NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt.Mohamed Said Dimwa,amesema Chama Cha Mapinduzi hakitofanya upendeleo wa kutoa nafasi za kugombea uongozi kwa kigezo cha fedha na utajiri bali kitaweka mbele maslahi ya wanachama wote bila kujali hali zao za maisha.
Kauli hiyo ametoa wakati akiwahutubia viongozi na wanachama wa CCM katika Mkutano Mkuu Maalum wa Jimbo la Pangawe huko Wilaya ya Dimani Kichama Unguja.
Dkt.Dimwa,alisema kila mwanachama ana haki ya kuchagua na kuchaguliwa hivyo ni lazima waondoshe dhana iliyojengeka siku za hivi karibuni kuwa wenye haki ya kugombea na kupata nafasi za uongozi ni watu wenye fedha na matajiri wakati Chama hicho kimetokana na wakwezi,wakulima na wafanyakazi.
Katika maelezo yake Naibu Katibu Mkuu huyo Dkt.Dimwa,alisema CCM itaendelea kusimamia kikamilifu misingi ya usawa,haki,uhuru na demokrasia pana ndani na nje ya Chama ili kutoa nafasi ya wanachama kunufaika na fursa mbalimbali zinazipatikana ndani ya Chama hicho.
“Wapo baadhi ya watu kila ikikaribia wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Dola wanawahadaa kwa fedha na vitu vya thamani wanachama wetu ili wawachague na wakisha pata uongozi wanapandisha mabega na wanajisifu kuwa tulipata Ubunge,Uwakilishi na Udiwani kwa sababu ya fedha zetu hivyo mtuache turejeshe fedha zetu kwanza maendeleo baadae.
Awamu hii watu wa aina hiyo mkiwaleta basi mjue hawatovuka kwani kigezo chetu ni kuangalia sifa za msingi za mgombea na tukiridhika naye hata akiwa mnyonge na maskini huyo huyo ndo tutaenda naye.”,alisema na kuongeza kuwa CCM sio mali ya matajiri bali ipo kwa manufaa ya wananchi wote.
Kupitia hotuba yake Naibu Katibu huyo,aliwapongeza Mwakilishi,Mbunge na Madiwani wa Jimbo la Pangawe kwa kazi nzuri wanayofanya ya kushirikiana katika kutatua changamoto za wananchi wa jimbo hilo ikiwemo zoezi la kutoa sadaka ya futari kwa wananchi wenye mahitaji ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya CCM.
Pamoja na hayo amewapongeza waumini wa dini ya kikiristo kwa kuathimisha siku kuu ya Pasaka pamoja kuwasihi waumini wa dini ya kiislamu kuendelea kufanya ibada kwa wingi,kujikataza na maasi na kutoa sadaka ili funga zao katika mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani zikubaliwe na Mwenyezi Mungu.
Aliwasihi wanachama hao kuendelea kuthamini na kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais wa Zanzibar Dk.Hussein Mwinyi kwa kutekeleza llani ya CCM ya mwaka 2020/2025 kwa ufanisi mkubwa.
Naibu Katibu mkuu huyo Dkt.Dimwa, alizindua rasmi zoezi la ugawaji wa vitambulisho vya kisasa kwa Mabalozi wa mashina wa CCM pamoja na kuwapatia posho la shilingi 20,000 ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Hussein Mwinyi litakalofanyika katika majimbo yote ya Zanzibar.
Pia Dkt.Dimwa, aligawa sadaka ya futari kwa niaba ya uongozi wa jimbo zikiwemo sukari,mchele,mafuta ya kula na unga wa ngano kwa makundi mbalimbali ya Watu wenye mahitaji Maalum,Wazee,Wajane,Masheha na Mabalozi wa Jimbo la hilo.
Akizungumza Mwakilishi wa Jimbo la Pangawe Ali Suleiman Mrembo,amesema lengo la Mkutano huo Maalum wa Jimbo ni viongozi hao kurejesha shukrani kwa wanachama wa CCM wa ngazi mbalimbali kutokana na kazi nzuri waliyofanya ya kuvuka malengo katika awamu ya kwanza ya zoezi la uhakiki wa Daftari la kudumu la uandikishaji wa wapiga kura.
Naye Mbunge wa Jimbo la Pangawe Haji Amour Haji,amesema mafanikio yaliyofikiwa ndani ya jimbo hilo yametokana na dhamira ya dhati ya viongozi hao ya kuleta maendeleo kwa kila mwananchi inayochechewa na ushirikiano kutoka kwa Wanaccm na wananchi wenyewe.
𝐊𝐈𝐇𝐎𝐍𝐆𝐎𝐒𝐈 𝐀𝐊𝐔𝐓𝐀𝐍𝐀 𝐍𝐀 𝐖𝐀𝐍𝐀𝐍𝐂𝐇𝐈 𝐇𝐀𝐍𝐀𝐍𝐆, 𝐀𝐒𝐈𝐊𝐈𝐋𝐈𝐙𝐀 𝐍𝐀 𝐊𝐔𝐓𝐀𝐓𝐔𝐀 𝐊𝐄𝐑𝐎 𝐙𝐀𝐎
02-06-2026
𝐌𝐖𝐄𝐍𝐄𝐙𝐈 𝐀𝐏𝐎𝐊𝐄𝐋𝐄𝐖𝐀 𝐇𝐀𝐍𝐀𝐍𝐆’-𝐌𝐀𝐍𝐘𝐀𝐑𝐀
02-06-2026
𝐍𝐈 𝐍𝐙𝐀𝐌𝐔 𝐘𝐀 𝐌𝐊𝐎𝐀 𝐖𝐀 𝐌𝐀𝐍𝐘𝐀𝐑𝐀!
