BALOZI DKT. NCHIMBI AHIMIZA JUU YA UTUNZAJI WA MIRADI YA UMMA, ASISITIZA KUJIBU UONGO KWA HOJA NA SI MATUSI.
> Asisitiza tabia ya Uadilifu kwa kila mtanzania.
"Tutunze, tuvienzi na tusikie uchungu kwa mali za umma, kama hatujali miradi yetu basi kunakuwa hakuna maana hata tunayemsifia usiku na mchana kwa kazi kubwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, tutamfedhehesha bure kama hatulindi na kuitunza miradi yetu ya maendeleo kwenye maeneo yenu"
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akizungumza na Mabalozi wa Mashina, Viongozi mbalimbali wa serikali, Taasisi zisizo za kiserikali, Wazee na viongozi wa dini wakati wa mkutano wa uwasilishaji wa taarifa ya utekelezaji wa ilani ya CCM ya mwaka 2020/25 kwa kipindi cha mwaka 2021 - 2023.
Balozi Dkt. Nchimbi amesema kila mtanzania yampasa kuwa na uzalendo wa kulipenda taifa lake na kuwa na uadilifu na kuwaomba viongozi wa dini na wazazi kusimamia hilo.
" Lazima tabia ya kuipenda Nchi na uadilifu tuendelee kuisimamia bila kuona haya, viongozi wa dini , kimila na wazazi muendelee kusisitiza kwa watoto wetu juu ya uadilifu ndani ya nyumba na nje ya nyumba zetu "
" Zamani wakati tunasoma ilikuwa ukiwa mda wa shule haupo shuleni basi mzazi wa mtu mwingine au wale mabwana huruma wanakurudisha uende shule kupata elimu na ndivyo inavyotakiwa lakini kwasasa ukimwambia mtoto wa mtu rudi shuleni cha ajabu mzazi wake atakwambia anakuhusu nini kwani mtoto wako ?...sasa kama mtoto hatuhusu kisa wako mbona ukimua lazima ushtakiwe...kama angekuwa ni mali yako pekee basi usingeshtakiwa hivyo ni lazima kila mmoja kuwa na uadilifu na kuona uchungu wa kulijenga taifa letu "
" Tujielekeze kwenye malezi kwa watoto wetu kuhakikisha tunapata vizazi vya kesho vyenye maana kwa Taifa letu "
Pia Dkt. Nchimbi amesisitiza juu ya kujibu uongo kwa hoja na si matusi,
"Kuna watu watazunguka huko na kusema CCM haijafanya lolote wakati mambo yamefanyika na yapo waziwazi"
"Kawaida ya uongo upo kila sehemu na uongo hutafutwa na ukweli, uongo upo kwenye vikao vya CCM, kwa CHADEMA, kwa CUF kwenye mahusiano na hata familia zetu lakini niwaambie ni wajibu wa kila mwana CCM kuwakumbusha watu kila anapotokea mtu na kuaema CCM haijafanya kazi na msimuache mtu huyo apate nafasi"
"Hata wakianzisha maandamano waambieni hao ndio waongo na mseme kazi kubwa zinazofanyika na uongo ukataliwe kwa hoja na si matusi"
"Tukifanya hivi mwisho wa siku watu wataendelea kuelewa na kutambua ukweli wa kazi nzuri anayoendelea kuifanya Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuijenga na kuiletea maendeleo Nchi yetu"
"Tutaisimamia haki kwa nguvu zote, tutahakikisha Rais Samia Suluhu Hassan, haangushwi wala hayumbishwi na watendaji wetu wavivu na wazembe , tutaisimamia serikali ipasavyo"
ποΈ19 Aprili, 2024
πNjombe
DKT SAMIA:TUNAFANYA UCHAGUZI KWA FEDHA ZETU WENYEWE
05-11-2025
MGOMBEA URAIS KUPITIA CCM DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA MANYARA
05-11-2025
π¨ππππ£πππππ πͺπ πππ§. π¦ππ ππ π¨π ππππ§π ππ ππ‘π ππͺπ πͺππ£ππ‘πππ‘π, πͺππππ¨ππππ πππ
πππ©πππͺ ππ πͺπͺ πΏπ π©. πππππ§π€ ππ¬ππ₯π€π ππ πππ€π£ππ€π―π π¬π πΎππΌπΏπππΌ π£π πΌπΎπ
05-11-2025
πππ§. π¦ππ ππ ππ§π¨π π‘πππ‘π π¬π ππ₯πππ π¬π ππππ’π π
05-11-2025
KATIBU MKUU WA CCM, BALOZI DKT. ASHA-ROSE MIGIRO AKUTANA NA RAIS MWINYI – ZANZIBAR
05-11-2025
ILANI YA UCHAGUZI YA CCM 2025-2030
05-11-2025
WASIRA:CCM HATUKATI MGOMBEA ILA TUNATEUA WACHACHE KATI YA WENGI
05-11-2025
WANACHAMA 280 WA CHADEMA WATIMKIA CCM
05-11-2025
BALOZI NCHIMBI: MAONI YOYOTE KUHUSU AMANI YA TANZANIA HAYATAPUUZWA
05-11-2025
π¦ππ₯πππππ π¬π π₯πππ¦ πππ§. π¦ππ ππ ππ ππͺπππ ππππ π π¬π π πππ‘πππππ’ ππππ π¦ππππ π¨ - ππ£π. ππ π’π¦ π ππππππ
05-11-2025
MAKALLA: BARABARA YA MPWAPWA NJIAPANDA KONGWA KUJENGWA LAMI
05-11-2025
BALOZI NCHIMBI AWASILI ARUSHA
05-11-2025
TAARIFA KWA UMMA
05-11-2025
UCHAGUZI MKUU SIO AJALI-WASIRA
05-11-2025
πͺπππ¨π ππ π π¦ππππππ¨π π©ππ’π‘ππ’ππ ππππππππ ππͺππ‘π¬π ππ¨π₯π ππ π ππ’π‘π - (π ππ) πππ©π¨
05-11-2025
MONGELLA AONGOZA MAZISHI YA KADA WA CCM JIJINI MWANZA
05-11-2025
ASIYETII SHERIA, KATIBA NA KUWA TAYARI KUUA KWA MASLAHI BINAFSI HUO NI UGAIDI’
05-11-2025
πππ π¬ππ¦ππ¦ππ§πππ πͺπππ’π πππ ππ¨πππππππͺπ ππͺπ ππ¨πππ‘πππ§ππ π¨πͺπππ’, π¨πππππ‘ππ’ π‘π π¨πππππππ¨, π¬ππππ ππ π πππ¨π‘ππ - πππ. πππ©π¨
05-11-2025
KAENI KIMYA KAMA HAMJUI NCHI ILIKOTOKA - WASIRA
05-11-2025
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefungua kiwanda cha kutengeneza mabomba ya maji na uchakataji pamba cha MOLI Oil Mills Co. Ltd kilichopo Bariadi Mkoani Simiyu tarehe 16 Juni, 2025.
05-11-2025