA SIHA KWENYE MKUTANO MKUBWA WA HADHARA
31-05-2026
MAPOKEZI YA KATIBU MWENEZI WA CCM NDUGU KENANI L KIHONGOSI MKOANI KILIMANJARO
31-05-2026
🔰 𝐊𝐈𝐇𝐎𝐍𝐆𝐎𝐒𝐈 𝐀𝐖𝐀𝐒𝐈𝐋𝐈 𝐊𝐖𝐀 𝐊𝐈𝐒𝐇𝐈𝐍𝐃𝐎 𝐊𝐈𝐋𝐈𝐌𝐀𝐍𝐉𝐀𝐑𝐎
31-05-2026
CCM INAWATAKIA HERI YA SIKUKUU YA EID AL ADHA
31-05-2026
🔰VYAMA VYA UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA VYAIMARISHA MSHIKAMANO, DKT. DIMWA AHITIMISHA MAFUNZO MAALUM
31-05-2026
KATIBU WA NEC, ITIKADI, UENEZI NA MAFUNZO CCM TAIFA NDUGU KENANI KIHONGOSI AMNADI MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA ISIMANI EMMANUELA KAGANDA MTATIFIKOLO
31-05-2026
MUENDELEZO WA MAFUNZO YA VIONGOZI KATIKA SHULE YA UONGOZI YA MWALIMU JULIUS NYERERE – KIBAHA
31-05-2026
SIKU YA KWANZA YA MAFUNZO KATIKA SHULE YA UONGOZI YA MWALIMU JULIUS NYERERE LEADERSHIP SCHOOL.
31-05-2026
UFUNGUZI WA MAFUNZO YA VYAMA SITA RAFIKI VYA UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA
31-05-2026
MHE. DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA MJUMBE WA KAMATI KUU YA CPC, KOMREDI LIU HAIXING IKULU DAR ES SALAAM
31-05-2026
KIKAO CHA KAMATI KUU YA HALMASHAURI KUU YA CCM
31-05-2026
CCM NA FRELIMO KUIMARISHA USHIRIKIANO WA KIUCHUMI
31-05-2026
UZINDUZI WA JENGO LA MAKAO MAKUU YA ULINZI WA TAIFA
31-05-2026