RAIS wa Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali anayoiongoza tayari imepita lengo la Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinzi (CCM) ya kutaka zijengwe barabara za kilomita 200 Unguja na Pemba na badala yake imetekeleza kwa vitendo ujenzi wa kilomita 500 za barabara zilizojengwa nchi nzima.
Dk. Mwinyi, ameyasema hayo alipoweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya kilomita 6.5 ya Uwanja wa ndege, Kiembesamaki hadi Mmazi Moja Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi, ikiwa ni mwendelezo wa shamrashamra za miaka 60 ya
Mapinduzi ya Zanzibar. Alisema, Serikali inajenga mtandao wa barabara za kilomita 100 mijini kwa Unguja na Pemba pamoja na ujenzi wa kilomita 130 za barabara za Tunguu-Makunduchi, Kisauni - Fumba na Chake – Mkoani, Pemba mbali na barabara za kilomita 285 za vijini.
Rais Dk. Mwinyi alieleza, ujenzi wa barabara hizo zinazotegemewa kudumu kwa zaidi ya miaka 50 hadi 70 ijayo kutokana na uimara na ubora wa kiwango cha hali ya juu uliojumuishwa na miundombinu ya kupishia maji ikiwemo mitaro ya maji machafu, miundombinu ya huduma za jamii ikiwemo maji safi, umeme na njia za mawasiliano pamoja na barabara za watembea kwa miguu. Akizungumzia adha za usafiri wa umma nchini, Rais Dk. Mwinyi alieleza, Serikali imedhamiria kuondosha changamoto ya foleni barabarani na usumbufu kwa wananchi ikiwemo ujenzi wa barabara za juu Amani - Mwanakwerekwe.
Rais Dk. Mwinyi pia alieleza, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imekusudia kuweka usafiri wa umma wa uhakika ili kuwaondoshea wananchi wake usumbufu kwa kuleta mabasi ya kisasa yatakayokidhi haja za wananchi. Akizungumzia kuimarisha na kuendelea kutunza mazingira endelevu, Rais Dk. Mwinyi alisema Serikali inampango wa kuweka usafiri wa umma utakaotumia gasi na umeme pamoja na kudhibiti changamoto zinazosababishwa na usafiri huo kwa kuendelea kujenga vituo vingi vya mabasi ya usafiri wa umma.
Pia Rais Dk. Mwinyi aliwatanabahisha wananchi kuzitumia vizuri barabara hizo kwa kukuza uchumi wa nchi sio kusababisha maafa na ajali kwa kujiepusha uvunjifu wa sheria barabarani na kuepuka mwendo wa kasi. Aidha, aliviomba vyombo vya usalama barabarani kuwachukulia hatua kali za sheria kwa madereva na watumiaji wa barabara hizo watakaokwenda kinyume na sheria.
Naye, Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi, Dk. Khalid Salum Mohamed alisema, Serikali imekusudia kurejesha historia ya Zanzibar ya mwaka 1879 ya usafiri wa umma wa treni kama iliyotoka Mji mkongwe hadi Chukwani na ile ya mjini hadi Bububu.
Alisema Serikali itajenga miundombinu ya kisasa ya usafiri treni za abiria pamoja na kuweka mfumo mpya wa mabasi ya umeme kwa maagizo ya Rais Dk. Mwinyi.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Khadija Khamis Rajab amesema, ujenzi wa barabara ya Uwanja wa ndege Mnazi mmoja wenye urefu wa kilomita 6.5 umegharimu zaidi ya shilingi bilioni 5, ina upana wa mita saba kila upande na uwezo wa kupitisha magari yenye uzito wa 50. Alisema barabara hiyo yenye ubora wa kiwango cha G45, imejumuisha mitaro kila upande, pamoja na madaraja madogo 41 yatakayopitisha miundominu ya huduma za jamii ikiwemo miundominu ya maji, umeme na mawasiliano, taa za barabarani na taa za kuongozea magari.
Akizunguza kuhusu fidia kwa wananchi walioathiriwa na barabara hiyo, Katibu Khadija alisema, hakuna fidia yoyote iliyogharimu Serikali kwa ujenzi wa barabara hiyo isipokuwa wananchi wawili ambao tayari washafanyiwa tathmini baada ya kuonekanwa kuna haja ya wao kupisha ujenzi wa barabara hiyo.
πππ¦πππ‘ππ’ πππ πππ§. π ππππ₯π’ ππππ£π’πππππͺπ ππͺπ π¦πππ‘ππͺπ πππ₯ ππ¦ π¦πππππ
08-01-2026
NAIBU KATIBU MKUU WA CCM BARA AMWAKILISHA KATIBU MKUU WA CCM KWENYE MSIBA WA MBUNGE WA JIMBO LA PERAMIHO
08-01-2026
π©ππππ‘π π§π¨ππππ‘ππ ππ ππ‘π π¬π π‘πππ π¬ππ§π¨ - π πͺππ‘πππ πππ‘ππ‘π
08-01-2026
DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AONGOZA KIKAO MAALUMU CHA KAMATI KUU YA CCM
08-01-2026
RAIS SAMIA AKIWAAPISHA MAWAZIRI NA MANAIBU WAZIRI WATEULE- IKULU CHAMWINO DODOMA
08-01-2026
WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU NCHEMBA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA DODOMA (GENERAL)
08-01-2026
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ..
08-01-2026
RAIS SAMIA AKIHUTUBIA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
08-01-2026
DKT SAMIA:TUNAFANYA UCHAGUZI KWA FEDHA ZETU WENYEWE
08-01-2026
MGOMBEA URAIS KUPITIA CCM DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA MANYARA
08-01-2026
π¨ππππ£πππππ πͺπ πππ§. π¦ππ ππ π¨π ππππ§π ππ ππ‘π ππͺπ πͺππ£ππ‘πππ‘π, πͺππππ¨ππππ πππ
πππ©πππͺ ππ πͺπͺ πΏπ π©. πππππ§π€ ππ¬ππ₯π€π ππ πππ€π£ππ€π―π π¬π πΎππΌπΏπππΌ π£π πΌπΎπ
08-01-2026
πππ§. π¦ππ ππ ππ§π¨π π‘πππ‘π π¬π ππ₯πππ π¬π ππππ’π π
08-01-2026
KATIBU MKUU WA CCM, BALOZI DKT. ASHA-ROSE MIGIRO AKUTANA NA RAIS MWINYI – ZANZIBAR
08-01-2026
ILANI YA UCHAGUZI YA CCM 2025-2030
08-01-2026
WASIRA:CCM HATUKATI MGOMBEA ILA TUNATEUA WACHACHE KATI YA WENGI
08-01-2026
WANACHAMA 280 WA CHADEMA WATIMKIA CCM
08-01-2026
BALOZI NCHIMBI: MAONI YOYOTE KUHUSU AMANI YA TANZANIA HAYATAPUUZWA
08-01-2026
π¦ππ₯πππππ π¬π π₯πππ¦ πππ§. π¦ππ ππ ππ ππͺπππ ππππ π π¬π π πππ‘πππππ’ ππππ π¦ππππ π¨ - ππ£π. ππ π’π¦ π ππππππ
08-01-2026
MAKALLA: BARABARA YA MPWAPWA NJIAPANDA KONGWA KUJENGWA LAMI
08-01-2026
BALOZI NCHIMBI AWASILI ARUSHA
08-01-2026