RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI, DK. HUSSEIN ALI MWINYI AMEWAKARIBISHA ZANZIBAR WAFANYABIASHARA WAKUBWA NA WENYE VIWANDA KUTOKA CHINA.
Akizungumza na Makamo Mwenyekiti wa Shirikisho la wenye viwanda na wafanyabiashara wa China, Xu Lejiang na ujumbbe wa wafanyabiashara 15 Ikulu, Zanzibar, Rais Dk. Mwinyi aliwaeleza wafanyabiashara hao, utalii ni fursa muhimu ya uwekezaji kwa Zanzibar. Aliwaeleza utalii hasa wa hoteli na maeneo ya kupumzikia unafursa nyingi za uwekezaji, kwani Zanzibar ina maeneo mazuri ya fukwe nyeupe zinazowavutia wageni na watalii wengi.
Kuhusu sekta ya Uchumi wa Buluu, Rais Dk. Mwinyi aliwakaribisha wafanyabiashara hao kuangalia fursa eneo hilo kwani Zanzibar mbali sekta ya Utalii inayoingiza asilimia 30 ya pato la taifa lakini uvuvi na ufugaji wa vifaranga vya samaki ni sekta muhimu pia kwa uchumi wa nchi, hivyo alilitaka Shirikisho la wenye viwanda na wafanyabiashara kutoka China kuangalia fursa za uwekezaji kwenye eneo hilo.
Pia, Rais Dk. Mwinyi aliwaeleza wageni hao maumbile ya visiwa vya Zanzibar vina fursa adhimu ya bandari, hivyo aliikaribisha China kuitumia fursa hiyo kwa uwekezaji pamoja na kutuma na kupokea mizigo kwa pande mbili hizo za ushirikiano. Akiizungumzia sekta ya Mafuta na Gesi, Rais Dk. Mwinyi pia alilitaka Shirikisho hilo la Wenyeviwana na wafanyabiashara la China kuangalia pia eneo hilo kwa uwekezaji.
Naye, bw. Xu Lejiang, alimueleza Rais Dk. Mwinyi kwamba Shirikisho hilo la wenye viwanda na wafanyabiashara ni kubwa zaidi kwa China kwani limeyaweka pamoja zaidi ya makampuni makubwa na viwanda 700 wakiwemo wafanyabiashara wa madini, makampuni ya vifaa mbalimbali ikiwemo ujenzi na teknolojia, wafanyabiashara wakubwa na masuala ya kilimo kikubwa ambapo wengi wao wapo Zanzibar.
Kiongozi huyo alimuahidi Rais Dk. Mwinyi kuwashawishi wafanyabiashara wengi zaidi kuja kuwekeza Zanzibar huku ikiangaliwa Zanzibr na China inatimiza miaka 60 ya ushirikiano wao wa diplomasia pamoja na uhusiano wao wa kiuchumi, kisiasa na jamii.
DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AONGOZA KIKAO MAALUMU CHA KAMATI KUU YA CCM
09-12-2025
RAIS SAMIA AKIWAAPISHA MAWAZIRI NA MANAIBU WAZIRI WATEULE- IKULU CHAMWINO DODOMA
09-12-2025
WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU NCHEMBA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA DODOMA (GENERAL)
09-12-2025
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ..
09-12-2025
RAIS SAMIA AKIHUTUBIA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
09-12-2025
DKT SAMIA:TUNAFANYA UCHAGUZI KWA FEDHA ZETU WENYEWE
09-12-2025
MGOMBEA URAIS KUPITIA CCM DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA MANYARA
09-12-2025
π¨ππππ£πππππ πͺπ πππ§. π¦ππ ππ π¨π ππππ§π ππ ππ‘π ππͺπ πͺππ£ππ‘πππ‘π, πͺππππ¨ππππ πππ
πππ©πππͺ ππ πͺπͺ πΏπ π©. πππππ§π€ ππ¬ππ₯π€π ππ πππ€π£ππ€π―π π¬π πΎππΌπΏπππΌ π£π πΌπΎπ
09-12-2025
πππ§. π¦ππ ππ ππ§π¨π π‘πππ‘π π¬π ππ₯πππ π¬π ππππ’π π
09-12-2025
KATIBU MKUU WA CCM, BALOZI DKT. ASHA-ROSE MIGIRO AKUTANA NA RAIS MWINYI – ZANZIBAR
09-12-2025
ILANI YA UCHAGUZI YA CCM 2025-2030
09-12-2025
WASIRA:CCM HATUKATI MGOMBEA ILA TUNATEUA WACHACHE KATI YA WENGI
09-12-2025
WANACHAMA 280 WA CHADEMA WATIMKIA CCM
09-12-2025
BALOZI NCHIMBI: MAONI YOYOTE KUHUSU AMANI YA TANZANIA HAYATAPUUZWA
09-12-2025
π¦ππ₯πππππ π¬π π₯πππ¦ πππ§. π¦ππ ππ ππ ππͺπππ ππππ π π¬π π πππ‘πππππ’ ππππ π¦ππππ π¨ - ππ£π. ππ π’π¦ π ππππππ
09-12-2025
MAKALLA: BARABARA YA MPWAPWA NJIAPANDA KONGWA KUJENGWA LAMI
09-12-2025
BALOZI NCHIMBI AWASILI ARUSHA
09-12-2025
TAARIFA KWA UMMA
09-12-2025
UCHAGUZI MKUU SIO AJALI-WASIRA
09-12-2025
πͺπππ¨π ππ π π¦ππππππ¨π π©ππ’π‘ππ’ππ ππππππππ ππͺππ‘π¬π ππ¨π₯π ππ π ππ’π‘π - (π ππ) πππ©π¨
09-12-2025