Serikali yaja na Helikopta kukabiliana na Majanga ya Moto
Serikali yaja na Helikopta kukabiliana na Majanga ya Moto
Serikali imedhamiria kufanya maboresho makubwa katika Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ikiwa ni juhudi za kupambana na athari za majanga pindi zitokeapo ajali mbalimbali ikiwemo ajali ya moto ili kuweza kuokoa mali na maisha.Maboresho hayo yanajumuisha ununuzi wa magari ya kuzimia moto yasiyopungua 150,magari 20 ya Kubebea Wagonjwa, Boti za Kisasa 25 za Uokozi na Helikopta Moja Maalumu ya Uokozi.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhandisi Hamad Masauni wakati akizungumza katika Mkutano wa Kuwajengea uwezo Wakuu wa Mikoa yote Tanzania Bara na Makatibu Tawala, ulioandaliwa na Ofisi ya Rais Tawala za Miko ana Serikali za Mitaa (TAMISEMI), katika Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Nyerere, Kibaha mkoani Pwani ambapo pia ulihudhuriwa na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi, Daniel Chongolo.
“Kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hii, Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan inakwenda kufanya uwekezaji mkubwa katika Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ambapo tutashuhudia magari ya Zimamoto na Uokoaji yasiyopungua 150 yakimwagika, Boti Maalumu za Uokozi zisizopungua 25, Gari Maalumu za Kubebea majeruhi (Ambulance) zisizopungua 20, na Helikopta, lengo ikiwa kuokoa mali na Maisha ya Watanzania pindi yanapotokea majanga” alisema Mhandisi Masauni
Waziri Masauni amewaomba pia Wakuu wa Mikoa kuhakikisha kunakuwepo vituo vya kuchotea maji ambayo yatatumika pindi yatokeapo majanga ya moto huku akitaja maeneo mengine ya vipaumbele kwa Jeshi la Zimamoto kuwa ni kuimarisha vitendea kazi vya Zimamoto na Uokoaji, Ujenzi wa Vituo vya Zimamoto pamoja na Nyumba za Makazi ya Askari wa Jeshi hilo na kuwasiliana na Mamlaka za Maji katika mikoa mbalimbali nchini ili kuweza kusimika mabomba ya kuzimia moto(fire hydrants) huku pia serikali ikitenga kiasi cha shilingi milioni 120 kwa ajili ya ukarabati wa vituo vibovu.
“Serikali imeendelea na Ujenzi wa Vituo vya Zimamoto na Uokoaji katika maeneo mbalimbali nchini lengo ikiwa ni kuboresha huduma za uokoaji katika maeneo hayo na katika Mwaka wa Fedha 2023/2024 jumla ya Shilingi Bilioni 2 zimetengwa kwa ajili ya Ujenzi na Uendeshaji wa Vituo Saba vya Zimamoto na Uokoaji katika mikoa ya Songwe, Simiyu, Manyara, Kagera, Katavi, Geita na Njombe, vilevile Shilingi Milioni 400 zimetengwa kwa ajili ya Ukarabati wa Nyumba 10 za Makazi ya Askari katika mikoa ya Arusha, Morogoro na Iringa”
DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AONGOZA KIKAO MAALUMU CHA KAMATI KUU YA CCM
09-12-2025
RAIS SAMIA AKIWAAPISHA MAWAZIRI NA MANAIBU WAZIRI WATEULE- IKULU CHAMWINO DODOMA
09-12-2025
WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU NCHEMBA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA DODOMA (GENERAL)
09-12-2025
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ..
09-12-2025
RAIS SAMIA AKIHUTUBIA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
09-12-2025
DKT SAMIA:TUNAFANYA UCHAGUZI KWA FEDHA ZETU WENYEWE
09-12-2025
MGOMBEA URAIS KUPITIA CCM DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA MANYARA
09-12-2025
π¨ππππ£πππππ πͺπ πππ§. π¦ππ ππ π¨π ππππ§π ππ ππ‘π ππͺπ πͺππ£ππ‘πππ‘π, πͺππππ¨ππππ πππ
πππ©πππͺ ππ πͺπͺ πΏπ π©. πππππ§π€ ππ¬ππ₯π€π ππ πππ€π£ππ€π―π π¬π πΎππΌπΏπππΌ π£π πΌπΎπ
09-12-2025
πππ§. π¦ππ ππ ππ§π¨π π‘πππ‘π π¬π ππ₯πππ π¬π ππππ’π π
09-12-2025
KATIBU MKUU WA CCM, BALOZI DKT. ASHA-ROSE MIGIRO AKUTANA NA RAIS MWINYI – ZANZIBAR
09-12-2025
ILANI YA UCHAGUZI YA CCM 2025-2030
09-12-2025
WASIRA:CCM HATUKATI MGOMBEA ILA TUNATEUA WACHACHE KATI YA WENGI
09-12-2025
WANACHAMA 280 WA CHADEMA WATIMKIA CCM
09-12-2025
BALOZI NCHIMBI: MAONI YOYOTE KUHUSU AMANI YA TANZANIA HAYATAPUUZWA
09-12-2025
π¦ππ₯πππππ π¬π π₯πππ¦ πππ§. π¦ππ ππ ππ ππͺπππ ππππ π π¬π π πππ‘πππππ’ ππππ π¦ππππ π¨ - ππ£π. ππ π’π¦ π ππππππ
09-12-2025
MAKALLA: BARABARA YA MPWAPWA NJIAPANDA KONGWA KUJENGWA LAMI
09-12-2025
BALOZI NCHIMBI AWASILI ARUSHA
09-12-2025
TAARIFA KWA UMMA
09-12-2025
UCHAGUZI MKUU SIO AJALI-WASIRA
09-12-2025
πͺπππ¨π ππ π π¦ππππππ¨π π©ππ’π‘ππ’ππ ππππππππ ππͺππ‘π¬π ππ¨π₯π ππ π ππ’π‘π - (π ππ) πππ©π¨
09-12-2025