02-06-2026
🔰𝐀𝐒𝐀𝐍𝐓𝐄𝐍𝐈 𝐒𝐀𝐍𝐀 𝐖𝐀𝐍𝐀𝐍𝐂𝐇𝐈 𝐖𝐀 𝐊𝐈𝐋𝐈𝐌𝐀𝐍𝐉𝐀𝐑𝐎!
02-06-2026
𝐒𝐇𝐔𝐋𝐄 𝐘𝐀 𝐌𝐒𝐈𝐍𝐆𝐈 𝐊𝐖𝐀 𝐒𝐀𝐃𝐀𝐋𝐀 𝐘𝐀𝐎𝐍𝐃𝐎𝐀 𝐊𝐄𝐑𝐎 𝐘𝐀 𝐊𝐔𝐓𝐄𝐌𝐁𝐄𝐀 𝐊𝐈𝐋𝐎𝐌𝐄𝐓𝐀 𝟏𝟐 𝐊𝐖𝐀 𝐖𝐀𝐍𝐀𝐅𝐔𝐍𝐙𝐈
02-06-2026
𝐌𝐖𝐄𝐍𝐄𝐙𝐈 𝐖𝐀 𝐂𝐂𝐌 𝐓𝐀𝐈𝐅𝐀 𝐀𝐀𝐍𝐙𝐀 𝐙𝐈𝐀𝐑𝐀 𝐖𝐈𝐋𝐀𝐘𝐀𝐍𝐈 𝐇𝐀𝐈, 𝐊𝐈𝐋𝐈𝐌𝐀𝐍𝐉𝐀𝐑𝐎
02-06-2026
𝐌𝐖𝐄𝐍𝐄𝐙𝐈 𝐖𝐀 𝐂𝐂𝐌 𝐓𝐀𝐈𝐅𝐀 𝐀𝐀𝐍𝐙𝐀 𝐙𝐈𝐀𝐑𝐀 𝐖𝐈𝐋𝐀𝐘𝐀 𝐘𝐀 𝐇𝐀𝐈 𝐌𝐊𝐎𝐀 𝐖𝐀 𝐊𝐈𝐋𝐈𝐌𝐀𝐍𝐉𝐀𝐑𝐎
02-06-2026
𝐍𝐈 𝐌𝐔𝐃𝐀 𝐖𝐀 𝐖𝐀𝐍𝐀𝐇𝐀𝐈-𝐊𝐈𝐋𝐈𝐌𝐀𝐍𝐉𝐀𝐑𝐎 𝐒𝐀𝐒𝐀
02-06-2026
𝐑𝐀𝐈𝐒 𝐒𝐀𝐌𝐈𝐀 𝐀𝐌𝐏𝐀 𝐁𝐀𝐉𝐀𝐉𝐈 𝐌𝐊𝐀𝐙𝐈 𝐖𝐀 𝐒𝐈𝐇𝐀 𝐌𝐖𝐄𝐍𝐘𝐄 𝐔𝐋𝐄𝐌𝐀𝐕𝐔 𝐖𝐀 𝐌𝐈𝐆𝐔𝐔
02-06-2026
MAWENZI YAVUNJA REKODI: MITUNGI 3,313 YA OKSIJENI YAZALISHWA KWA MIEZI 6, ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 126 ZAOKOLEWA!
02-06-2026
MAFURIKO YA WANANCHI WA SIHA KWENYE MKUTANO MKUBWA WA HADHARA
02-06-2026
MAPOKEZI YA KATIBU MWENEZI WA CCM NDUGU KENANI L KIHONGOSI MKOANI KILIMANJARO
02-06-2026
🔰 𝐊𝐈𝐇𝐎𝐍𝐆𝐎𝐒𝐈 𝐀𝐖𝐀𝐒𝐈𝐋𝐈 𝐊𝐖𝐀 𝐊𝐈𝐒𝐇𝐈𝐍𝐃𝐎 𝐊𝐈𝐋𝐈𝐌𝐀𝐍𝐉𝐀𝐑𝐎
02-06-2026
CCM INAWATAKIA HERI YA SIKUKUU YA EID AL ADHA
02-06-2026
🔰VYAMA VYA UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA VYAIMARISHA MSHIKAMANO, DKT. DIMWA AHITIMISHA MAFUNZO MAALUM
02-06-2026
KATIBU WA NEC, ITIKADI, UENEZI NA MAFUNZO CCM TAIFA NDUGU KENANI KIHONGOSI AMNADI MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA ISIMANI EMMANUELA KAGANDA MTATIFIKOLO
02-06-2026
MUENDELEZO WA MAFUNZO YA VIONGOZI KATIKA SHULE YA UONGOZI YA MWALIMU JULIUS NYERERE – KIBAHA
02-06-2026
SIKU YA KWANZA YA MAFUNZO KATIKA SHULE YA UONGOZI YA MWALIMU JULIUS NYERERE LEADERSHIP SCHOOL.
02-06-2026
UFUNGUZI WA MAFUNZO YA VYAMA SITA RAFIKI VYA UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA
02-06-2026
MHE. DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA MJUMBE WA KAMATI KUU YA CPC, KOMREDI LIU HAIXING IKULU DAR ES SALAAM
02-06-2026