RAIS WA ZANZIBAR MHE.DK.HUSSEIN MWINYI AZUNGUMZA NA BALOZI WA UJERUMANI NCHINI TANZANIA IKULU ZANZIBAR.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema sekta ya uwekezaji ni muhimu katika ustawi wa uchumi wa Zanzibar.
Dk. Mwinyi aliyasema hayo, Ikulu, Zanzibar alipozungumza na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Regine Hess aliefika kwa lengo la kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa utumishi hapa Tanzania. Alisema, Zanzibar bado ina fursa pana ya kuendelea kunufaika na uwekezaji kutoka Ujerumani kutokana na ushirikiano mwema ulipo baina yao.“Bado tuna fursa kubwa ya kuendelea kushirikiana na Ujerumani katika kukuza uwekezaji na kuongeza watalii wengi, Zanzibar. Tunashajihisha sana suala la uwekezaji sababu ndio kiungo kikubwa kwa uchumi wa Zanzibar” Alifafanua Dk. Mwinyi.Rais Dk. Mwinyi alieleza, Ujerumani imetoa mchango mkubwa kwa kuiinga mkono Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia sekta ya maji safi na salama ambayo aliieleza kuwa ni sekta muhimu kwa ustawi wa watu wa Zanzibar.
Pia Dk. Mwinyi aliishikuru Serikali ya Ujerumani kwa ushirikiano wanaendelea kuutoa kwa SMZ kupitia Sekta ya Afya na Michezo pamoja na kushajihisha watalii wengi raia wa Ujerumani wanaoingia Tanzania.Akizungumza kwenye hafla hiyo, Balozi Hess alimpongeza Rais Dk. Mwinyi kwa weledi wake wa kuridhia uongozi wake wa Serikali ya Umoja wa kitaifa pamoja na hatua alizozichukua za kuunda kamati ya maridhiano kitaifa kati ya Chama tawala CCM na cha upinzani ACT Wazalendo, akimsifu kwa jitihada zake za kuendelea kudumisha amani na utulivu wa kisiasa, Zanzibar.
Wakati huo huo, Balozi Hess alimtambulisha kwa Rais wa Zanzibar, Balozi wa heshima Dk. Jenny Bouraima atakaeiwakilisha Ujerumani na kufanya kazi zake hapa Zanzibar.Akizungumza mara bara baada ya utambulisho huo, Dk. Jenny ameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zaznzibar na kuahidi kushirikiana nayo bega kwa bega hasa kwenye suala zima la kuitangaza zaidi Zanzibar kupitia sekta ya utalii pamoja na kuiunga mkono sera ya Uchumi wa Buluu kwa kuwashajihisha zaidi Wajerumani kuja Zanzibar kuwekeza kupitia rasilimali bahari.
UZINDUZI WA JENGO LA MAKAO MAKUU YA ULINZI WA TAIFA
03-03-2026
CCM YAIPA POLE MSUMBIJI KWA KUKUMBWA NA MAFURIKO
03-03-2026
INJINI YA CHAMA CHA MAPINDUZI IPO MASHINANI; DKT.MIGIRO
03-03-2026
DK.MIGIRO:CCM INAJENGWA KUANZIA NGAZI YA MASHINA SIO MAJUKWAANI.
03-03-2026
πππ¦πππ‘ππ’ πππ πππ§. π ππππ₯π’ ππππ£π’πππππͺπ ππͺπ π¦πππ‘ππͺπ πππ₯ ππ¦ π¦πππππ
03-03-2026
NAIBU KATIBU MKUU WA CCM BARA AMWAKILISHA KATIBU MKUU WA CCM KWENYE MSIBA WA MBUNGE WA JIMBO LA PERAMIHO
03-03-2026
π©ππππ‘π π§π¨ππππ‘ππ ππ ππ‘π π¬π π‘πππ π¬ππ§π¨ - π πͺππ‘πππ πππ‘ππ‘π
03-03-2026
DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AONGOZA KIKAO MAALUMU CHA KAMATI KUU YA CCM
03-03-2026
RAIS SAMIA AKIWAAPISHA MAWAZIRI NA MANAIBU WAZIRI WATEULE- IKULU CHAMWINO DODOMA
03-03-2026
WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU NCHEMBA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA DODOMA (GENERAL)
03-03-2026
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ..
03-03-2026
RAIS SAMIA AKIHUTUBIA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
03-03-2026
DKT SAMIA:TUNAFANYA UCHAGUZI KWA FEDHA ZETU WENYEWE
03-03-2026
MGOMBEA URAIS KUPITIA CCM DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA MANYARA
03-03-2026
π¨ππππ£πππππ πͺπ πππ§. π¦ππ ππ π¨π ππππ§π ππ ππ‘π ππͺπ πͺππ£ππ‘πππ‘π, πͺππππ¨ππππ πππ
πππ©πππͺ ππ πͺπͺ πΏπ π©. πππππ§π€ ππ¬ππ₯π€π ππ πππ€π£ππ€π―π π¬π πΎππΌπΏπππΌ π£π πΌπΎπ
03-03-2026
πππ§. π¦ππ ππ ππ§π¨π π‘πππ‘π π¬π ππ₯πππ π¬π ππππ’π π
03-03-2026
KATIBU MKUU WA CCM, BALOZI DKT. ASHA-ROSE MIGIRO AKUTANA NA RAIS MWINYI – ZANZIBAR
03-03-2026
ILANI YA UCHAGUZI YA CCM 2025-2030
03-03-2026
WASIRA:CCM HATUKATI MGOMBEA ILA TUNATEUA WACHACHE KATI YA WENGI
03-03-2026
WANACHAMA 280 WA CHADEMA WATIMKIA CCM
03-03-2026