BURIANI DKT SAM NUJOMA
Katibu wa NEC Mambo ya Siasa na Uhusiano wa kimataifa CCM (SUKI) Ndg. Rabia Abdalla Hamid asaini kitabu cha maombolezo kufuatia kifo cha Rais wa kwanza wa Namibia na mpigania uhuru maarufu, Dk. Sam Nujoma.
Ndg Rabia amesaini Kitabu hicho katika ofisi za ubalozi wa nchi hiyo zilizopo Masaki, jijini Dar es Salaam leo Februari 18, 2025.