Wazazi na walezi wametakiwa kuwasimamia watoto wao katika suala zima la kufanya Ibada hasa katika mwezi wa Ramadhan ambao ni mwezi wenye fadhila nyingi ambao humtakasa mja kutokana na maovu na machafu.
Hayo yamesemwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla wakati akiwasalimia waumini wa Masjid SHEYKHAT NAIMA uliopo TOMONDO MADUKA saba(7) mara baada ya kumaliza Ibada ya Sala ya Ijumaa.
Amesema kuwa kuwasimamia vyema vijana katika kufanya Ibada na kuwapa elimu juu ya kuijua dini yao pamoja na nchi yao kutapelekea Taifa kupata viongozi bora na wenye kufanya kazi kwa maslahi ya nchi na Taifa kwa ujumla.
Alhajj Hemed amesisitiza kuwa zimebaki siku chache kuingia kwa mwezi mtukufu wa ramadhani hivyo ni vyema waislamu kuongeza bidii katika kuwahimiza vinjana wao kufanya ibada ikiwemo visimamo vya usiku, kuhudhuria madrasa na kupendana baina yao ambako kutapelekea kupata wanazuoni walio bora na wenye kuijua dini yao.
Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar amesema katika mwezi wa Ramadhani waumini wanapaswa kuzidisha upendo na mshikamano baina yao sambamba na kutoa sadaka kwa kuwasaidia watu wasio na uwezo ili kupata fadhila za mwezi mtukufu wa ramadhani.
Sambamba na hayo Alhajj Hemed amewataka wananchi wa Zanzibar kuendelea kudumisha mila, silka na desturi zilizopo nchini hasa katika kipindi cha mwezi mtukufu wa ramadhania kwa kuacha kuvaa nguo zisizofaa ambazo zitawapelekea waumini wa dini ya kiisalumu kutokufikia lego la kufunga.
Mapema akitoa Khutba katika Sala ya Ijumaa, Ustadh. KASSIM HAMAD amewaasa waumini wa Dini ya Kiislam kuacha tabia ya kuingila Mamlaka ya Taasisi za Kiserikali hasa Taasisi iliyopewa dhamana ya kutangaza kuandama kwa mwezi hususan Mwezi mtukuru wa ramadhan kwani kufanya hivyo ni kwenda kinyume na sheria za nchi na za dini ya Kiislamu.
Amesema kuwa kumekuwa na tabia kwa baadhi ya waislamu kufarakana na kutosaidiana kutokana na tofauti zao za kimadhehebi katika kufuata muandamo wa mwezi hivyo amewasisitiza waislamu kujiepusha kabisa na matendo hayo kwani kufanya hivyo ni kwenda kinyume na maamrisho ya Allah (S.W) na kutapelekea kutokufikia lengo la kufunga.
NAIBU KATIBU MKUU WA CCM BARA AMWAKILISHA KATIBU MKUU WA CCM KWENYE MSIBA WA MBUNGE WA JIMBO LA PERAMIHO
07-01-2026
π©ππππ‘π π§π¨ππππ‘ππ ππ ππ‘π π¬π π‘πππ π¬ππ§π¨ - π πͺππ‘πππ πππ‘ππ‘π
07-01-2026
DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AONGOZA KIKAO MAALUMU CHA KAMATI KUU YA CCM
07-01-2026
RAIS SAMIA AKIWAAPISHA MAWAZIRI NA MANAIBU WAZIRI WATEULE- IKULU CHAMWINO DODOMA
07-01-2026
WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU NCHEMBA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA DODOMA (GENERAL)
07-01-2026
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ..
07-01-2026
RAIS SAMIA AKIHUTUBIA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
07-01-2026
DKT SAMIA:TUNAFANYA UCHAGUZI KWA FEDHA ZETU WENYEWE
07-01-2026
MGOMBEA URAIS KUPITIA CCM DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA MANYARA
07-01-2026
π¨ππππ£πππππ πͺπ πππ§. π¦ππ ππ π¨π ππππ§π ππ ππ‘π ππͺπ πͺππ£ππ‘πππ‘π, πͺππππ¨ππππ πππ
πππ©πππͺ ππ πͺπͺ πΏπ π©. πππππ§π€ ππ¬ππ₯π€π ππ πππ€π£ππ€π―π π¬π πΎππΌπΏπππΌ π£π πΌπΎπ
07-01-2026
πππ§. π¦ππ ππ ππ§π¨π π‘πππ‘π π¬π ππ₯πππ π¬π ππππ’π π
07-01-2026
KATIBU MKUU WA CCM, BALOZI DKT. ASHA-ROSE MIGIRO AKUTANA NA RAIS MWINYI – ZANZIBAR
07-01-2026
ILANI YA UCHAGUZI YA CCM 2025-2030
07-01-2026
WASIRA:CCM HATUKATI MGOMBEA ILA TUNATEUA WACHACHE KATI YA WENGI
07-01-2026
WANACHAMA 280 WA CHADEMA WATIMKIA CCM
07-01-2026
BALOZI NCHIMBI: MAONI YOYOTE KUHUSU AMANI YA TANZANIA HAYATAPUUZWA
07-01-2026
π¦ππ₯πππππ π¬π π₯πππ¦ πππ§. π¦ππ ππ ππ ππͺπππ ππππ π π¬π π πππ‘πππππ’ ππππ π¦ππππ π¨ - ππ£π. ππ π’π¦ π ππππππ
07-01-2026
MAKALLA: BARABARA YA MPWAPWA NJIAPANDA KONGWA KUJENGWA LAMI
07-01-2026
BALOZI NCHIMBI AWASILI ARUSHA
07-01-2026
TAARIFA KWA UMMA
07-01-2026