KATIBU wa Kamati Maalum ya NEC,Idara ya Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUK) CCM Zanzibar Khadija Salum Ali,amesema Chama Cha Mapinduzi kitaendelea kuthamini uhusiano wa kisiasa na kijamii uliopo baina yake na Chama Tawala cha Msumbiji cha Frelimo.
Hayo ameyasema wakati akizungumza na Balozi Mdogo wa Msumbiji anayefanyia kazi zake Zanzibar Agostinho Abacar Trinza, huko Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar.
Ndugu Khadija,alisema uhusiano huo ulianza kabla ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 ambapo Tanzania kwa kiasi kikubwa ilisaidia Msumbiji kufanikisha malengo yake ya kujitawala yenye,hatua ambayo ni kumbukumbu muhimu katika historia ya ukomboni wa nchi za Bara la Afrika.
"Chama Cha Mapinduzi kinaheshimu na kulinda mahusiano yake na Vyama rafiki vyote duniani,lakini kwa upande wa Msumbiji urafiki wetu umekuwa wa kipekee kutokana na ukaribu wetu ambao kwa sasa wapo Wazanzibar na Watanzania wengi wanaishi Msumbiji na pia wapo Wananchi wengi wa Msumbiji waishi kwa amani hapa Zanzibar.",alisema Katibu huyo wa Kamati Maalum ya NEC Khadija.
Kwa upande wa Balozi mdogo wa Msumbiji Zanzibar Agostinho Abacar Trinza,alisema Chama Frelimo na Serikali ya Msumbiji vinajivunia uwepo uhusiano wa kijamii unaotoa fursa kwa Wananchi wa Msumbiji kuishi kwa amani na utulivu nchini.
Balozi Trinza,aliwapongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Mwinyi kwa kazi kubwa ya kuwaletea Wananchi maendeleo endelevu katika nyanja za kiuchumi,kisiasa,kijamii na kidiplomasia.
"Tunaona namna Tanzania bara na Zanzibar zinavyopiga hatua kubwa ya maendeleo yote hayo yanafanyika kwa ufanisi,kutokana na uwepo wa amani na utulivu katika nchi hii",alieleza Balozi Trinza.
Baada ya mazungumzo hayo Balozi Agostinho Abacar,alitembelea maeneo mbali mbali ya kihistoria yaliyopo Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui pamoja na kuzuru kaburi la aliyekuwa Rais wa kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi marehemu Abeid Amani Karume
CCM NA FRELIMO KUIMARISHA USHIRIKIANO WA KIUCHUMI
13-03-2026
UZINDUZI WA JENGO LA MAKAO MAKUU YA ULINZI WA TAIFA
13-03-2026
CCM YAIPA POLE MSUMBIJI KWA KUKUMBWA NA MAFURIKO
13-03-2026
INJINI YA CHAMA CHA MAPINDUZI IPO MASHINANI; DKT.MIGIRO
13-03-2026
DK.MIGIRO:CCM INAJENGWA KUANZIA NGAZI YA MASHINA SIO MAJUKWAANI.
13-03-2026
πππ¦πππ‘ππ’ πππ πππ§. π ππππ₯π’ ππππ£π’πππππͺπ ππͺπ π¦πππ‘ππͺπ πππ₯ ππ¦ π¦πππππ
13-03-2026
NAIBU KATIBU MKUU WA CCM BARA AMWAKILISHA KATIBU MKUU WA CCM KWENYE MSIBA WA MBUNGE WA JIMBO LA PERAMIHO
13-03-2026
π©ππππ‘π π§π¨ππππ‘ππ ππ ππ‘π π¬π π‘πππ π¬ππ§π¨ - π πͺππ‘πππ πππ‘ππ‘π
13-03-2026
DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AONGOZA KIKAO MAALUMU CHA KAMATI KUU YA CCM
13-03-2026
RAIS SAMIA AKIWAAPISHA MAWAZIRI NA MANAIBU WAZIRI WATEULE- IKULU CHAMWINO DODOMA
13-03-2026
WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU NCHEMBA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA DODOMA (GENERAL)
13-03-2026
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ..
13-03-2026
RAIS SAMIA AKIHUTUBIA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
13-03-2026
DKT SAMIA:TUNAFANYA UCHAGUZI KWA FEDHA ZETU WENYEWE
13-03-2026
MGOMBEA URAIS KUPITIA CCM DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA MANYARA
13-03-2026
π¨ππππ£πππππ πͺπ πππ§. π¦ππ ππ π¨π ππππ§π ππ ππ‘π ππͺπ πͺππ£ππ‘πππ‘π, πͺππππ¨ππππ πππ
πππ©πππͺ ππ πͺπͺ πΏπ π©. πππππ§π€ ππ¬ππ₯π€π ππ πππ€π£ππ€π―π π¬π πΎππΌπΏπππΌ π£π πΌπΎπ
13-03-2026
πππ§. π¦ππ ππ ππ§π¨π π‘πππ‘π π¬π ππ₯πππ π¬π ππππ’π π
13-03-2026
KATIBU MKUU WA CCM, BALOZI DKT. ASHA-ROSE MIGIRO AKUTANA NA RAIS MWINYI – ZANZIBAR
13-03-2026
ILANI YA UCHAGUZI YA CCM 2025-2030
13-03-2026
WASIRA:CCM HATUKATI MGOMBEA ILA TUNATEUA WACHACHE KATI YA WENGI
13-03-2026