CCM HAITAKI UONGOZI WA KUGAWANYA WATU KWAKUWA UNAPELEKEA MPASUKO WA NDANI YA CHAMA NA KUKWAMISHA MAENDELEO KWA WANANCHI - BALOZI DKT. NCHIMBI
"Chama Cha Mapinduzi hakitaki na kinakemea tabia ya Uongozi wa kugwanya watu kwakuwa unapelekea mpasuko ndani ya Chama na kukwamisha maendeleo kwa Watanzana." hiyo ni kauli ya Katibu Mkuu Dkt. Nchimbi wakati akizungumza na Viongozi mbalimbali wa CCM kuanzia Mashina hadi Mkoa, Viongozi wa Serikali, Taasisi zisizo za kiserikali, Viongozi wa dini na Wazee.
Katibu Mkuu Dkt. Nchimbi amesema Chama chochote cha siasa lazima kiwe na chaguzi za kweli na hizo zinatokana na uwepo wa Haki ambayo ndiyo yenye kupelekea ushindani wa kweli.
Balozi Dkt. Nchimbi amebainisha kuwa moja ya changamoto kubwa iliyopo ndani ya CCM ni tabia ya baadhi ya viongozi wanaoshindwa na wanaoshinda kutokukubali matokeo miyoyoni mwao na matokeo yake pamoja na uchache wao lakini wanakuwa na madhara makubwa na kusema tabia hiyo iachwe mara moja kwakuwa ni ujinga na sio misingi ya demokrasia.
" Unakuta mtu kagombea na kashida lakini akimaliza kushinda anaanza kutafuta nani hakumuunga mkono ili apambane nae na kumkandamiza, hiyo ni tabia ya kijinga na haiungwi mkono, tuache mara moja " Alisema Balozi Dkt. Nchimbi
Pia, Balozi Dkt. Nchimbi ameendelea kuhimiza juu ya misingi ya haki na wajibu na kusema mti yeyote anapoingia kwenye uchaguzi anatakiwa kufahamu kila mtu ana haki sawa na mwengine hivyo ni lazia uwe na dhamira ya utumishi na wakati mwingine usipochaguliwa unatakiwa kuhisi kwamba mzigo mkubwa umekuepukia.
"Vyama vidogo vinapokataa matokeo ni wanaiiga CCM kwa kuona baadhi wa wagombea ndani ya CCM wanavyopinga matokeo ya ndani, tuache tabia hiyo mara moja"
"Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere aliwahi kusema 'Mimi nanga'atuka lakini naendelea kuamini kuwa bila CCM madhubuti nchi hii itayumba' Hivyo niwaambie ndugu zangu mtu asiyeitakia mema nchi hii atatamani kuona CCM inapasuka."
"...Tujue kwamba CCM madhubuti inaongozwa na misingi ya demokrasia na kiongozi wa kweli ni yule ambaye anakubali matokeo bila vita, mimi nilishawahi kugombeaga mara 28 na mara 4 nilishindwa lakini naelewa kuna kushinda na kushindwa na matokeo nikakubali."
"Wana CCM nchi nzima tueshimu utaratibu wa kidemorsia ndan ya CCM, tufanye chaguzi kwa haki na tukubali matokeo, kiongozi wa kweli ni mnyenyekevu na habagui, waonganishe watu wote kwa usawa sio utume vikosi vya upererezi."
🗓️ 13 Aprili, 2024
📍 Mpanda - Katavi
🔰 𝐀𝐆𝐎𝐒𝐓𝐈 𝐘𝐀 𝐌𝐀𝐅𝐔𝐍𝐙𝐎, 𝐔𝐉𝐄𝐍𝐙𝐈 𝐖𝐀 𝐂𝐇𝐀𝐌𝐀 𝐍𝐀 𝐔𝐎𝐍𝐆𝐄𝐙𝐀𝐉𝐈 𝐖𝐀 𝐖𝐀𝐍𝐀𝐂𝐇𝐀𝐌𝐀!
