MAKAMU WA PILI WA RAIS ALHAJJ HEMED SULEIMAN ABDULLA AMEWATAKA WANANCHI KUZINGATIA MAELEKEZO YANAYOTOLEWA NA WATAALAMU WA HALI YA HEWA HASA KATIKA KIPINDI HICHI CHA MVUA ZA VULI ZINAZOENDELEA KUNYESHA NCHINI.
Alhajj Hemed ameyasema hayo alipokuwa akiwasalimia waumini wa Masjid LILLAH kianga Wilaya ya Magharibi "A" mara baada ya kumaliza Ibada ya sala ya Ijumaa.
Amesema imekuwa ni utamaduni wa wananchi wa Zanzibar kujisahau na kufanya shuhuli za ujenzi wakati wa jua kali sehemu ambazo sio sahihi kwa makaazi ya watu na kupelekea kuhangaika na familia wakati wa mvua kali zinaponyesha jambo ambalo huleta usumbufu mkubwa kwa baadhi ya wananchi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema ili kujinga na maafa hasa katika kipindi hiki cha Mvua zinazoendelea kunyesha ni vyema wananchi kuacha kujenga nyumba za makaazi sehemu ambazo sio salama pamoja na wale wanaoziba njia za maji jambo ambalo hupelekea athari kubwa kwa wananchi wakati wa mvua kubwa.
Alhajj Hemed ametoa pole kwa wale wote ambao wamepatwa na maafa kutokana na mvua kubwa iliyonyesha mwishoni mwa wiki iliyopita na kuwataka wananchi kuweza kusaidiana pale mmoja wao anapopatwa na tatizo la aina yoyote ikiwemo la maafa.
Aidha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema Serikali ya Awamu ya Nane (8) inayoongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dkt. Hussein Ali Mwinyi itahakikisha inatoa ushirikiano na msaada wa hali ya juu kwa mwananchi yeyote atakaepatwa na tatizo la aina yoyote ikiwemo la maafa.
Sambamba na hayo Alhajj Hemed amewasisistiza waumini wa Msikiti huo na wananchi kwa ujumla kuzidisha kudumisha amani, upendo na ushirikiano katika jamii ili nchi iweze kupata maendeleo.
Hata hivyo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amewaomba waumini kuendelea kuunga mkono juhudi zinazochukuliwa na Serekali za kuwaletea maendeleo wananchi wake kwani Serikali inajenga miradi mingi ya kimkakati ambayo itakuwa na tija kwa vizazi vya sasa na baadae.
Mapema akitoa Khutba katika Sala ya Ijumaa, Maalim Suleiman Hamad Suleiman amewataka waumini kushirikiana pamoja na kupeana elimu juu ya maisha ya ahera jambo ambalo wengi wao mamejisahau kuwa maisha ya dunia ni mapito tu.
Amesema ni wajibu wa waumini kumlingania mwenzake kwa kutumia lugha nzuri ili kuondosha mifarakano inayoweza kutokea pamoja na kuwataka waumini kutafuta chumo la halali katika kipato chao cha kila siku ili kujiwekea maisha yaliyobora mbele ya allah.
DKT SAMIA:TUNAFANYA UCHAGUZI KWA FEDHA ZETU WENYEWE
08-11-2025
MGOMBEA URAIS KUPITIA CCM DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA MANYARA
08-11-2025
π¨ππππ£πππππ πͺπ πππ§. π¦ππ ππ π¨π ππππ§π ππ ππ‘π ππͺπ πͺππ£ππ‘πππ‘π, πͺππππ¨ππππ πππ
πππ©πππͺ ππ πͺπͺ πΏπ π©. πππππ§π€ ππ¬ππ₯π€π ππ πππ€π£ππ€π―π π¬π πΎππΌπΏπππΌ π£π πΌπΎπ
08-11-2025
πππ§. π¦ππ ππ ππ§π¨π π‘πππ‘π π¬π ππ₯πππ π¬π ππππ’π π
08-11-2025
KATIBU MKUU WA CCM, BALOZI DKT. ASHA-ROSE MIGIRO AKUTANA NA RAIS MWINYI – ZANZIBAR
08-11-2025
ILANI YA UCHAGUZI YA CCM 2025-2030
08-11-2025
WASIRA:CCM HATUKATI MGOMBEA ILA TUNATEUA WACHACHE KATI YA WENGI
08-11-2025
WANACHAMA 280 WA CHADEMA WATIMKIA CCM
08-11-2025
BALOZI NCHIMBI: MAONI YOYOTE KUHUSU AMANI YA TANZANIA HAYATAPUUZWA
08-11-2025
π¦ππ₯πππππ π¬π π₯πππ¦ πππ§. π¦ππ ππ ππ ππͺπππ ππππ π π¬π π πππ‘πππππ’ ππππ π¦ππππ π¨ - ππ£π. ππ π’π¦ π ππππππ
08-11-2025
MAKALLA: BARABARA YA MPWAPWA NJIAPANDA KONGWA KUJENGWA LAMI
08-11-2025
BALOZI NCHIMBI AWASILI ARUSHA
08-11-2025
TAARIFA KWA UMMA
08-11-2025
UCHAGUZI MKUU SIO AJALI-WASIRA
08-11-2025
πͺπππ¨π ππ π π¦ππππππ¨π π©ππ’π‘ππ’ππ ππππππππ ππͺππ‘π¬π ππ¨π₯π ππ π ππ’π‘π - (π ππ) πππ©π¨
08-11-2025
MONGELLA AONGOZA MAZISHI YA KADA WA CCM JIJINI MWANZA
08-11-2025
ASIYETII SHERIA, KATIBA NA KUWA TAYARI KUUA KWA MASLAHI BINAFSI HUO NI UGAIDI’
08-11-2025
πππ π¬ππ¦ππ¦ππ§πππ πͺπππ’π πππ ππ¨πππππππͺπ ππͺπ ππ¨πππ‘πππ§ππ π¨πͺπππ’, π¨πππππ‘ππ’ π‘π π¨πππππππ¨, π¬ππππ ππ π πππ¨π‘ππ - πππ. πππ©π¨
08-11-2025
KAENI KIMYA KAMA HAMJUI NCHI ILIKOTOKA - WASIRA
08-11-2025
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefungua kiwanda cha kutengeneza mabomba ya maji na uchakataji pamba cha MOLI Oil Mills Co. Ltd kilichopo Bariadi Mkoani Simiyu tarehe 16 Juni, 2025.
08-11-2025