Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


π—₯π—”π—œπ—¦ π——π—žπ—§. π—¦π—”π— π—œπ—” π—”π—¦π—œπ—¦π—œπ—§π—œπ—­π—” π— π—”π—›π—”π—žπ—”π— π—” π—žπ—¨π—˜π—‘π——π—˜π—Ÿπ—˜π—” π—žπ—¨π—§π—’π—” π—›π—”π—žπ—œ

alternative

π˜Όπ™¨π™šπ™’π™– π™Žπ™šπ™§π™žπ™ π™–π™‘π™ž 𝙠π™ͺπ™šπ™£π™™π™šπ™‘π™šπ™– 𝙠π™ͺ𝙩𝙀𝙖 π™ͺπ™¨π™π™žπ™§π™žπ™ π™žπ™–π™£π™€ 𝙒𝙯π™ͺπ™§π™ž 𝙠𝙬𝙖 𝙒π™ͺπ™π™žπ™’π™žπ™‘π™ž 𝙝π™ͺ𝙀.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesisitiza Mahakama ya Tanzania kuendelea kusimamia haki nchini huku akiahidi kwamba serikali yake anayoiongoza itaendelea kutoa ushirikiano wake kwa muhimili huo.

Rais Dkt. Samia amebainisha hayo wakati akimuapisha Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mhe. George Mcheche Masaju, ambaye ameapishwa kuwa Jaji wa saba Mzawa wa Mahakama ya Tanzania, akichukua nafasi ya Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma ambaye amestaafu utumishi wake.

Katika maelezo yake kwa Jaji Mkuu Mhe. Masaju, Rais Dkt. Samia amesisitiza umuhimu wa kuendelezwa mazuri ya Mahakama hiyo, kuendeleza utekelezaji wa mapendekezo ya Tume ya haki jinai sambamba na kuendelea kusimamia haki ndani ya nchi na haki za Tanzania nje ya nchi.

Katika baadhi ya nukuu ya hotuba yake, Rais Dkt. Samia ametoa pongezi kwa Jaji mstaafu na Jaji mpya.

"Pongezi zangu ni kwa Jaji Mkuu mstaafu kwa kukamilisha kazi hii bila ya makandokando lakini pia kwa Jaji Mkuu mpya nikupongeze lakini pia nikupe pole kwasababu mzigo huu sio mdogo."

"Una kazi ya kufanya, nakutakia kila la kheri, Mungu akupe busara na hekima uweze kuifanya kazi hii vyema."

πŸ—“οΈ15 Juni 2025
#OktobaTunatiki
#KaziNaUtuTunasongaMbele

alternative alternative alternative alternative
Habari Nyingine