DEMOKRASIA SIO RUHUSA YA KUTUKANA WENGINE - Wasira
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira amesema uwepo wa demokrasia na uhuru wa kutoa maoni sio ruhusa ya kuvunja sheria, kutukana watu na kwamba anayefanya hivyo anastahili kuchukuliwa hatua ikiwemo kukamatwa na kuhojiwa polisi.
Amesema lengo la uhuru ni kutoa maoni na kufuata sheria ambazo zimewekwa kuifanya jamii iishi pamoja bila ya bughudha na kuondoa uwezekano wa mtu mmoja kumuonea mtu mwingine.
Wasira ameeleza hayo leo Juni 12, 2025 alipokuwa akizungumza na viongozi wa ngazi mbalimbali wa CCM wakiwemo mabalozi wa shina katika Jimbo la Peramiho, wilayani Songea mkoani Ruvuma.
"Siku hizi ukisoma mitandao eti matusi ndio demokrasia, eti matusi ndio uhuru ah! Uhuru wa kutukanana sasa hapo tumekosea njia, ungekuwa uhuru wenyewe ni wa kutukanana tungeutafuta wa nini, tulitafuta uhuru ili utusaidie kujenga watu pamoja kuleta amani katika nchi na kusimamia maendeleo yao.
"Uhuru ni kutoa maoni, uhuru ni kufuata sheria maana unaweka sheria ambazo zinaifanya jamii iishi pamoja bila ya bughudha ili kuondoa mtu asimuonee mwingine, lakini hata kutukana ni kosa la jinai ukisoma sheria za Tanzania.
"Ukitukana mtu hapo mjini Peramiho akikupeleka polisi ukaulizwa nini kimetokea ukasema kanitukana polisi hawezi kuacha atasema eleza ilikuaje, alisemaje, mlianzaje, ndio sheria," ameeleza Wasira.
Kwa mujibu wa Wasira, siku hizi dunia imeanza kutupa tafsiri nyingine ya uhuru, kwamba mkitukanana sana kwenye mitandao ya kijamii ndio uhuru.
"Hebu niulize wazee watuambie hivi huku katika mila na utamaduni watoto walikuwa wanatukana baba zao, walizuiwa na nani, walizuiwa na utamaduni sindio, walikuwa wanamtukana mama yao...walikuwa wamejiwekea utaratibu tofauti na demokrasia ya sasa...
"Mtoto hawezi kusema baba naye amezidi tupige kura kupata baba mwingine, hata akiwa mkorofi wanasema ah! baba naye hata akiwa mlevi wanasema baba naye karudi leo kayanywa lakini hawasemi uongozi wake unakoma wa ubaba, hapo ndipo tulipoanzia.
"Sasa unapopanua demokrasia, tena unapokuja kwenye kitu kipya kinachoitwa vyama vingi vizuri sana lakini na vyenyewe vinaweza kuwa tabu sana, lakini hakuna kisicholuwa na tabu jambo kubwa ni kuweka utaratibu ili vyama hivi vifanye kazi kwa kuzingatia katiba na sheria mliyojiwekea," amesisitiza.
CCM NA FRELIMO KUIMARISHA USHIRIKIANO WA KIUCHUMI
15-03-2026
UZINDUZI WA JENGO LA MAKAO MAKUU YA ULINZI WA TAIFA
15-03-2026
CCM YAIPA POLE MSUMBIJI KWA KUKUMBWA NA MAFURIKO
15-03-2026
INJINI YA CHAMA CHA MAPINDUZI IPO MASHINANI; DKT.MIGIRO
15-03-2026
DK.MIGIRO:CCM INAJENGWA KUANZIA NGAZI YA MASHINA SIO MAJUKWAANI.
15-03-2026
πππ¦πππ‘ππ’ πππ πππ§. π ππππ₯π’ ππππ£π’πππππͺπ ππͺπ π¦πππ‘ππͺπ πππ₯ ππ¦ π¦πππππ
15-03-2026
NAIBU KATIBU MKUU WA CCM BARA AMWAKILISHA KATIBU MKUU WA CCM KWENYE MSIBA WA MBUNGE WA JIMBO LA PERAMIHO
15-03-2026
π©ππππ‘π π§π¨ππππ‘ππ ππ ππ‘π π¬π π‘πππ π¬ππ§π¨ - π πͺππ‘πππ πππ‘ππ‘π
15-03-2026
DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AONGOZA KIKAO MAALUMU CHA KAMATI KUU YA CCM
15-03-2026
RAIS SAMIA AKIWAAPISHA MAWAZIRI NA MANAIBU WAZIRI WATEULE- IKULU CHAMWINO DODOMA
15-03-2026
WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU NCHEMBA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA DODOMA (GENERAL)
15-03-2026
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ..
15-03-2026
RAIS SAMIA AKIHUTUBIA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
15-03-2026
DKT SAMIA:TUNAFANYA UCHAGUZI KWA FEDHA ZETU WENYEWE
15-03-2026
MGOMBEA URAIS KUPITIA CCM DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA MANYARA
15-03-2026
π¨ππππ£πππππ πͺπ πππ§. π¦ππ ππ π¨π ππππ§π ππ ππ‘π ππͺπ πͺππ£ππ‘πππ‘π, πͺππππ¨ππππ πππ
πππ©πππͺ ππ πͺπͺ πΏπ π©. πππππ§π€ ππ¬ππ₯π€π ππ πππ€π£ππ€π―π π¬π πΎππΌπΏπππΌ π£π πΌπΎπ
15-03-2026
πππ§. π¦ππ ππ ππ§π¨π π‘πππ‘π π¬π ππ₯πππ π¬π ππππ’π π
15-03-2026
KATIBU MKUU WA CCM, BALOZI DKT. ASHA-ROSE MIGIRO AKUTANA NA RAIS MWINYI – ZANZIBAR
15-03-2026
ILANI YA UCHAGUZI YA CCM 2025-2030
15-03-2026
WASIRA:CCM HATUKATI MGOMBEA ILA TUNATEUA WACHACHE KATI YA WENGI
15-03-2026