Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


BALOZI NCHIMBI MSIBANI KWA MZEE MONGELLA

alternative

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, akisaini kitabu cha maombolezo na kumpatia pole, Mama Gertrude Ibengwe Mongella, familia yake na waombolezaji wengine, kwa msiba wa Mzee Silvin Ibengwe Emmanuel Mongella, ambaye ni mwenza wa Mama Mongella, leo Jumanne, tarehe 3 Juni 2025, eneo la Makongo juu, jijini Dar Es Salaam. 

Marehemu Mzee Mongella (85), ambaye pia ni baba mzazi wa John Mongella, Naibu Katibu Mkuu wa CCM (bara), alifariki tarehe 31 Mei 2025, na mazishi yake yamepangwa kufanyika huko Mwanza, tarehe 7 Juni 2025.
 

alternative alternative alternative alternative
Habari Nyingine