Serikali itaendelea kuweka mazingira Bora kwa Taasisi na Mashirika binafsi katika kuhakikisha wanatimiza majukumu yao ya utoaji wa huduma za msaada wa kisheria haapa -nchini.
Ameyasema hayo katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla katika kilele cha maadhimisho ya Tano(5) ya wiki ya msaada wa kisheria Zanzibar yaliyofanyika katika Ukumbi wa asheikh aidrisa Abdul Wakil Kikwajuni Zanzibar.
Rais Dkt Mwinyi amesema Serikali kwa kushirikiana na Idara ya Katiba na Sheria itaendelea kutekeleza kampeni Kitaifa ya msaada wa Kisheria ya Mama Samia na Kampeni nyenginezo za Kitaifa na Kimataifa kwa lengo la kuwawezesha wananchi katika suala la upatikanaji wa haki zao.
Aidha Dkt Mwinyi amesema watoa huduma za msaada wa Kisheria wamekuwa wakombozi wakubwa kwa jamii katika masuala ya kisheria, kwa kutoa elimu ya kisheria na msaada wa kisheria kwa makundi mbali mbali wakiwemo vijana, wazee, watu wenye Ulemavu na wanafunzi ambapo wameweza kuwafikia wananchi laki nne kumi na tisa elfu mia nne na moja ( 419, 401) kati yao wanawake ni laki mbili ishirini na sita elfu mia moja na sabiini na mbili ( 226, 172) ni wanawake na laki moja tisiini na tatu mia mbili na ishirini na tisa (193, 229) ni wanaume.
Sambamba na hayo Rais Dkt Mwinyi amesema uwepo wa namba maalum itakayowasaidia wananchi katika upatikanaji wa huduma za Msaada wa Kisheria ni hatua muhimu inayohamasisha upatikanaji wa huduma hio na itakuwa kiungo kikubwa baina ya watoa huduma za Msaada wa Kisheria na wananchi ambao wengi wao mjini na vijijini wanamiliki vifaa vya kieletroniki ikiwemo simu za mkononi.
Rais Dkt Mwinyi ametoa wito kwa Idara ya Katiba na Msaada wa kisheria pamoja na watoa huduma za Msaada wa Kisheria kuendelea kuelimisha wananchi juu ya uwepo wa namba hio maalum ya Huduma za Msaada wa Kisheria pamoja na upatikanaji wa huduma hizo kwa njia ya Teknolojia na kuwataka wananchi kuitumia vyema namba hio kwa utaratibu uliowekwa ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Nae Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora Mhe. Haroun Ali Suleiman amesema watoa Msaada wa Kisheria wanafanya kazi kubwa ya kujitolea katika kutoa elimu ya Sheria na Msaada wa kisheria kwa wananchi hivyo ameiomba Serikali kuangalia ni kwa namna gani itawasaidia watoa huduma hao katika kuendelea kutekeleza majukumu yao ya kila siku.
Waziri Haroon amesema ili kuendelea kuisaidia jamii katika kuwapatia elimu na kutoa Msaada wa Kisheria ni lazima kuwepo na mazingira mazuri ya kufanyia kazi, hivyo amewaomba Wakuu wa Mikoa na Wilaya kuwapatia ofisi watoaji wa Msaada wa kisheria katika kila Wilaya ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa utulivu na kwa ufanisi mkubwa.
Kwa upande wao wawakilishi wa mashirika ya msaada wakisheria wakiwemo UNDP, LSF na UN WEMEN wamesema wataendela kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na wadau mbali mbali katika kupambana ili kuhakikisha upatikanaji wa haki kwa wahanga wa vitendo vya Ukatili na Udhalilishaji wa kijinsia hasa wanawake na watoto uanpatikana kwa wakati.
Wamesema kusaidia na kupambana kwa hali zote katika harakati mbali mbali za kimaendelo hasa katika kuhakikisha upatikanaji wa haki, haki za Binaadamu zinalindwa na kuhakikisha elimu ya Sheria inawafikia wananchi wote mijini na vijini.
Mapema Mkurugenzi wa Idara ya Katiba na Msaada wa Kisheria Bi. Hanifa Ramadhan Said amesema Idara ya Katiba imeona ipo haja ya kuanzisha namba maalum ambayo itatumika katika kurahisisha upatikanaji wa Msaada wa kisheria na kuwa kiunganishi kikubwa kati wa Idara , watoa huduma za Msaada wa Kisheria na wananchi.
