Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Hemed Suleiman Abdulla amewataka viongozi wa Jumuiya ya wavuvi ya Kiwani(JUWAKI) kuvitunza na kuvitumia kwa uangalifu vifaa pamoja na Boti za uvuvi walizopatiwa na Benki ya NMB ili viweze kudumu kwa muda mrefu sambamba na kuwasaidia katika kujikimu kimaisha
Ameyasema hayo wakati akizindua Mkopo maalumu wa boti yaani (Master boat) Uliotolewa na Bank ya NMB kwa jumuiya ya wavuvi wa Kiwani (JUWAKI) hafla iliyofanyika katika kijiji cha Tasani kiwani Mkoa wa Kusini Pemba.
Amesema kuwa boti hizo tano (5) za kisasa zikiwa na vifaa kamili vya kuvulia waliyokabidhiwa wavuvi wa Kiwani zitasaidia kutoa ajira kwa wananchi wa kiwani na vitongoji vyake pamoja na kukuza kipato cha mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.
Mhe Hemed amesema endapo wavuvi na wananchi wa Kiwani watazitumia vyema boti hizo na kurejesha mkopo waliopatiwa na NMB Benk kwa wakati, Serikali ya Awamu ya Nane (8) inayoongozwa na Rais Dkt Hussen Mwinyi itawajengea mtambo wa kuhifadhia samaki kijijini hapo sambamba na kuwatafutia soko la kuuza samaki ndani na nje ya nchi.
Aidha, amewahakikishia wananchi wa Kiwani kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kutafuta namna bora ya kuwaletea wananchi wake maendeleo ikiwa ni pamoja na kuwawezesha kiuchumi.
Mhe Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesisitiza umoja na ushirikiano na kuachana na tabia ya ubaguzi wa aina yoyote ikiwemo ya itikadi za vyama vya siasa na badala yake kufanya kazi kwa pamoja kwa maslahi ya nchi kama dhamira ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yanavyopinga ubaguzi na kusisitiza mshikamano kwa wazanzibari wote.
Sambamba na hayo Mhe. Hemed amekemea vikali vitendo vya udhalilishaji wa wanawake na watoto, ubakaji na ulawiti kwa watoto wa kiume na kuwataka wananchi kuachana na rushwa ya muhali kwa kuwa tayari kutoa ushirikiano kwa vyombo ya sheria ili haki iweze kutendeka .
Nae Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Mhe. Suleiman Massoud Makame amesema kuwa kijiji cha Kiwani ni miongoni mwa eneo linalozalisha mwani kwa wingi kwa Mkoa wa Kusini Pemba, hii ni kutokana na Rais Dkt Mwinyi kulithaminisha zao la mwani na kuwapa ari na hamasa wakulima wa mwani kujikita zaidi katika ukulima wa zao hilo.
Amesema kuwa Sekta ya Uvuvi inachangia kwa asilimia 9 ya mpango wa GDV katika kukuza uchumi wa Zanzibar na kuwaletea wananchi maendeleo.
Massoud ameishukuru Benki ya NMB kwa kuendelea kufanya kazi na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hasa katika Sekta ya Uchumi wa Buluu kwa kuwapatia wananchi mikopo nafuu na Vifaa vya Uvuvi ambapo Kisiwani Pemba maeneo mbali yameshafaidika kupitia Benk ya NMB.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya wavuvi wa Kiwani (JUWAKI) ndugu Kassim Omar Suleiman amemshukuru Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe Dkt Hussen Ali Mwinyi kwa kuendelea kuwajali wavuvi na wakulima wa mwani kwa kuwawekea mazingira mazuri na wezeshi ya kufanyia kazi zao.
Amesema JUWAKI inaahidi kuwasimamia wavuvi katika kuvitunza na kuvitumia vizuri vifaa hivyo na kuhakikisha wanarejesha mikopo kwa wakati ili na wengine waweze kunufaika na mikopo inayotolewa na Benki ya NMB.
UZINDUZI WA JENGO LA MAKAO MAKUU YA ULINZI WA TAIFA
04-03-2026
CCM YAIPA POLE MSUMBIJI KWA KUKUMBWA NA MAFURIKO
04-03-2026
INJINI YA CHAMA CHA MAPINDUZI IPO MASHINANI; DKT.MIGIRO
04-03-2026
DK.MIGIRO:CCM INAJENGWA KUANZIA NGAZI YA MASHINA SIO MAJUKWAANI.
04-03-2026
πππ¦πππ‘ππ’ πππ πππ§. π ππππ₯π’ ππππ£π’πππππͺπ ππͺπ π¦πππ‘ππͺπ πππ₯ ππ¦ π¦πππππ
04-03-2026
NAIBU KATIBU MKUU WA CCM BARA AMWAKILISHA KATIBU MKUU WA CCM KWENYE MSIBA WA MBUNGE WA JIMBO LA PERAMIHO
04-03-2026
π©ππππ‘π π§π¨ππππ‘ππ ππ ππ‘π π¬π π‘πππ π¬ππ§π¨ - π πͺππ‘πππ πππ‘ππ‘π
04-03-2026
DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AONGOZA KIKAO MAALUMU CHA KAMATI KUU YA CCM
04-03-2026
RAIS SAMIA AKIWAAPISHA MAWAZIRI NA MANAIBU WAZIRI WATEULE- IKULU CHAMWINO DODOMA
04-03-2026
WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU NCHEMBA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA DODOMA (GENERAL)
04-03-2026
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ..
04-03-2026
RAIS SAMIA AKIHUTUBIA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
04-03-2026
DKT SAMIA:TUNAFANYA UCHAGUZI KWA FEDHA ZETU WENYEWE
04-03-2026
MGOMBEA URAIS KUPITIA CCM DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA MANYARA
04-03-2026
π¨ππππ£πππππ πͺπ πππ§. π¦ππ ππ π¨π ππππ§π ππ ππ‘π ππͺπ πͺππ£ππ‘πππ‘π, πͺππππ¨ππππ πππ
πππ©πππͺ ππ πͺπͺ πΏπ π©. πππππ§π€ ππ¬ππ₯π€π ππ πππ€π£ππ€π―π π¬π πΎππΌπΏπππΌ π£π πΌπΎπ
04-03-2026
πππ§. π¦ππ ππ ππ§π¨π π‘πππ‘π π¬π ππ₯πππ π¬π ππππ’π π
04-03-2026
KATIBU MKUU WA CCM, BALOZI DKT. ASHA-ROSE MIGIRO AKUTANA NA RAIS MWINYI – ZANZIBAR
04-03-2026
ILANI YA UCHAGUZI YA CCM 2025-2030
04-03-2026
WASIRA:CCM HATUKATI MGOMBEA ILA TUNATEUA WACHACHE KATI YA WENGI
04-03-2026
WANACHAMA 280 WA CHADEMA WATIMKIA CCM
04-03-2026