01-08-2026
𝐑𝐀𝐈𝐒 𝐒𝐀𝐌𝐈𝐀: 𝐌𝐀𝐑𝐈𝐃𝐇𝐈𝐀𝐍𝐎 𝐍𝐈 𝐌𝐒𝐈𝐍𝐆𝐈 𝐖𝐀 𝐌𝐀𝐁𝐎𝐑𝐄𝐒𝐇𝐎 𝐘𝐀 𝐊𝐀𝐓𝐈𝐁𝐀
01-08-2026
𝐑𝐀𝐈𝐒 𝐒𝐀𝐌𝐈𝐀 𝐀𝐒𝐇𝐈𝐑𝐈𝐊𝐈 𝐌𝐀𝐀𝐃𝐇𝐈𝐌𝐈𝐒𝐇𝐎 𝐘𝐀 𝐒𝐈𝐊𝐔 𝐘𝐀 𝐌𝐀𝐒𝐇𝐔𝐉𝐀𝐀 𝐃𝐎𝐃𝐎𝐌𝐀
01-08-2026
𝐂𝐂𝐌 𝐘𝐀𝐓𝐇𝐈𝐁𝐈𝐓𝐈𝐒𝐇𝐀 𝐌𝐒𝐈𝐍𝐆𝐈 𝐖𝐀 𝐊𝐔𝐇𝐔𝐃𝐔𝐌𝐈𝐀 𝐖𝐀𝐍𝐀𝐍𝐂𝐇𝐈 𝐊𝐖𝐀 𝐕𝐘𝐀𝐌𝐀 𝐓𝐀𝐖𝐀𝐋𝐀 𝐀𝐅𝐑𝐈𝐊𝐀
01-08-2026
𝐒𝐀𝐌𝐈𝐀 𝐀𝐍𝐀𝐈𝐅𝐔𝐍𝐆𝐔𝐀 𝐄𝐍𝐙𝐈 𝐌𝐏𝐘𝐀 𝐊𝐈𝐆𝐎𝐌𝐀!
01-08-2026
🚆 𝐓𝐔𝐊𝐔𝐓𝐀𝐍𝐄 𝐊𝐈𝐆𝐎𝐌𝐀!
01-08-2026
ZIARA YA RAIS WA MISRI-TANZANIA
01-08-2026
🔰 CCM NA ACT-WAZALENDO WASAINI MARIDHIANO YA PAMOJA YA KISIASA ZANZIBAR
01-08-2026
🎉 𝐇𝐄𝐑𝐈 𝐘𝐀 𝐒𝐈𝐊𝐔 𝐘𝐀 𝐊𝐔𝐙𝐀𝐋𝐈𝐖𝐀, 𝐃𝐊𝐓. 𝐀𝐒𝐇𝐀-𝐑𝐎𝐒𝐄 𝐌𝐈𝐆𝐈𝐑𝐎! 🔰
01-08-2026
🔰𝐍𝐀𝐈𝐁𝐔 𝐊𝐀𝐓𝐈𝐁𝐔 𝐌𝐊𝐔𝐔 𝐖𝐀 𝐂𝐂𝐌 𝐁𝐀𝐑𝐀 𝐀𝐒𝐇𝐈𝐑𝐈𝐊𝐈 𝐊𝐈𝐊𝐀𝐎 𝐂𝐇𝐀 𝐇𝐀𝐋𝐌𝐀𝐒𝐇𝐀𝐔𝐑𝐈 𝐊𝐔𝐔 𝐘𝐀 𝐂𝐂𝐌 𝐌𝐊𝐎𝐀 𝐖𝐀 𝐌𝐖𝐀𝐍𝐙𝐀
01-08-2026
🔰𝐇𝐄𝐑𝐈 𝐘𝐀 𝐌𝐀𝐀𝐃𝐇𝐈𝐌𝐈𝐒𝐇𝐎 𝐘𝐀 𝐒𝐀𝐁𝐀 𝐒𝐀𝐁𝐀 𝟐𝟎𝟐𝟔!
01-08-2026
𝐒𝐀𝐒𝐀 𝐍𝐈 𝐙𝐀𝐌𝐔 𝐘𝐀 𝐏𝐖𝐀𝐍𝐈; 𝐀𝐑𝐃𝐇𝐈 𝐘𝐀 𝐇𝐈𝐒𝐓𝐎𝐑𝐈𝐀, 𝐌𝐖𝐄𝐍𝐄𝐙𝐈 𝐀𝐍𝐀𝐊𝐔𝐉𝐀!!!!!
