SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR IMEAHIDI KUWALIPA FIDIA YA VIPANDO NA MAJENGO WANANCHI WOTE WA ENEO LA BUMBWINI WALIOPITIWA NA MRADI WA BARABARA NA UJENZI WA BANDARI JUMUISHI YA MANGAPWANI.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi ameyasema hayo alipozungumza na wananchi wa Bumbwini Misufini, shehia ya Kidanzini, kijiji cha Mwembe mdema, Mkoa wa Kaskazini Unguja alipofanya ziara ya kutembelea ujenzi wa nyumba za fidia kwa wananchi waliopisha miradi ya maendeleo kijijini hapo.
Amesema, tayari zoezi la ulipwaji wa fidia kwa baadhi ya wananchi hao limeanza kwa wakaazi wa Mangapwani na baadae kumalizia vijiji nyengine vilivyopitiwa na miradi hiyo. “Kwa wale wote wanaostahili kulipwa fidia iwe ya vipando au majengo, tunahakikisha
fidia zenu mtalipwa nyote kwa kipidi kifupi” Dk. Mwinyi aliwahakikishia wananchi hao. Aidha, Rais Dk. Mwinyi aliwashauri viongozi wa jimbo hilo, kushirikiana na Mkandarasi wa mradi wa nyumba za wananchi zinazoendelea kujengwa kwenye maeneo ya Mwembe mdema, Shehia ya Kidanzini na nyumba za Mangapwani kwa kuangalia mahitaji halisi ya aina ya nyumba wananchi watakazoridhika nazo.
Pia, aliishauri kamati inayosimamia ujenzi wa nyumba hizo, kushirikiana na mkandarasi kujenga nyumba zitakazokidhi haja za walengwa ili kuwaepushia usumbufu wa baadae. Akizungumza kwenye hafla hiyo, Waziri wa Ujenzi na Mawasiliano, Dk. Khalid Salum
Muhamed, amesema hatua za ujenzi wa awali wa nyumba hizo zitasaidisha kuboshesha mwendelezo wa nyumba zitakazofuata kwa kuepuka changamoto zilizojitokeza baada ya kukamilika nyumba mbili za mwanzo.
Akigusua suala la fidia Dk. Khalid pia alieleza mbali ya fidia za mazao na nyumba lakini wananchi waliopoteza maeneo yao, ikiwemo viwanja alisema, tayari Serikali imeunda kamati inayojumuisha wataalamu wa ardhi na wanasheria kulishighulikia suala hilo ili kukamilisha ahadi ya Serikali ya kulipwa na kueleza tayari eneo hilo limefanyiwa tathmini na tayari ripoti imetoka.
Nae, Mkandarasi wa ujenzi wa nyumba hizo kampuni ya “Orkun” kutoka Uturuki, imeiahidi Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kufanya maboresho kwa mujibu ya maelekezo wanayokubaliana. Ujenzi wa nyumba hizo unatarajiwa kukamilisha nyumba 370 kwa wananchi wa maeneo ya Bumbwini Misufini pamoja na wakaazi wa maeneo ya Mangapwani ikiwa ni sehemu ya fidia yao watakayopewa na Serikali baada ya kupisha miradi ya maendeleo iliwemo miundombinu ya barabara na ujenzi wa bandari kubwa ya Mangapwani.
Ujenzi huo pia utahusisha maduka ya biasahara na skuli ya maandalizi, miundombinu ya maji safi na maji taka, zikiwemo barabara za ndani ya eneo hilo za kiwango cha lami pamoja na mitaro ya maji machafu.
DKT SAMIA:TUNAFANYA UCHAGUZI KWA FEDHA ZETU WENYEWE
06-11-2025
MGOMBEA URAIS KUPITIA CCM DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA MANYARA
06-11-2025
π¨ππππ£πππππ πͺπ πππ§. π¦ππ ππ π¨π ππππ§π ππ ππ‘π ππͺπ πͺππ£ππ‘πππ‘π, πͺππππ¨ππππ πππ
πππ©πππͺ ππ πͺπͺ πΏπ π©. πππππ§π€ ππ¬ππ₯π€π ππ πππ€π£ππ€π―π π¬π πΎππΌπΏπππΌ π£π πΌπΎπ
06-11-2025
πππ§. π¦ππ ππ ππ§π¨π π‘πππ‘π π¬π ππ₯πππ π¬π ππππ’π π
06-11-2025
KATIBU MKUU WA CCM, BALOZI DKT. ASHA-ROSE MIGIRO AKUTANA NA RAIS MWINYI – ZANZIBAR
06-11-2025
ILANI YA UCHAGUZI YA CCM 2025-2030
06-11-2025
WASIRA:CCM HATUKATI MGOMBEA ILA TUNATEUA WACHACHE KATI YA WENGI
06-11-2025
WANACHAMA 280 WA CHADEMA WATIMKIA CCM
06-11-2025
BALOZI NCHIMBI: MAONI YOYOTE KUHUSU AMANI YA TANZANIA HAYATAPUUZWA
06-11-2025
π¦ππ₯πππππ π¬π π₯πππ¦ πππ§. π¦ππ ππ ππ ππͺπππ ππππ π π¬π π πππ‘πππππ’ ππππ π¦ππππ π¨ - ππ£π. ππ π’π¦ π ππππππ
06-11-2025
MAKALLA: BARABARA YA MPWAPWA NJIAPANDA KONGWA KUJENGWA LAMI
06-11-2025
BALOZI NCHIMBI AWASILI ARUSHA
06-11-2025
TAARIFA KWA UMMA
06-11-2025
UCHAGUZI MKUU SIO AJALI-WASIRA
06-11-2025
πͺπππ¨π ππ π π¦ππππππ¨π π©ππ’π‘ππ’ππ ππππππππ ππͺππ‘π¬π ππ¨π₯π ππ π ππ’π‘π - (π ππ) πππ©π¨
06-11-2025
MONGELLA AONGOZA MAZISHI YA KADA WA CCM JIJINI MWANZA
06-11-2025
ASIYETII SHERIA, KATIBA NA KUWA TAYARI KUUA KWA MASLAHI BINAFSI HUO NI UGAIDI’
06-11-2025
πππ π¬ππ¦ππ¦ππ§πππ πͺπππ’π πππ ππ¨πππππππͺπ ππͺπ ππ¨πππ‘πππ§ππ π¨πͺπππ’, π¨πππππ‘ππ’ π‘π π¨πππππππ¨, π¬ππππ ππ π πππ¨π‘ππ - πππ. πππ©π¨
06-11-2025
KAENI KIMYA KAMA HAMJUI NCHI ILIKOTOKA - WASIRA
06-11-2025
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefungua kiwanda cha kutengeneza mabomba ya maji na uchakataji pamba cha MOLI Oil Mills Co. Ltd kilichopo Bariadi Mkoani Simiyu tarehe 16 Juni, 2025.
06-11-2025