Makamu wa Pili wa Rais Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendeleza ushirikiano na Serikali ya Jamhuri ya watu wa China katika mambo mbali ya Kimaendeleo ikiwemo Sekta ya Uchumi wa Buluu, Miundombinu, Mafuta na gesi.
Ameyasema hayo wakati alipofanya mazungumzo na Gavana wa jimbo la JIANGSU nchini China Bwana XU KUNLIN na ujumbe wake waliofika ofisini kwake Vuga kwa ajili ya kufanya mazungumzo kufuatia kutimia kwa miaka 60 ya ushirikiano wa China na Zanzibar katika sekta ya Afya.
Amesema, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeipa kipaumbele Sekta ya uchumi wa Buluu ambayo imekuwa ikitoa fursa mbali mbali za ajira kwa wananchi hivyo amemtaka Gavana huyo kuendeleza mashirikiano katika sekta hio pamoja na Sekta nyengine ikiwemo Afya, Miundombinu, Utalii, Mafuta na Gesi.
Mhe. Hemed amesema wakati China na Zanzibar inatimiza miaka 60 ya ushirikiano katika Sekta mbali mbali ikiwemo sekta ya Afya, Zanzibar inajivunia kuendelea kupokea madaktari wa kada mbali mbali kutoka China ambao wamekuwa wakifanya kazi kwa bidii na kutoa msaada mkubwa katika masuala ya Kitabibu.
Sambamba na hayo, Makamu wa Pili wa Zanzibar amemuhakikishia Gavana XU KUNLIN kuwa Zanzibar itaendeleza ushirikiano uliopo na Serikali ya watu wa China na kuwataka kuendelea kuwekeza Zanzibar katika maeneo mbali mbali ya kiuchumi na kimaendeleo.
Kwa upande wake Gavana wa Jimbo la JIANGSU nchini china Bwana XU KUNLIN ameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa ushirikiano wa muda mrefu kupitia Nyanja mbali mbali ikiwemo za elimu na afya .
Amesema Jimbo la JIANGSU limekuwa likipiga hatua katika mambo mbali mbali yakiwemo masuala ya Uchumi hivyo wako tayari kushirikiana na Zanzibar katika eneo hilo ili kuhakikisha inazidi kupiga hatua kwa maslahi mapana ya wananchi wa pande zote mbili.
Bwana XU KUNLIN amesema katika sekta ya Afya China itahakikisha inaendeleza ushirikiano na Zanzibar katika suala la Teknolojia katika kukinga na kutibu maradhi mbali mbali sambamba na kuwapatia Taaluma na kuwajengea uzoefu watendaji wa Wizara ya Afya .
Nae Waziri wa Afya Mhe. Nassor Ahmed Mazurui ameishukuru Serikali ya watu wa China kwa kuendelea kuisaidia Zanzibar hasa katika sekta ya Afya kwa kuleta madaktari bingwa kuja Zanzibar kwa kutoa msaada wa kitabibu kila mwaka na kuwajengea uwezo madaktari wazawa .
Mhe. Mazurui amesema Miaka 60 ya ushirikiano katika sekta ya Afya kwa Serikali ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya watu wa China umeleta mabadiliko makubwa ya kimaendeleo katika sekta ya hio ikiwemo kuboreshwa kwa upatikanaji wa huduma kuanzia Vituo vya Afya hadi Hospitali ya Rufaa zilizopo nchini.
DKT SAMIA:TUNAFANYA UCHAGUZI KWA FEDHA ZETU WENYEWE
26-10-2025
MGOMBEA URAIS KUPITIA CCM DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA MANYARA
26-10-2025
π¨ππππ£πππππ πͺπ πππ§. π¦ππ ππ π¨π ππππ§π ππ ππ‘π ππͺπ πͺππ£ππ‘πππ‘π, πͺππππ¨ππππ πππ
πππ©πππͺ ππ πͺπͺ πΏπ π©. πππππ§π€ ππ¬ππ₯π€π ππ πππ€π£ππ€π―π π¬π πΎππΌπΏπππΌ π£π πΌπΎπ
26-10-2025
πππ§. π¦ππ ππ ππ§π¨π π‘πππ‘π π¬π ππ₯πππ π¬π ππππ’π π
26-10-2025
KATIBU MKUU WA CCM, BALOZI DKT. ASHA-ROSE MIGIRO AKUTANA NA RAIS MWINYI – ZANZIBAR
26-10-2025
ILANI YA UCHAGUZI YA CCM 2025-2030
26-10-2025
WASIRA:CCM HATUKATI MGOMBEA ILA TUNATEUA WACHACHE KATI YA WENGI
26-10-2025
WANACHAMA 280 WA CHADEMA WATIMKIA CCM
26-10-2025
BALOZI NCHIMBI: MAONI YOYOTE KUHUSU AMANI YA TANZANIA HAYATAPUUZWA
26-10-2025
π¦ππ₯πππππ π¬π π₯πππ¦ πππ§. π¦ππ ππ ππ ππͺπππ ππππ π π¬π π πππ‘πππππ’ ππππ π¦ππππ π¨ - ππ£π. ππ π’π¦ π ππππππ
26-10-2025
MAKALLA: BARABARA YA MPWAPWA NJIAPANDA KONGWA KUJENGWA LAMI
26-10-2025
BALOZI NCHIMBI AWASILI ARUSHA
26-10-2025
TAARIFA KWA UMMA
26-10-2025
UCHAGUZI MKUU SIO AJALI-WASIRA
26-10-2025
πͺπππ¨π ππ π π¦ππππππ¨π π©ππ’π‘ππ’ππ ππππππππ ππͺππ‘π¬π ππ¨π₯π ππ π ππ’π‘π - (π ππ) πππ©π¨
26-10-2025
MONGELLA AONGOZA MAZISHI YA KADA WA CCM JIJINI MWANZA
26-10-2025
ASIYETII SHERIA, KATIBA NA KUWA TAYARI KUUA KWA MASLAHI BINAFSI HUO NI UGAIDI’
26-10-2025
πππ π¬ππ¦ππ¦ππ§πππ πͺπππ’π πππ ππ¨πππππππͺπ ππͺπ ππ¨πππ‘πππ§ππ π¨πͺπππ’, π¨πππππ‘ππ’ π‘π π¨πππππππ¨, π¬ππππ ππ π πππ¨π‘ππ - πππ. πππ©π¨
26-10-2025
KAENI KIMYA KAMA HAMJUI NCHI ILIKOTOKA - WASIRA
26-10-2025
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefungua kiwanda cha kutengeneza mabomba ya maji na uchakataji pamba cha MOLI Oil Mills Co. Ltd kilichopo Bariadi Mkoani Simiyu tarehe 16 Juni, 2025.
26-10-2025