01-08-2026
𝐈𝐑𝐈𝐍𝐆𝐀 𝐌𝐉𝐈𝐍𝐈 𝐘𝐀𝐌𝐏𝐀 𝐊𝐄𝐍𝐀𝐍𝐈 𝐌𝐀𝐏𝐎𝐊𝐄𝐙𝐈 𝐘𝐀 𝐊𝐈𝐇𝐈𝐒𝐓𝐎𝐑𝐈𝐀
01-08-2026
𝐌𝐖𝐄𝐍𝐄𝐙𝐈 𝐊𝐄𝐍𝐀𝐍𝐈 𝐀𝐙𝐈𝐍𝐃𝐔𝐀 𝐒𝐇𝐈𝐍𝐀 𝐋𝐀 𝐖𝐀𝐊𝐄𝐑𝐄𝐊𝐄𝐓𝐖𝐀 𝐌𝐋𝐀𝐍𝐃𝐄𝐆𝐄, 𝐊𝐈𝐋𝐎𝐒𝐀-𝐈𝐑𝐈𝐍𝐆𝐀
01-08-2026
𝐌𝐖𝐄𝐍𝐄𝐙𝐈 𝐊𝐄𝐍𝐀𝐍𝐈 𝐀𝐓𝐄𝐌𝐁𝐄𝐋𝐄𝐀 𝐒𝐇𝐈𝐍𝐀 𝐍𝐀. 𝟏𝟎 𝐌𝐀𝐅𝐈𝐅𝐈, 𝐀𝐒𝐈𝐒𝐈𝐓𝐈𝐙𝐀 𝐀𝐌𝐀𝐍𝐈, 𝐔𝐌𝐎𝐉𝐀 𝐍𝐀 𝐌𝐒𝐇𝐈𝐊𝐀𝐌𝐀𝐍𝐎
01-08-2026
𝐌𝐑𝐀𝐃𝐈 𝐖𝐀 𝐌𝐀𝐅𝐔𝐍𝐙𝐎 𝐘𝐀 𝐔𝐅𝐔𝐍𝐃𝐈 𝐊𝐈𝐋𝐎𝐋𝐎 𝐊𝐔𝐅𝐔𝐍𝐆𝐔𝐀 𝐅𝐔𝐑𝐒𝐀 𝐙𝐀 𝐀𝐉𝐈𝐑𝐀 𝐊𝐖𝐀 𝐕𝐈𝐉𝐀𝐍𝐀
01-08-2026
𝐊𝐈𝐋𝐎𝐋𝐎, 𝐙𝐀𝐌𝐔 𝐘𝐄𝐍𝐔 𝐍𝐈 𝐋𝐄𝐎!
01-08-2026
𝐑𝐀𝐁𝐈𝐀: 𝐃𝐊𝐓. 𝐒𝐀𝐌𝐈𝐀 𝐒𝐔𝐋𝐔𝐇𝐔 𝐇𝐀𝐒𝐒𝐀𝐍 𝐍𝐈 𝐌𝐓𝐄𝐊𝐄𝐋𝐄𝐙𝐀𝐉𝐈 𝐌𝐀𝐇𝐈𝐑𝐈 𝐖𝐀 𝐀𝐇𝐀𝐃𝐈 𝐙𝐀 𝐂𝐂𝐌
01-08-2026
𝐒𝐈𝐌𝐔 𝐈𝐌𝐄𝐈𝐓𝐀, 𝐍𝐄𝐄𝐌𝐀 𝐘𝐀 𝐔𝐓𝐀𝐓𝐔𝐙𝐈 𝐊𝐈𝐋𝐎𝐋𝐎!
01-08-2026
𝐑𝐔𝐀𝐇𝐀 𝐌𝐁𝐔𝐘𝐔𝐍𝐈 𝐘𝐀𝐅𝐔𝐑𝐈𝐊𝐀; “𝐂𝐇𝐈𝐄𝐅 𝐂𝐇𝐎𝐆𝐀𝐕𝐀𝐓𝐀𝐌𝐁𝐔𝐋𝐄” 𝐀𝐊𝐈𝐓𝐄𝐊𝐀 𝐌𝐊𝐔𝐓𝐀𝐍𝐎 𝐖𝐀 𝐇𝐀𝐃𝐇𝐀𝐑𝐀!
01-08-2026