Mkurugenzi Hanifa amesema Idara ya Katiba na Msaada wa kisheria itahakikisha inazidisha ushirikiano katika utendaji wa kazi baina yao na watoa huduma za Msaada wa Kisheria ili lengo halisi la upatikanaji wa haki, kutokomeza Ukatili na Unyanyasaji wa kijinsia kwa wananchi liweze kufikiwa .
Amezishukuru Taasisi na Mashirika mbali mbali ikiwemo L.S.F, UNDP, UN WOMEN Mahakama, Polisi na Chuo cha Mafunzo kwa ushirikiano wao mkubwa wanaoendelea kuwapatia ambao unarahisisha katika harakati zao za ufanyaji wa kazi za kila siku.
Nao watoaji Msaada wa kisheria Wameishukuru Idara ya Katiba na Msaada wa kisheria kwa kuwapatia ushirikiano mkubwa unaowapelekea kufanya kazi zao za uweledi na ufanisi mkubwa sambamba na kuiomba serikali za mikoa na wilaya kuwapatia ofisi za kufanyia kazi zao ili kufikia malengo waliojiwekea.
DKT SAMIA:TUNAFANYA UCHAGUZI KWA FEDHA ZETU WENYEWE
28-10-2025
MGOMBEA URAIS KUPITIA CCM DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA MANYARA
28-10-2025
π¨ππππ£πππππ πͺπ πππ§. π¦ππ ππ π¨π ππππ§π ππ ππ‘π ππͺπ πͺππ£ππ‘πππ‘π, πͺππππ¨ππππ πππ
πππ©πππͺ ππ πͺπͺ πΏπ π©. πππππ§π€ ππ¬ππ₯π€π ππ πππ€π£ππ€π―π π¬π πΎππΌπΏπππΌ π£π πΌπΎπ
28-10-2025
πππ§. π¦ππ ππ ππ§π¨π π‘πππ‘π π¬π ππ₯πππ π¬π ππππ’π π
28-10-2025
KATIBU MKUU WA CCM, BALOZI DKT. ASHA-ROSE MIGIRO AKUTANA NA RAIS MWINYI – ZANZIBAR
28-10-2025
ILANI YA UCHAGUZI YA CCM 2025-2030
28-10-2025
WASIRA:CCM HATUKATI MGOMBEA ILA TUNATEUA WACHACHE KATI YA WENGI
28-10-2025
WANACHAMA 280 WA CHADEMA WATIMKIA CCM
28-10-2025
BALOZI NCHIMBI: MAONI YOYOTE KUHUSU AMANI YA TANZANIA HAYATAPUUZWA
28-10-2025
π¦ππ₯πππππ π¬π π₯πππ¦ πππ§. π¦ππ ππ ππ ππͺπππ ππππ π π¬π π πππ‘πππππ’ ππππ π¦ππππ π¨ - ππ£π. ππ π’π¦ π ππππππ
28-10-2025
MAKALLA: BARABARA YA MPWAPWA NJIAPANDA KONGWA KUJENGWA LAMI
28-10-2025
BALOZI NCHIMBI AWASILI ARUSHA
28-10-2025
TAARIFA KWA UMMA
28-10-2025
UCHAGUZI MKUU SIO AJALI-WASIRA
28-10-2025
πͺπππ¨π ππ π π¦ππππππ¨π π©ππ’π‘ππ’ππ ππππππππ ππͺππ‘π¬π ππ¨π₯π ππ π ππ’π‘π - (π ππ) πππ©π¨
28-10-2025
MONGELLA AONGOZA MAZISHI YA KADA WA CCM JIJINI MWANZA
28-10-2025
ASIYETII SHERIA, KATIBA NA KUWA TAYARI KUUA KWA MASLAHI BINAFSI HUO NI UGAIDI’
28-10-2025
πππ π¬ππ¦ππ¦ππ§πππ πͺπππ’π πππ ππ¨πππππππͺπ ππͺπ ππ¨πππ‘πππ§ππ π¨πͺπππ’, π¨πππππ‘ππ’ π‘π π¨πππππππ¨, π¬ππππ ππ π πππ¨π‘ππ - πππ. πππ©π¨
28-10-2025
KAENI KIMYA KAMA HAMJUI NCHI ILIKOTOKA - WASIRA
28-10-2025
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefungua kiwanda cha kutengeneza mabomba ya maji na uchakataji pamba cha MOLI Oil Mills Co. Ltd kilichopo Bariadi Mkoani Simiyu tarehe 16 Juni, 2025.
28-10-2025